Lionel AtebaLionel Ateba

WAKIMATAIFA Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kazi inaanza ambapo kete yao ya kwanza inatarajiwa kuwa ugenini Septemba 15 2024 kwenye kusaka ushindi ndani ya dakika 90 za ushindani.

Chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids Simba ina kibarua hicho huku ikianzia ugenini. Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ipo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa imetinga hatua ya pili huku Azam FC iliyokuwa katika Ligi ya Mabingwa na Coastal Union kwenye Kombe la Shirikisho hizi ziligotea hatua ya awali.

Joshua Mutale
Joshua Mutale nyota wakimataifa wa Simba. Source: Simba.

WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA

Katika Kombe la Shirikisho Afrika Simba wapinzani wake ni Al Ahli Tripoli ya Libya ambapo miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa na hatari katika timu hiyo ni Mabululu ambaye ni mshambuliaji mpya katika timu hiyo.

Simba inatarajiwa kucheza mchezo wake kimataifa ugenini Septemba 15 2024 itakuwa ugenini na itarejea Bongo katika mchezo wa ligi kusaka pointi tatu muhimu uwanjani.

KOCHA WA Simba
KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids mwenye tuzo ya kocha bora Agosti. Source: Simba.

Kuhusu mchezo wa kimataifa Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu wanafanya maadalizi mazuri kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo.

“Kwenye mchezo wetu wa kimataifa tunatambua kwamba utakuwa na ugumu lakini kikubwa ambacho tunakifanya ni kuwa bora katika kutafuta matokeo uwanjani. Kupata ushindi kwenye mechi zilizopita kumetupa nguvu ya kujiamini hivyo tunaamini kazi bado inaendelea.”

DABI INAKUJA

Kariakoo Dabi inatarajiwa kuwa Oktoba 19 2024 Uwanja wa Mkapa ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge. Ikumbukwe kwamba Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imefanya maboresho katika ratiba kwenye mechi 14 ambazo zitakuwa na tarehe mpya hapo awali hazikuwa na tarehe.

Hivyo Simba na Yanga watani hawa wa jadi watakutana Oktoba. Sababu kubwa ya maboresho hayo ni kuondolewa kwa klabu za Azam FC na Coastal Union katika anga la kimataifa kwenye hatua za awali.

MZIZIMA DABI

Katika maboresho ya ratiba, Mzizima Dabi ambayo itawakutanisha Azam FC v Simba inatarajiwa kuchezwa Septemba 26, Uwanja wa Mkapa.

TUZO KABATINI

JEAN
JEAN kiungo wa kimataifa wa Simba kwenye majukumu yake ndani ya uwanja mchezo dhidi ya Fountain Gate. ource: SImba.

Simba wameanza kwa ushindi kwenye kila kona wakiandika rekodi ya kutwaa tuzo mbili kwa mpigo kwa kocha na mchezaji ndani ya ligi ikiwa ni msimu mpya wa 2024/25.

Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi aliyechaguliwa ni Jean ambaye ni chaguo la kwanza la kocha Fadlu ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani akitajwa kuwa ni mashine ya kutengeneza mabao ndani ya Simba.

Kwenye mechi mbili Ahoua alifunga bao moja na pasi tatu za mabao huku Fadlu akiwa mpanga ramani wakishinda mechi zote kwenye msako wa pointi sita wakakomba zote mazima uwanjani baada ya dakika 90 kugota mwisho.

Ni Septemba 2 2024 walitangazwa kushinda tuzo hizo ikiwa ni mwanzo kabisa wa msimu wa 2024/25 ambao una ushindani mkubwa ndani ya uwanja kutokana na kila timu kusaka matokeo ya ushindi mapema.

Ni pointi sita Simba ilikomba baada ya kucheza jumla ya mechi mbili ambazo ni dakika 180. Kwenye mechi hizo mchezo wa kwanza iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 Tabora United na mchezo wa pili ilikuwa Simba 4-0 Fountain Gate zote zilichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.

Fadlu wa Simba alikuwa akipambana na Patrick Aussesms kocha wa Singida Black Stars na Abdallah Mohamed huyu anainoa Mashujaa inayotumia Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kwa mechi za nyumbani hawa waliingia fainali.

SEMAJI LAUNGURUMA

SEMAJI LA KIMATAIFA
SEMAJI la Simba Ahmed Ally. Source: Simba.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa ubora wa wachezaji wote wa Simba unampa nafasi kocha kupanga kikosi cha ushindi na wanaimani kwamba walistahili kutwaa tuzo hizo za Agosti.

“Ukiangalia namna ambavyo tumecheza mechi za Agosti hakika ilikuwa ni burudani na furaha kwa kila Mwanasimba kutazama wachezaji wakiwa uwanjani kutimiza majukumu yao na imekuwa hivyo.

“Kwenye upande wa rekodi katika mechi mbili tumefunga mabao mengi kuliko timu nyingine hii ni kubwa na hata ukichukua mchezo mmoja bado tumeshinda mabao mengi unaona mchezo dhidi ya Tabora United tumeshinda mabao 3-0 na hatujaruhusu kufungwa.

“Mchezo wa pili ushindi wetu ulikuwa wa mabao 4-0 hata huo hatujafungwa licha ya makosa ambayo yamekuwa yakifanyika kwenye mchezo uliopita taratibu kumeanza kuwa na maboresho hivyo tunaamini kwamba tunazidi kuimarika zaidi.”

Share this: