Spurs Vs Man UnitedSpurs Vs Man United

Tottenham leo majira ya saa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki wanatarajia kuwa wenyeji wa Manchester United katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Carabao, ambapo taarifa mbaya kwa mashetani wekundu ni kuwa wanatarajia kumkosa straika wao, Marcus Rashford. Unaweza kushinda pesa kwa kubashiri matokeo ya mchezo huu kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubahatisha kwa kuingia kwenye tovuti hii www.sportpesa.co.tz

UNITED
Marcus Rashford

Spurs wataingia katika mchezo huo wakiwa na malengo makubwa ya kurudia historia yao ya mafanikio makubwa ya mashindano hayo mwaka 2008. Huku msimu huu kocha mkuu wa timu hiyo akiwa amewaahidi mashabiki kupambania angalau kushinda kombe moja.

MAN UNITED CHINI YA UTAWALA WA KOCHA MPYA

Kikosi cha United kinaingia katika mchezo huo wakiwa na utawala mpya wa benchi la ufundi ambalo kwa sasa liko chini ya Mreno, Ruben Amorim ambaye amechukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa kikosi cha timu hiyo, Erick Ten Hag ambaye pia aliwahi kubeba ubingwa wa mashindano haya katika msimu wake wa kwanza akiwa na United.

Ikiwa Amorim atashinda mchezo wa leo basi atakuwa amesaliwa na michezo miwili tu, ili kukata tiketi ya kucheza fainali ya mashindano hayo.

REKODI ZINAWABEBA SPURS.

UNITED
Baadhi ya mastaa wa Spurs

Timu hizo zinakutana wakati huu rekodi za michezo yao iliyopita ikiwa inaibeba zaidi Spurs ambao hawajapoteza mchezo wowote kati ya michezo yao minne ya Ligio Kuu England iliyopita wakifanikiwa kushinda michezo miwili na kupata sare michezo miwili iliyosalia.

Ikumbukwe mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye ligi msimu huu, Spurs walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. Ikiwa Spurs wataibuka na ushindi katika mchezo wa leo basi wataandika rekodi mpya ambayo haijawahi kufikiwa tangu mwaka 1990 ya kushinda michezo mitatu mfululizo.

UNITED
Baadhi ya mastaa wa Spurs

Kwenye mashindano haya katika mara sita ambazo timu hizi zimekutana kwenye hatuaya mtoano kila timu imefanikiwa kuiondosha timu nyingine mara 3, huku United wakiwa na rekodi ya kushinda kombe hilo kati ya mara mbili ambazo waliitoa Spurs.

HALI YA VIKOSI IKOJE?

Tottenham

Mpaka sasa Spurs wanapitia kipindi kigumu cha kuwa na kundi kubwa la majeruhi katika nafasi mbalimbali uwanjani. Huku mlinda mlango wao Guglielmo Vicario akiendelea kuuguza majeraha, kipa Fraser Forster anatarajia kuanza langoni leo.

Licha ya kiwango bora alichoonyesha, Djed Spence wikiendi iliyopita lakini, Pedro Porro anatarajia kuanza nafasi ya mlinzi wa kulia, upande wa kushoto, Destiny Udogie anatarajiwa kuendelea kuwa chaguo la kwanza.

Micky van de Ven na Cristian Romero wote wana maumivu ya nyama za paja, hivyo inatarajiwa, Radu Dragusin na Archie Gray wataanza kwenye nafasi ya kiungo wa ulinzi.

Rodrigo Bentancur anatumikia adhabu ya kufungiwa, hivyo Yves Bissouma na Pape Matar Sarr wataanza kwenye kiungo cha juu. Heung-min Son alipata majeraha madogo na kuna hofu ikiwa anaweza kuwa sehemu ya mchezo wa leo.

James Maddison ambaye amekuwa na wakati mzuri akifunga mabao mawili kwenye mchezo uliopita anatarajia kuanza juu pamoja na Dejan Kulusevski na Dominic Solanke.

Manchester United

UNITED
Leny Yoro

Mpaka sasa, Andre Onana hana mpinzani kwenye lango la Manchester United lakini huenda kukawa na mabadiliko kidogo ya kikosi. Leny Yoro anatarajiwa kuchukua nafasi ya, Harry Maguire. Noussair Mazraoui alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya City hivyo huenda akakosekana kwenye mchezo wa leo halia mabayo inatarajiwa kuleta mabadiliko ya kimfumo kwa, Amad Diallo kucheza kama ‘wing-back’ wa kulia.

Diogo Dalot anatarajia kuanzia upande wa kushoto, Kobbie Mainoo na Manuel Ugarte kwenye kiungo cha ulinzi, Bruno Fernandes na Alejandro Garnacho huenda wakacheza nyuma ya straika wao, Rasmus Hojlund.

DONDOO MUHIMU

UNITED
Baadhi ya mastaa wa Man United

Tottenham Hotspur wamefanikiwa kusonga mbele katika michezo yao minne iliyopita ya robo fainali waliyotinga. Hii ni tangu wapoteze kwa kipigo cha 2-1 kutoka kwa West Ham msimu wa 2013-14.

Manchester United ndio vinara wa kufunga mabao mengi kwenye mashindano ya mwaka huu wakiwa wameshaweka kambani mabao 12 huku wakishinda kwa idadi ya mabao  5+ katika michezo miwili (7-0 vs Barnsley, 5-2 vs Leicester).

Ushindi katika michezo miwili iliyopita ya United katika mashindano haya ulikuwa chini ya makocha tofauti akianza, Ten Hag 7-0 vs Barnsley na baadae Ruud van Nistelrooy.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.