WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Yanga na Simba wamewatambua wapinzani wao kwenye hatua ya makundi 2024/25 ambapo kila timu itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mechi tatu nyumbani na tatu ugenini.
Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo huko itakuwa na kibarua cha kupeperusha bendera ya Tanzania katika anga hilo baada ya matajiri wa Dar, Azam FC kugotea kwenye hatua ya awali.

Simba ni kwenye Kombe la Shirikisho huko ni Coastal Union ya Tanga hii iligotea hatua ya awali hivyo ni mwendo wa wawakilishi hawa kufanya vizuri kimataifa kutokana na ushindani kuwa mkubwa.
YANGA KUNDI A
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ilikuwa Pot 2 lilikuwa na timu za CR Belouizdad, Yanga na Pyramids. Pot 1 lilikuwa na :-Al Ahly, E.S.T Tunis, MSFC na TP Mazembe. POT 3 ilikuwa Al Hilal ya Sudan, Orlando Pirates ya Afrika Kusini, GDSE, ASFAR. Pot 4 ilikuwa na MC Alger, Maniema Union, Djoliba AC, Stade d’Abidjan.
KUNDI A LENYE YANGA

TP Mazembe
Yanga
Al Hilal
MC Alger
KUNDI B
Mamelod Sundowns, (MSFC)
Raja Casablanca
ASFRA
Maniema Union
KUNDI C
Al Ahly
CR Belouizdad
Orlando Pirates
Stade d’Abidjan
KUNDI D
E.S.T Tunis
Pyramids
GDSE
Djoliba AC
SEMAJI LA YANGA
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mashindano hayo watafanya kazi kubwa kupambana kupata matokeo mazuri kimataifa.
“Tunatambua mechi hizi ni ngumu na ushindani mkubwa kikubwa ni maandalizi mazuri na kupata matokeo chanya hilo inawezekana ambapo kila mchezaji anahitaji kuona tunapata ushindi na kufikia malengo.”
HAWA HAPA SIMBA KIMATAIFA

Simba kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika imepangwa kundi A baada ya droo hiyo kuchezeshwa nchini Misri. Itakuwa na CS Sfaxien, CS Constantine na FC Bravos do Maquis. Kundi B lina RS Berkane, Stade Malien, Stellenbosch, CD Luanda. Kundi C USM Alger, ASEC Mimosas, ASC Jaraaf, Orapa United.
Kundi D lina Zamalek, Al Masry, Enyimba, Black Bulls. Ambapo kila timu ni bora ndani ya uwanja kwenye kusaka ushindi kimataifa.
Simba itakuwa Kundi A na ilikuwa POT 1 lililokuwa na RS Berkane, Zamalek, Simba, USM Alger ambazo hizi hazitakuwa pamoja kwenye makundi na POT 2 lilikuwa na ASEC Mimosas, Stade Malien, Al Masry na CS Sfaxine, POT 3 lilikuwa na Enyimba, ASC Jaraaf ambazo hizi hazitakutana.
SEMAJI LA SIMBA
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa watafanya kazi kubwa kwenye anga la kimataifa ili kupata matokeo mazuri kwa namna ambavyo wameliona kundi wanahitaji kuona wanamaliza kundi likiwa halijabadilika.
“Tumeliona kundi letu namna ambavyo lipo na tunakwenda kupambana kwenye mechi zetu zote kimataifa kwa kuwa tuna kikosi imara chenye ushindani na hilo linawezekana kuelekea kwenye mechi zetu ambazo tunakwenda kucheza.
“Kama ambavyo kundi limeanza kwa sasa tunahitaji kuona linafika mwisho ikiwa haijabadilika kitu sisi tukiwa namba moja kwenye msimamo kuna pointi zetu nje ndani kutoka kwa wapinzani wetu hivyo ni muda wetu kwenda kufanya kazi kimataifa.
“Ubaya ubwela unakwenda kufanya kazi kimataifa kwani mpango wetu ni kuona kila mchezo tunapata matokeo mazuri na muda ni sasa benchi la ufundi linatambua uimara na mapungufu ya wachezaji ambayo yatafanyiwa kazi kupata matokeo kwenye mechi zetu.”
MAKUNDI A-D HAYA HAPA
KUNDI A

Timu ambazo zimepangwa na Simba katika kundi A ni CS Faxien ya Tunisia, CS Constantine ya Algeria na FC Bravos ya Angola. Kumbuka FC Bravos walimtoa Coastal Union ya Tanzania kwa katika hatua ya awali.
Katika Kundi A Simba wapo na CS Faxien ambao ni mabingwa mara tatu wa kombe hilo mwaka 2003, 2007 na 2008.
HAYA HAPA MAKUNDI MENGINE
KUNDI B
RS Berkane
Stade Malien
Stellenbosch
CD Luanda
KUNDI C
USM Alger
ASEC Mimosas
ASC Jaraaf
Orapa United
KUNDI D
Zamalek SC
Al Masry
Enyimba FC
Black Bulls

