Ngushi MashujaaNgushi Mashujaa

WAZEE wa mapigo na mwendo Mashujaa watakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu wa 2024/25 katika msako wa pointi tatu ndani ya dakika 90.

Ipo wazi kuwa Mashujaa ya Kigoma itawakaribisha Prisons saa 10:00 jioni mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika kwa wababe hao kusaka ushindi muhimu. Mechi hii unaweza kuweka mkeka wako na SportPesa ukatazama mapigo ya ushindi ukakomba mkwanja wako.

WAZEE wa Mapigo na Mwendo
WAZEE wa mapigo na mwendo, Mashujaa FC. Source: Mashujaa.

Kwenye mchezo uliopita Mashujaa walikomba pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji, walikula zabibu za Dodoma wakiwa Kigoma kwenye mchezo wa kwanza wakiwapa furaha mashabiki wao.

Seif Karihe nyota wa Mashujaa ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wao wa ligi dhidi ya Prisons watapambana kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tupo tayari kwa ajili ya kupambana kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu na kikubwa ni kuona kwamba tunawapa furaha mashabiki wetu ambao wapo pamoja nasi kwenye kila hatua.”

Katika mchezo uliochezwa Agosti 17, Mashujaa walipata bao la ushindi dakika ya 33 kupitia kwa Chrispin Ngushi mshambuliaji ambaye aliwahi kuwa ndani ya kikosi cha Yanga inayodhaminiwa na SportPesa.

Agosti 24 haijapoa ipo kazini kwa kuwa ligi inaendelea kupamba moto kwa kila timu kupambania malengo ndani ya uwanja kwenye kusaka pointi tatu.

Pamba Jiji ya Mwanza ambayo imepanda ligi baada ya kupita zaidi ya miaka 15 itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji, kutoka makao makuu ya Tanzania.

PAMBA JIJI NA DODOMA JIJI, MAJIJI KAZINI

Pamba Jiji
Wazee wa mapigo na mwendo watawakabili Prisons waliotoshana nguvu na Pamba Jiji, 2024. Source: Pamba Jiji.

Hizi mechi ya Pamba na Dodoma Jiji itachezwa mapema kabisa jioni ya saa 10:00 kwa mashabiki kushuhudia burudani huku wababe hao wawili wakiwa kazini kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.

Katika mchezo wa ufunguzi wa ligi uliochezwa Agosti 16 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ulisoma Pamba 0-0 Tanzania Prisons. Hivyo kete ya pili kwa Pamba itakuwa dhidi ya Dodoma Jiji ambayo ilitoka kupoteza dhidi ya Mashujaa.

Kagera Sugar watakuwa Uwanja wa Kaitaba kukabiliana na Singida Black Stars mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku. Huu ni mchezo wa kwanza kwa Kagera Sugar huku Singida Black Stars wao kete yao ilikuwa Agosti 18 Uwanja wa Sokoine Mbeya ulisomaKen Gold 1-3 Singida Black Stars walikomba pointi tatu ugenini.

MNYAMA SIMBA KAZINI

Balua na Tabora United
EDWIN Balua akiwa kwenye mapigo na mwendo uwanjani Agosti 18 2024. Source: Simba.

Agosti 25 itakuwa imechangamka kweli kutokana na mechi kali kutarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge Dar hapa wababe wawili watavuja jasho kumsaka mshindi.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids itawakaribisha wapinzani wao Fountain Gate inayodhaminiwa na SportPesa hii itachezwa saa 10:00 jioni.

Mchezo wa Agosti 18 Simba 3-0 Tabora United ilkuwa ni ushindi kwa Simba iliyokomba pointi tatu kwenye mchezo wa ufunguzi ndani ya msimu mpya wa 2024/25.

NENO LA SEMAJI

Ahmed Semaji
Ahmed Semaji la Simba inayoshiriki Ligi Kuu Bara 2024/25. Source: Simba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa tayari maandalizi kwa mchezo wao dhidi ya Fountain Gate yanaendelea na kikubwa wanahitaji ushindi.

“Kuwa na mwendelezo kwenye mechi ambazo tunacheza hilo tunahitaji kwa kuwa timu imetoka kushinda mchezo wake wa ufunguzi ikiwa ni mwanzo mzuri licha ya kwamba hatujapata ushindi mkubwa na wachezaji bado hawajawa kwenye muunganiko mzuri.”

Namungo inayotumia Uwanja wa Majaliwa itawakaribisha Tabora United kwenye mchezo wa ligi ikiwa ni mzunguko wa kwanza ndani ya 2024/25 inayokwenda kwa kasi kwelikweli.

SINGIDA BLACK STARS WAKALI UGENINI

Singida Black Stars chini ya Patrick Aussems ambaye ni Kocha Mkuu wameonekana kuwa na makali kwenye mechi za ugenini hilo linatokana na usajili waliofanya pamoja na uzoefu wa wachezaji.

Aussems amesema kuwa kikubwa ambacho wanahitaji ni ushindi ndani ya uwanja kupata pointi tatu muhimu iwe ugenini ama nyumbani.

“Tunatambua ushindani ni mkubwa tupo tayari kwa ajili ya kuona kwamba tunapata matokeo mazuri hilo ni jambo la msingi, pongezi kwa wachezaji namna ambavyo wanajituma na hili linaongeza nguvu ya kupambana kwenye mechi zetu zote.”

MASHUJAA NYUMBANI MAPIGO NA MWENDO

Ushind kwenye mchezo wa kwanza nyumbani kwa Mashujaa unaonyesha kwamba ni timu ambayo inaendeleza mapigo na mwendo wake wa msimu wa 2023/24 kutokana na wapinzani wengi kukwama kukomba pointi tatu kwa wepesi.

Ikumbukwe kwamba mchezo wao wa ufunguzi walikutana na Dodoma Jiji wakamaliza kazi kipindi cha kwanza na watakuwa nyumbani kwa mara nyingine dhidi ya Prisons ambayo haijafunga bao kwenye mchezo wa ufunguzi walipotoshana nguvu na Pamba Jiji ya Mwanza.

Share this: