Yanga Vs TP MazembeYanga Vs TP Mazembe

NI vita ya kisasi na rekodi leo Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga watashuka Uwanjani kuwakaribisha wageni wao kikosi cha TP Mazembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Unaweza kubashiri mechi hizi kwa kuweka ubashiri wako kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa tembelea tovuti ya www.sportpesa.co.tz

Mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa majira ya saa 10:00 jioni unatarajiwa kuwa wa kisasi kwa TP Mazembe ambao wataingia na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 3-1 katika mchezo wa mwisho timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, lakini kwa Yanga itakuwa vita ya rekodi ambapo watakuwa wanapambana kuendeleza ubabe wao kwa TP Mazembe.

YANGA
Mastaa wa Yanga wakijiandaa kuivaa TP Mazembe

Ikumbukwe katika michezo mitatu iliyopita dhidi ya TP Mazembe, Yanga haijapoteza mchezo wowote wakiwa wameshinda mechi mbili na kupata sare mchezo mmoja.

YANGA WANASEMAJE?

YANGA
Ali Kamwe

Kuelekea katuika mchezo huo, Ali Kamwe ambaye ni Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa maandalizi yameendelea vizuri na kuwa hawaangalii tu, mchezo dhidi ya TP Mazembe, bali mechi zao zote tatu za kimataifa walizosaliwa nazo wakianza na mchezo wa nyumbani dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa leo Jumamosi huku ukitarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

“Tutakuwa nyumbani kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya TP Mazembe kikubwa ni kuona tunapata pointi tatu kwani tutakuwa nyumbani na wachezaji wanatambua kwamba huu ni mchezo muhimu, nasi tutapambana kwa ajili ya kuona kwamba tunapata matokeo mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwapa nguvu wachezaji.

“Maandalizi yetu yameanza mapema ambapo safari hii tunaanza kwa shabiki mmojammoja kwenye maandalizi kisha wachezaji na benchi la ufundi, yaani hii mechi kila mmoja anahusika na kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri kwa kupata pointi tatu.

“Wapinzani wetu tunawaheshimu unaona kwenye mechi ambazo zimepita Desemba tumekuwa na mwendelezo mzuri na malengo ni kuona hii kasi inaendelea bila kupoa, mashabiki tuendelee kuwa pamoja na tushikamane kwenye mechi hii muhimu, lakini maandalizi haya ni kwa ajili ya mechi zote za kimataifa.”

RATIBA YA MECHI ZA YANGA KIMATAIFA

Januari 4, 2025 dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni ambapo wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya bao 1-1  walipokutana mchezo uliopita, Yanga ilipata bao la jioni kupitia kwa Prince Dube.

Januari 15, 2025 itakuwa dhidi ya Al Hilal ambapo Yanga watakuwa ugenini nchini Mauritania ngoma inatarajiwa kupigwa saa 4:00 usiku, walipokutana mchezo uliopita Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.

Yanga v MC Alger hii itapigwa Uwanja wa Mkapa Januari 18, 2025 saa 10:00 jioni ugenini Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 hivyo kwa ratiba hii mechi mbili za Yanga itakuwa nyumbani na mchezo mmoja itakuwa ugenini.

SIMBA WATUA TUNISIA KIBABE

Wawakilishi wengine wa Tanzania kimataifa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika Simba tayari wamewasili salama katika mji wa Tunis nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien utakaopigwa Januari 5.

Kikosi cha Simba kiliondoka jijini Dar es Salaam kikipitia Instanbul, Uturuki kabla ya kuunganisha Ndege kuelekea Tunisia. Timu imeondoka na msafara wa watu 50 huku wachezaji wakiwa 22 ambao tunaamini wapo tayari kuipambania timu kupata matokeo chanya.

KUCHEZWA BILA MASHABIKI

Mchezo huo ambao utapigwa kesho Jumapili Januari 5, 2025 saa moja usiku kwa saa za Tanzania hautakuwa na mashabiki kutokana na CS Sfaxien kufungiwa baada ya kufanya vurugu viwanjani.

MAZOEZI YA SIMBA BALAA

YANGA
Mazoezi ya mastaa Simba kuivaa Sfaxien

Kikosi cha Simba tayari kimefanya mazoezi Tunisia tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien. Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa nje wa Olympique De R – Tunis ambao ndio utatumika kwa ajili ya mchezo wa siku ya Jumapili saa moja usiku kwa saa za Tanzania.

Wachezaji wote 22 waliosafiri kwa ajili ya mchezo huo wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo kwenye hali nzuri huku wakiendelea kuzoea hali ya hewa. Akizungumzia hali ya kikosi tangu tulivyowasili Tunisia jana jioni, Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kila kitu kinaendelea vizuri na hali ya hewa sio baridi kali na haitakuwa kikwazo siku ya mchezo.

“Leo tumeanza mazoezi kwa siku ya kwanza, tutaendelea kesho pamoja na Jumamosi kabla ya kushuka dimbani Jumapili. Maandalizi kwa ujumla yanaendelea vizuri na jambo la kushukuru baridi sio kali kama tulivyoenda Algeria kwahiyo tunaamini tutakuwa na nafasi nzuri ya kupata matokeo chanya,” amesema Ahmed.

 

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.