Safari ya SingidaSafari ya Singida

HAKUNA kulala! Ndivyo unavyoweza kusema kwani licha ya kusimama kwa ligi kupisha mashindano ya kimataifa, ambapo timu mbalimbali za Taifa zinaendelea na ratiba ya michezo ya kufuzu mashindano mbalimbali ikiwemo timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, ambayo itavaana na Morocco siku ya Jumanne, kikosi cha Simba tayari kimerejea kambini kujiandaa na mchezo wao wa Kombe la FA, huku watani zao wa jadi Yanga nao wakisafiri mpaka Singida kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida Bigstars.

Kumbuka kuwa kupitia Kampuni bora ya kubashiri michezo ya SportPesa unaweza kujishindia mamilioni kwa kuweka ubashiri wako kupitia uchaguzi wa ‘odds’ za kibabe.

Unahisi jambo gani walikuwa wanaongea hapa #WenyeNchi #NguvuMoja
Wachezaji wa Simba

Ikumbukwe kuwa Simba wana mchezo muhimu dhidi ya Bigman katika hatua ya 16 bora ya mashindano ya CRDB Federation Cup utakaopigwa Machi, 27 katika Uwanja wa KMC Complex saa 10 jioni.

Simba wanauelekea mchezo huu wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji, ambao ulipigwa Machi 14 mwaka huu ambapo mara tu baada ya mchezo huo wachezaji walipewa mapumziko ya siku chache.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Bigman kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza safari ya kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry utakaopigwa Aprili 2.

TUJIKUMBUSHE 6-0 ZA DODOMA ZILIKUWAJE?

Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika Uwanja wa KMC Complex ambapo, Elie Mpanzu aliipatia timu hiyo bao la kwanza dakika ya 15 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Kibu Denis.

Jean Charles Ahoua aliipatia bao la pili dakika ya 21 kwa shuti la chini chini akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’, Ahoua pia aliipatia bao la tatu dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na Kibu.

Steven Mukwala aliifungia bao la nne kwa kisigino dakika ya 46 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mpanzu. Karamu ya mabao iliendelea mara baada ya Kibu kuipatia bao la tano dakika ya 54 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Mpanzu. Kibu pia aliipatia bao la sita dakika ya 69 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ahoua.

Ushindi huo uliwafanya kufikisha pointi 57 wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ambapo wanazidiwa alama moja na vinara Yanga.

Kikosi cha Simba kilichohusika katika mchezo huo;

Ally (Abel 61′), Duchu (Kijili 82′) Zimbwe Jr (Nouma 82′) Chamou, Hamza, Kagoma, Kibu, Ngoma (Mavambo 61′) Mukwala (Ateba 77′) Ahoua, Mpanzu

Kikosi cha Dodoma kilichohusika katika mchezo huo;

Ngeleka, Augustino, Apollo, Hoza (Banda 49′) Milandu (Mwaterema 49′), Mwana, Mhilu, Mukrimu, Lusajo, Obata (Ajibu 49′) P. Peter

MASTAA 8 WAKOSEKANA KAMBINI SIMBA

Licha ya kikosi cha timu hiyo kuingia kambini lakini inawakosa mastaa wao nane ambao wameitwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa ambapo stia kati ya hao wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco.

Mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa nchini Morocco, Machi 25 kufuatia ile ya kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam, Novemba 21, 2023 na Stars kupoteza kwa mabao 2-0. Nyota hao sita wa Simba ni mlinda mlango Ally Salim, walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Abdulrazak Hamza. Wengine walioitwa ni pamoja na viungo Yusuph Kagoma na Kibu Denis.

STARS NAO WATUA MOROCCO

Kikosi cha Timu ya Taifa @taifastars- kimefanya mazoezi kwenye uwanja wa Mkwakwani- Tanga kujiandaa na mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia ---- dhidi ya Morocco utakaochezwa Machi --- ---- Oujda- Morocco
Mazoezi ya Taifa Stars

Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ tayari imewasili nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa Kundi E wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wenyeji Morocco utakaochezwa Machi 25, 2025.

YANGA HAOO SINGIDA

Safari ya Singida imeanza Wananchi wa Singida watafurahi #timuyawananchi#daimambelenyumamwiko (-)
Safari ya Singida imeanza Wananchi

Kikosi cha Yanga leo Jumapili kimeondoka Dar es Salaam kwenda Singida kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida Black Stars ambao unatarajiwa kufanyika kesho Jumatatu mkoani Singida, kama sehemu ya sherehe za ufunguzi wa uwanja wa Airtel Stadium.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.