TRA United SC vs Dodoma Jiji FC | Singida Black Stars vs Polisi Tanzania | Ratiba, matokeo, msimamo | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

August 29, 2026
TRA United SC vs Dodoma Jiji FCTRA UnitedTRA United
  • TRA United SC vs Dodoma Jiji FC NBC Premier League 2026/27 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
  • Singida Black Stars vs Polisi Tanzania itapigwa saa 12:30 Uwanja wa Airtel
  • Tumekuletea ratiba ya mzunguko wa 4, matokeo na msimamo

Kazi inaendelea kuelekea TRA United SC vs Dodoma Jiji FC ni mchezo unaofuata kwenye ratiba ya NBC Premier League. Wababe hawa watakutana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Agosti 29, 2026. Saa 10:00 jioni ni muda rasmi wa mchezo kupigwa.

Ijue ratiba ya TRA United: TRA United FC: fixtures, results, table, squad and latest news

SportPesa Aviator Maximum Payout – TZS Million

Taarifa muhimu TRA United vs Dodoma Jiji FC

TRA United SC vs Dodoma Jiji FC
Yassin Mzamiru kiungo wa TRA United.

Mjue Kocha Mkuu wa TRA United: Tabora United Head Coach- Etienne Ndayiragije: Biography, Coaching Career, Achievements and Latest News

Mchezo: TRA United vs Dodoma Jiji FC

Uwanja: Sheikh Amri Abeid

Muda: Saa 10:00 jioni

Siku: Jumamosi

Mashindano: NBC Premier League

Ratiba ya mechi nyingine Agosti 29, 2026

Singida Black Stars vs Polisi Tanzania, Uwanja wa Airtel, saa 12:30 jioni

JKT Tanzania vs Namungo FC, Uwanja wa Mej. Gen. Isamuhyo, saa 3:00 usiku

Matokeo ya mzunguko wa 4 NBC Premier League

Mashujaa FC 2-1 Kagera Sugar, Uwanja wa Lake Tanganyika, Agosti 27,2026. Wafungaji wa mabao ni Mishano Daud dakika ya 64 na Haroun Lyawatana dakika ya 72 kwa Mashujaa FC. Mudathir Said dakika ya 38 ni mfungaji wa bao la Kagera Sugar. Man of The Match Mishamo Michael wa Mashujaa FC

Simba SC 1-0 Coastal Union, mchezo ulichezwa Uwanja wa Meja Jen. Isahmuyo, Agosti 27,2026. Bao la ushindi lilifungwa na Ismail Toure dakika ya 75. Man of The Match Nathaniel Chilambo.

Fountain Gate 0-2 Mbeya City, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Agosti 28,2026. Mfungaji wa mabao yote ni Osca Mwajanga dakika ya 83 na 85. Baada ya mchezo Man of The Match alitangazwa kuwa Mwajanga.

Geita Gold 2-2 Azam FC, Uwanja wa Bukombe, Agosti 28,2026. Mabao ya Geita Gold yalifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 45+4 penalti na Martin Kigi dakika ya 90+3. Magoli ya Azam FC, Sopu dakika ya 45+1 penalti na Himid Mao dakika ya 90+1. Man of The Match Kigi.

Yanga SC 2-0 Pamba Jiji FC, Uwanja wa KMC Complex, Agosti 28, 2026. Mabao yalifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 17 na Ibrahim Toure dakika ya 22. Man of The Match Maxi.

Hitimisho

TRA United SC vs Dodoma Jiji FC ni mchezo mkali kwa mzunguko wa 4. Vinara wa ligi ni Yanga SC wakiwa na pointi 12 baada ya mechi 4 wameshinda zote.Wakusanya mapato wana pointi 2 wakiwa nafasi 11 baada ya mechi 3wamepoteza 1 na kupata sare mchezo 1.

Share this: