Ki na NzengeliKi na Nzengeli

RAIS wa Yanga, Injina Hersi Said amesema kuwa malengo makubwa kwa msimu wa 2024/25 ni kufanya vizuri kwenye mashindano yote wanayoshiriki huku katika Ligi ya Mabingwa Afrika ni kufika hatua ya robo fainali. Aliweka wazi kuwa ushindi wa 5G uliwapa tabu kutokana na wapinzani wao kukamia.

Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ina kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara ilitwaa msimu wa 2023/24 baada ya mechi 30 ilikomba jumla ya pointi 80 kibindoni inadhaminiwa na kampuni ya SportPesa.

Injnia
RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said. Source: Yanga.

Injinia kupitia mahojiano maalumu katika kituo cha Wasafi alibainisha kuwa wamekuwa wakifanya kazi kubwa kwa ushirikiano na wadhamini SportPesa ambao wamekuwa bega kwa bega na timu hiyo inayopeperusha bendera kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa upande wa usajili wa wachezaji wao wapya na wale waliopo kwenye kikosi hicho amebainisha kuwa haikuwa rahisi kuwapata wachezaji hao kutokana na timu nyingi kuhitaji saini za wachezaji hao kuwa kwenye timu zao.

KUHUSU WADHAMINI

KAMWE
ALI Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga akiwa na uzi wenye nembo ya SportPesa. Source: Yanga.

“Tumekuwa na mahusiano mazuri ya wadhamini wetu ambao kila tunapowakimbilia wanatushika mkono, nichukue fursa hii kuwashukuru sana Kampuni ya SportPesa, Azam TV, GSM Group kwa kuwa na sisi katika kipindi chote cha uongozi wangu

“Kama kuna jambo ambalo Wanayanga wanapaswa kuliombea dua liendelee ni uwepo wa GSM kwenye timu yetu, amekuwa akitusapoti katika mambo mengi mno.

“Mfano juzi kwenye Ngao ya Jamii kabla ya kuwashughulikia watu fulani, alikuja na kutuuliza bajeti ya Bonasi ikoje, tulipomwambia akasema haitoshi, akaongeza fungu la maana vijana wakaenda kupambana tukashinda.

MWENDO WA 5 G

Kariakoo Dabi
Pacome akiwa na Ngoma kwenye Kariakoo Dabi. Source: Yanga.

Msimu wa 2023/24 Yanga ilikuwa ikitembeza kichapo cha mabao 5 kwa wapinzani wao na miongoni mwa timu zilizofungwa ilikuwa ni Simba zama za Roberto Oliveira aliyekutana na Thank You.

“Zile goli 5 tulizoshinda msimu uliopita zilitupa wakati mgumu sana. Wapinzani walikuwa wanakuja kwenye mechi zetu wakikamia kwa ajili ya kuzuia wasifungwe goli 5 na hiyo ilifanya mechi zetu kuwa ngumu sana. Tulichofanya msimu huu ni kuongeza ubora kwenye kikosi chetu, hivyo mtu akizuia sana asifungwe goli 5 anapata kichapo cha goli 4.

“Kila unapoona Wanayanga wanakunywa supu, ujue ni maadhimisho ya zile goli 5. Nimemwambia Ally Kamwe zoezi hili liendelee kwa sababu linatukumbusha tukio lililotupa raha sana mashabiki wa Yanga.

ISHU YA CHAMA

Clatous Chama
Clatous Chama kiungo wa Yanga aliyeibuka hapo akitokea kikosi cha Simba. Source:Yanga.

“Chama ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa sana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ana ambao 19 mpaka sasa, kwa ubora wake kwa msimu huu hakuna timu aliyostahili kucheza Afrika zaidi ya Yanga.

“Nilizungumza nae na kumwambia anakuja kwenye timu ambayo imesheheni ubora kila eneo, itamsaidia kufikia mafanikio makubwa zaidi. Chama aliichagua Yanga kwa sababu ya ubora wa kikosi chetu.

SAINI YA KOCHA MASTA GAMONDI

“Kabla ya kusaini mkataba mpya, kocha wetu Miguel Gamondi alipata ofa nyingi sana kutoka Klabu nyingine kubwa Afrika na aliahidiwa hela nyingi lakini alichagua kubaki Yanga kwa sababu ya ubora wa timu tuliyoitengeneza. Hii timu yetu inaweza kumpa heshima kubwa zaidi Afrika.

MALENGO KIMATAIFA

“Malengo yetu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu ni tufike tena hatua ya Robo Fainali. Lakini kwenye maisha Mwenyezi Mungu hutoa zawadi, tukipata zawadi ya kufika fainali na kuchukua ubingwa basi tutashukuru. Target yetu ni Robo Fainali na tutapambana kufanikisha hilo.

“Kila mchezaji anayecheza Yanga anatakiwa na timu nyingine Afrika. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu tuna wachezaji bora sana katika kikosi chetu.

Walid Mzize ni tegemeo la taifa letu. Makocha wote wawili wa Yanga Nabi na Gamondi wamempa nafasi. Kwa sasa yuko kwenye mikono salama zaidi akiwa na jezi ya Yanga na ana mengi ya kujifunza na hapa ndio mahala sahihi kwake kwa maslahi ya timu yetu ya Taifa pia.

KIMATAIFA KUPIGWA CHAMAZI

“Kutokana na marekebisho yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mkapa, mechi yetu ya marudiano dhidi ya Vital’O, hatutacheza tena uwanja wa Mkapa, Tutacheza katika uwanja wa Azam Complex, Jumamosi majira ya saa 1:00 jioni.

“Mechi iliyopita wenzetu Vital O walisema watatunywa kama supu lakini tulifanikiwa kupata ushindi wa goli 4, Lakini kwenye mchezo huu wa marudiano ni zamu yetu sasa kuwanywa wao kama supu.

Share this: