Taarifa ya kushtua ambayo imeripotiwa na majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii na kuthibitishwa na uongozi wa Yanga zimeeleza kuwa kocha mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na timu hiyo, huku ikielezwa yupo kwenye rada za kutua nchini Algeria kwenye klabu ya CR Belouzdad.

Ikumbukwe Ramovic alichukua jukumu la kuiongoza Yanga mwezi Novemba mwaka jana 2014 na hii ni mara baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho Muargentina, Miguel Gamondi.
Kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya kocha mkuu mpya, Miloud Hamdi mwenye asili ya nchini Argentina na Ufaransa.
MJADALA WA WAAMUZI WATIKISA
Achana na taarifa ya hivi punde ya, Ramovic kushtua wengi, siku ya leo kwenye vijiwe vya michezo kumekuwa bize hasa kwa mtifuano wa hoja kuhusu mjadala mkali wa makosa ya waamuzi na kushuhudia mpaka wakuu wa idara za habari za timu zote mbili, Ali Kamwe na Ahmed Ally kuchapisha maandiko yaliyotafsiriwa kujibizana kuhusu jambo hilo.
YANGA KUWAVAA KENGOLD JUMATANO HII
Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuendelea tena rasmi siku ya kesho Jumatano ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga wanatarajia kushuka uwanjani kuvaana na KenGold katika mchezo unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa Yanga katika duru hii ya pili ya Ligi Kuu Bara ambapo Yanga wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wao uliopita.
Kumbuka unaweza kushinda mamilioni kwa kuweka ubashiri wako wa mchezo huu na michezo mingine mingi kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambayo inakupa ‘odds’ kubwa kwa kutembelea tovuti hii; www.sportpesa.co.tz
KOCHA YANGA ANATAKA MATOKEO

Akizungumzia mchezo huo kabya ya kutangazwa kuachana na Yanga kocha, Ramovic amesema: “Kesho tutakabiliana na timu ambayo imepata wachezaji wapya wengi. Pia Kocha wao ana mtindo wake wa kucheza, na itakuwa mechi ngumu kwa sababu hatujui jinsi wanavyocheza na wachezaji wapya wote kwenye timu. Lakini huenda, kama tulivyokabiliana na wapinzani wa mwisho, watacheza kwa kujilinda zaidi. Hiyo inamaanisha tunapaswa kutafuta nafasi na mianya ili tuweze kupata matokeo.
“Tunahitaji kujaribu kucheza kati ya mistari. Tunapaswa kucheza katika nafasi ndogo nyuma ya safu ya ulinzi. Tunahitaji kuwasambaza ili tuweze kupata nafasi kati ya mistari. Kwa ujumla, itakuwa mechi ngumu tena, lakini kama ninavyosema kila wakati, sisi ni timu bora zaidi nchini Tanzania. Tumeshinda taji mara tatu, na tunataka kushinda tena.
“Nadhani tumeboresha mambo mengi tangu nilipokuja, na bila shaka tunahitaji kuwa makini zaidi katika safu ya ushambuliaji. Katika mechi za mwisho, tulifunga mabao mengi na tulipata nafasi nyingi mbele ya goli. Hii ni moja ya nguvu zetu, lakini tunapaswa kuwa na umakini zaidi katika kumalizia na kujaribu kufunga mabao zaidi, kwa sababu tunataka kuwa bora katika kila kitu tunachofanya.”
MASTAA WAPYA KENGOLD WAMSHTUA MSHERY

“Maandalizi yetu kwa ujumla yapo vizuri, tumejiandaa vizuri kwenda kucheza mchezo wetu dhidi ya KenGold. Wamesajili wachezaji wengi wazoefu ukilinganisha na mzunguko wa kwanza, na kwetu sisi hiki ni kitu kizuri maana mechi itakuwa nzuri sana maana wana wachezaji wazoefu na wachezaji wanaojua.
“Tutaboresha uwezo wetu kwenye mchezo huu unaofuata na michezo inayokuja, Ligi si rahisi timu nyingi zinazokuja kwenye huu mzunguko wa pili wanajilinda sana kutokufungwa kwa hiyo nyingi zinaona bora kupata sare kuliko kupoteza alama zote tatu, walimu wanaliona hilo na wanalifanyia kazi,” amesema mlinda mlango wa Yanga, Aboutwalib Mshery.
Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa inakamatia nafasi ya pili kwenye msimamo wakijikusanyia pointi 42. Mchezo wa kwanza Yanga wakicheza ugenini waliitandika KenGold bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Michezo mingine itakayopigwa Februari 5, ni Tabora United v Namungo, ambapo baada ya kumalizana na Simba, Tabora United wamebaki hapohapo nyumbani kumalizana na Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda. Namungo wapo nafasi ya 12 wakiwa na pointi 17.
Mechi nyingine ni Dodoma Jiji v Pamba, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Dodoma Jiji ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 19 inakutana na Pamba iliyo nafasi ya 14 na pointi 12.
