HELLO Desemba baada ya kuanza Januari sasa ni Desemba ndani ya 2024 ikiwa kuna funga kazi za kibabe kwa watani wa jadi Yanga na Simba kwa kila timu kuvuja jasho dakika 90 kusaka ushindi ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.
Yanga inayodhaminiwa na SportPesa hawa ni mabingwa watetezi ambapo walitwaa taji msimu wa 2023/24 zama za Miguel Gamondi ambaye amekutana na Thank You na sasa timu ipo chini ya Kocha Mkuu Sead Ramovic.

Ikiwa ni muda wa funga mwaka basi acha Desemba pochi livimbe kwa maokoto yakutosha kwa kubashiri kupitia SportPesa mechi za ligi pendwa itakuwa kicheko kwako timu yako inashinda na wewe unashinda mkwanja mrefu kabisa.
GARI LIMEWAKA KWA YANGA
Yanga kwenye mechi tatu mfululizo ngoma ilikuwa nzito kwa kukosa matokeo mazuri ila kwenye mchezo wa nne geri iliwaka ugenini wakakomba pointi tatu muhimu mazima mbele ya Namungo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.
Ikumbukwe kwamba katika mechi tatu mfululizo ngoma ilikuwa nzito kimataifa mchezo mmoja na kwenye Ligi Kuu Bara ilikuwa kwenye mechi mbili na matokeo ilikuwa Yanga 0-1 Azam FC kisha Yanga 1-3 Tabora United.
Mchezo wa kwanza kwa mrithi wa mikoba ya Gamondi ilikuwa Uwanja wa Mkapa na baada ya dakika 90 ilikuwa Yanga 0-2 Al Hilal huu ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi pointi tatu zilisepa mazima.
Tayari msafara wa wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la Yanga wametua Dar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mechi zijazo kitaifa na kimataifa ambapo mchezo wao dhidi ya Namungo walikuwa Ruangwa, Uwanja wa Majaliwa kusaka pointi tatu muhimu.
KETE ZA YANGA DESEMBA 2024

Kituo kinachofuata ndani ya Yanga itakuwa kimataifa kwenye mchezo wa hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Desemba 7 2024 Yanga inatarajiwa kuwa na kibarua dhidi ya MC Alger.
Huu utakuwa ni mchezo wa pili kwenye hatua ya makundi. Wakimaliza ugenini kimataifa kete ya tatu itakuwa Desemba 14 dhidi ya TP Mazembe kwa mara nyingine Yanga watakuwa ugenini kwenye anga la kimataifa kusaka pointi tatu muhimu.
Desemba 19 itakuwa dhidi ya Mashujaa mchezo wa ligi unatarajiwa kuwa mchezo wa kwanza ndani ya Uwanja wa KMC, Complex baada ya kuhama Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za ushindani.
Desemba 22 2024 itakuwa ni Yanga v Tanzania Prisons huu pia ni NBC Premier League Uwanja wa KMC Complex. Desemba 25 itakuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji watakuwa ugenini na funga kazi ni Desemba 29 2024 dhidi ya Kagera Sugar, watakuwa nyumbani.
SIMBA FUNGA KAZI HII HAPA

Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika wanakete tano za kazi kufungwa mwaka 2024 katika mechi za ushindani ambazo ni dakika 450 za kazikazi uwanjani.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa kufunga Novemba ilikuwa katika kombe la Shirikisho Afrika walipopata ushindi wa bao 1-0 Bravos, Uwanja wa Mkapa ilikuwa Novemba 27 2024.
Desemba 8 2024 watakuwa kimataifa dhidi ya CS Constantine ugenini, Desemba 15 itakuwa Simba v Sfaxine kimataifa Uwanja wa Mkapa. Desemba 18 itakuwa dhidi ya Ken Gold, NBC Premier League Uwanja wa KMC, Desemba 21 itakuwa dhidi ya Kagera Sugar ugenini na funga kazi itakuwa ugenini dhidi ta Tabora United.
Mchezo dhidi ya Tabora United unatarajiwa kuchezwa Desemba 28 2024 Simba itakuwa ugenini ambapo timu zote mbili zitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.
SEMAJI NENO LAKE HILI HAPA

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa wanakazi kubwa kufanya kusaka ushindi katika mechi zao hivyo watapambana kupata matokeo mazuri kwa kuwa inawezekana.
Simba wameanza maandalizi kuelekea mchezo wao wa kimataifa ugenini dhidi ya Constantine ya Algeria unaotarajiwa kuchezwe Desemba 8 ambapo watakuwa ugenini.
Ally amesema: “Kikosi chetu kinaendelea na program ya mazoezi kujiandaa na mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Constantine ya Algeria. Mipango ipo vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu muhimu.”

