Nyie Hamuogopi VibeNyie Hamuogopi Vibe

KITAUMANA Uwanja wa Kaitaba kwa wababe wawili kuvuja jasho kwenye msako wa pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90 Kagera Sugar wakiwakaribisha Yanga huku wakimataifa Azam FC kweye dakika 90 za mwanzo msimu wa 2024/25 zikiwa ni moto ugenini.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kwa msimu wa 2024/25 ikiwa chini ya Kocha Mkuu,Miguel Gamondi. Unaweza kuweka mkeka wako SportPesa ukavuna mkwanja.

RATIBA YA AGOSTI 29 2024

Mechi tatu za Ligi Kuu Bara zinatarajiwa kuchezwa leo katika viwanja tofautitofauti itakuwa namna hii:-

KMC v Coastal Union, Uwanja wa KMC, Mwenge saa 10:00 jioni.

Kagera Sugar v Yanga, Uwanja wa Kaitaba, saa 11:00 jioni.

Namungo v Fountain Gate, Uwanja wa Majaliwa saa1:00 jioni.

KAITABA NA YANGA

 

Clatous
Wachezaji wa Yanga waishangilia moja ya bao kwenye mchezo wa ushindani. Source: Yanga.

Yanga ilipokutana na Kagera Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Februari 2 2024 msimu wa 2023/24 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-0 Yanga.

Ndani ya dakika 90 wababe hao wawili walivuja jasho huku makipa wakifanya kazi yao kuokoa hatari za washambuliaji wa timu zote mbili. Ni mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili ambazo zipo ndani ya ligi.

Kagera Sugar unakuwa ni mchezo wa pili kucheza ndani ya msimu wa 2024/25 walifungua pazia kwa kucheza na Singida Black Stars kwa kufungwa bao 1-0 dakika za lala salama hivyo leo wataingia kwa tahadhari wakiwa nyumbani.

YANGA KIMATAIFA WASHAMBULIAJI BALAA

Yanga sio kinyonge ni mechi mbili za kimataifa wamecheza dhidi ya Vital’O ya Burundi wakifunga jumla ya mabao 10 ndani ya dakika 180 hivyo inaonyesha kuwa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo sio ya mchezo.

Clatous Chama kahusika kwenye jumla ya mabao sita, kafunga mabao mawili na kutoa pasi mbili kiungo ambaye ameonesha ubora kwenye eneo la kutengeneza pasi za mwisho akifikisha jumla ya mabao 20 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

MASTA GAMONDI NENO

Gamondi
Gamond Miguel, Kocha Mkuu wa Yanga. Source: Yanga.

“Huu ni mwanzo wa msimu, nimeshawaeleza wachezaji wangu nini mashabiki wanahitaji. Kiufupi Wananchi wanahitaji alama tatu. Nafahamu mashabiki wetu wanatamani kweli tufunge magoli mengi, lakini kwetu sisi jambo la kwanza ni alama tatu.

“Tumefika salama na tumejiandaa vya kutosha, tunakwenda kuanza msimu mpya tukiwa na hamasa kubwa. Sitaki kuangalia sana mchezo uliopita ingawa tulipata somo. Tumeshajiandaa kisaikolojia kucheza dhidi yao kwa kuzingatia namna yao ya uchezaji na mazingira ya uwanja.”

KAGERA SUGAR HAWA HAPA

Paul Nkata, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani kwenye mechi watakazoshuka uwanjani kikubwa ni kupata matokao mazuri. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo waliopoteza dhidi ya Singida Black Stars, nyota wa mchezo alichaguliwa Ramadhan Chalamanda kipa wa Kagera Sugar.

KIBABAGE MSIKIE

Beki wa kupanda na kushuka ndani ya Yanga, Nickson Kibabage ameweka wazi kuwa walipata somo kwenye mchezo uliopita kwa kuwa hawakupata matokeo mazuri uwanjani.

“Mchezo uliopita katika uwanja huu hatukupata matokeo mazuri. Najua wachezaji wenzangu wanalitambua hilo. Bahati nzuri ni mchezo wa kwanza wa ligi tumeshajiandaa vyakutosha.”

AZAM FC WAKWAMA KWA WAJEDA

FEISAL
NYOTA wa Azam FC Feisal Salum akipambana na nyota wa JKT Tanzania kwenye moja ya mchezo wa ligi. Source: Azam.

Ligi inazidi kuchanja mbunga ambapo mchezo wa kwanza wa ufunguzi kwa matajiri wa Dar, Azam FC walikuwa ugenini mbele ya Wajeda, JKT Tanzania wakigotea kukomba pointi mojamoja kwa kushuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 0-0 Azam FC.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi ni matokeo ambayo walikuwa hawajatarajia ila ni mwanzo wa msimu ushindi unakuja kwenye mechi ambazo zinafuata ndani ya ligi kwa kuwa bado zipo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ibwe ameandika namna hii: “Angalia vizuri msimamo hapo ndio kwanza tumecheza game ya kwanza alama moja. Bahati mbaya tumetoa draw, (sare) ambayo hatukuitaka lakini tumeipokea japo kinyonge.

Ibwee
Ibwee Hasheem, Ofisa Habari wa Azam FC. Source: Azam.

“Tunaendelea kujiimarisha vizuri, bahati nzuri ni kwamba ligi haijafika mbali msituchukulie poa wengi walitaka tupoteze watuzomee kama wafanyavyo katika hii sare ya leo. Hatukati tamaa, hatuchoki we will fight to get back on our play style and more goals be scored.(Tutapambana kurejea kwenye mfumo wetu wa kucheza na mabao mengi yatafungwa).

“Poleni mashabiki wetu kwa sare ushindi wa mpira mwingi unakuja siku sio nyingi wala hamhitaji D 2 kuelewa aminini hili neno langu. Utamu waja.”

BOCCO NDANI YA UWANJA

Kwenye mchezo wa Agosti 28 nyota wa zamani wa Simba, John Bocco alipata nafasi ya kucheza licha ya kuanzia benchi ilikuwa dakika ya 88 kwenye mchezo huo aliingia akichukua nafasi ya Charles Ilanfya ambaye ni mshambuliaji.

Ikumbukwe kwamba Bocco alikuwa akicheza na waajiri wake wa zamani kwa kuwa kabla ya kuibukia Simba alitokea hapo kwa matajiri wa Dar ambao kwa sasa wanafundishwa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo.

Share this: