Yusuph KagomaYusuph Kagoma
SIMBA
Moussa Camara

Kikosi cha Simba leo Jumatano kinatarajia kushuka uwanjani kwa ajili ya kuvaana na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam.

Unaweza kuweka ubashiri wako wa mchezo huu kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kutembelea tovuti www.sportpesa.co.tz 

Katika mchezo huo Simba wanatarajiwa kuwa wenyeji kikanuni, ambapo wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wao wa wikiendi iliyopita walipocheza ugenini dhidi ya Mashujaa mkoani Kigoma.

Kuelekea katika mchezo huo Kocha mkuu wa Simba, Fadlu Davis ameweka wazi kuwa wanatarajia kukosa huduma ya nyota wao watatu ambao ni Valentino Mashaka, Yusuph Kagoma na Abdalazak Hamza huku Joshua Mutale naye akiwekwa kwenye uangalizi maalum.

Kocha huyo pia ameweka wazi kuwa mchezo huo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakuwa mgumu kutokana na kukutana na timu bora. Ambapo amekiri ubora wa kikosi cha KMC pamoja na kocha wao lakini ametamba kuwa nao wamejiandaa vizuri kuwakabili na kuondoka na pointi zote tatu.

‘’Tunatarajia mchezo mgumu dhidi ya KMC hasa kutokana na ubora ambao wanao kama kikosi na ubora wa benchi lao la ufundi, lakini kama ambavyo nimekuwa nikisema mara zote kuwa sisi ni Simba n ani lazima tuweke malengo ya pointi 3 muhimu katika kila mchezo na ndivyo ilivyo kuelekea mchezo huu.

‘’Kikosi kipo kwenye hali nzuri na kimepata siku nne za maandalizi kuelekea mchezo huu ambao utaanza saa 10 jioni katika Uwanja wa KMC Complex,” amesema Fadlu.

SIMBA ITAWAKOSA WANGAPI?

SIMBA
Fadlu Davis

Akizungumzia hali ya kikosi kocha Fadlu amesema kiungo mshambuliaji, Joshua Mutale alipata maumivu katika mchezo dhidi ya Mashujaa lakini itategemea na vipimo vya daktari kama atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa KMC.

“Mutale alipata maumivu lakini anaendelea vizuri, Abdulrazack Hamza ameanza mazoezi ingawa hayupo tayari kwa mchezo wa kesho, Yusuph Kagoma na Valentino Mashaka wao bado ni majeruhi,” amesema Kocha Fadlu.

SIKU NNE ZA MAPUMZIKO ZIMEIBEBA SIMBA

Kocha, Fadlu ameongeza kuwa kikosi chake kipo kwenye hali nzuri hasa mara baada ya kupata siku nne za maandalizi kuelekea mchezo huo, huku akitamba kuwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri na kupata matokeo.

“Itakuwa mechi ngumu na nzuri, aina soka wanalocheza KMC halitofautiani sana na sisi. Wana timu bora lakini sisi tupo vizuri pia na tumejipanga kuhakikisha tunapata alama zote tatu,” amesema Kocha Fadlu.

AWESU AWAITA MASHABIKI WA SIMBA

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji wa Simba, Awesu Awesu amewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani leo, ili kuwapa sapoti ambayo itawasaidia kupatikana kwa pointi tatu.

“Mashabiki ni wachezaji wa 12 tunawahitaji sana kwenye mchezo wa leo, nasi kama wachezaji tumejipanga kuhakikisha tunawapa furaha,” amesema Awesu.

SIMBA MAZOEZI YA MWISHO NI BUNJU

SIMBA
Jean Ahoua

Kuelekea mchezo huo dhidi ya KMC utakaopigwa leo Jumatano, jana Jumanne kikosi cha Simba kilifanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena.

Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kuwa wachezaji wote ambao wapo kwenye mpango wa mechi hiyo wamefanya mazoezi hayo kikamilifu na wapo tayari kwa mchezo wa leo.

Kama ilivyo kawaida katika michezo iliyopita katika mazoezi hayo ya jana Jumanne yaliongozwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids na mpaka yanakamilika hakukuwa na mchezaji yoyote ambaye alipata maumivu ambayo yangeweza kumfanya kuukosa mchezo wa leo Jumatano.

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa unajua utakuwa mchezo mgumu, lakini wametamba kuwa wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika Uwanja wa nyumbani. Uongozi huo pia umeweka wazi kuwa kikosi kina ari kubwa ya kupata matokeo ya ushindi hasa mara baada ya kutoka kwenye kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao moja ambao waliupata kwenye mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Mashujaa mkoani Kigoma.

Ikumbukwe ni goli pekee la straika raia wa Uganda, Steven Mukwala akitumia pasi ya mpira wa kona wa kiungo, Awesu Awesu dakika ya mwisho ya mchezo ndilo ambalo liliwapa ushindi pekee Wanasimba mkoani Kigoma.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.