Zimbwe JrZimbwe Jr

ORODHA ya wanaowania tuzo za TFF 2023/24 ipo hadharani ambapo kila mmoja ametambua nani yupo kwenye kipengele kipi kutokana na uteuzi ambayo umefanyika kulingana na vipengele husika. Ipo wazi kuwa kwenye vipengele vingi ndani ya Ligi Kuu Bara Yanga imekimbiza kila kona kwa kuwa na wachezaji wanaowania tuzo hizo.

Ni Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) imefanya uteuzi huo kwenye vipengele mbalimbali kuelekea kwenye tuzo hizo ambazo zilikuwa zinasubiriwa kwa shauku kubwa. Kwa sasa timu nyingi zipo kwenye maandalizi ya msimu mpya.

Usiku wa tuzo unatarajiwa kuwa ni Agosti Mosi, 2024 jijini Dar ikiwa ni mwezi ambao ligi inatarajiwa kurejea. Ikumbukwe kwamba msimu mpya wa 2024/25 unatarajiwa kuanza Agosti 16 2024.

Mabingwa kwa msimu wa 2023/24 ni Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya SportPesa. Kwa sasa Yanga imeweka kambi Afrika Kusini ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi ya msimu wa 2024/25.

Julai 24 Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya TX Galaxy na kupata ushindi wa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Prince Dube ambaye kafunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

ORODHA YA MAKUNDI YA TUZO

Fei Toto
Fei Toto kiungo wa Azam FC kwenye orodha ya wanaowania tuzo 2023/24 za TFF. sOURCE: Azam FC.

Tuzo zipo kwenye makundi tofauti ambayo yamewekwa kwa kufanyiwa  uteuzi namna hii:-

  1. Tuzo za Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB. Ikumbukwe kwamba bingwa wa kombe hili ni Yanga.
  2. Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake, bingwa ni Simba Queens.
  3. Tuzo za Ligi Kuu ya NBC, bingwa ni Yanga.
  4. Tuzo za utawala.
  5. Tuzo za ligi nyingine.

 

ORODHA YA TUZO MPYA

Kuna tuzo tatu mpya ambazo zimeongezeka hizo hazikuwepo msimu wa 2022/23 katika tuzo hizo mpya mbili hazijawahi kutolewa na moja iliwahi kutolewa lakini msimu uliopita haikutolewa.

 

Tuzo mpya ni ya mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje kwa upande wa Wanaume na nyingine ni mchezaji bora upande wa Wanawake anayecheza nje na tuzo ya mchezaji bora wa soka la ufukweni.

 

ORODHA YA TUZO KWA KOMBE LA CRDB

MFUNGAJI BORA

Clement Mzize wa Yanga

Edward Songo wa JKT Tanzania hawa wote walifunga mabao matano.

 

KIPA BORA

Djigui Diarra wa Yanga

Khomein Abubakar wa Ihefu

Mohamed Mustapha wa Azam FC.

 

Fei
KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum yupo kwenye orodha ya wanaonwania tuzo za TFF 2023/24. Source: Azam FC.

ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA

  1. Stephane Aziz Ki wa Yanga
    Feisal Salum wa Azam FC
    3. Kipre Jr wa Azam FC
    4. Djigui Diarra wa Yanga
    5. Ley Matampi wa Coastal Union
    6. Yao Kouassi wa Yanga
    7. Ibrahim Bacca wa Yanga
    8. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr wa Simba.ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA KIPA BORA NBC

    1. Ayoub Lakred wa Simba.
    2. Djigui Diarra wa Yanga
    3. Ley Matampi wa Coastal Union

 

ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA BEKI BORA

1. Yao Kouassi wa Yanga
2. Ibrahim Bacca wa Yanga
3. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr.’ wa Simba

Aziz KI
Aziz Ki kiungo wa Yanga yupo kwenye orodha ya wanaowania tuzo 2023/24. Source: Yanga.

ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA KIUNGO BORA
1. Stephane Aziz Ki wa Yanga
2. Feisal Salum wa Azam FC
3. Kipre Junior wa Azam FC

ORODHA YA WANAOWANIA TUZO YA KOCHA BORA

1. David Ouma wa Coastal Union
2. Bruno Ferry wa Azam FC
3. Miguel Gamondi wa Yanga

Kikosi bora kwa msimu wa 2023/24 kinatarajiwa kutangazwa ukumbini rasmi siku ya tukio huku tuzo ya mfungaji bora ikiwa mikononi mwa Aziz Ki.

Aziz Ki wa Yanga alifunga jumla ya mabao 21 akiwa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya ligi msimu uliopita na mshindani wake mkubwa alikuwa ni Feisal wa Azam.

Mzawa Feisal aligotea kwenye mabao 19 akiwa ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu wazawa huku kiujumla Aziz akikimbiza kwenye eneo hilo.

LIGI YA WANAWAKE

Mfungaji bora ni Aisha Mnuka wa Simba Queens.

KIPA BORA

Najath Abbas wa JKT Queens

Caroline Rufaa wa Simba Quens

Mariam Shaaban wa Bunda Queens.

MCHEZAJI BORA

Aisha Mnuka wa Simba Queens

Stumai Abdallah wa JKT Queens

Kaeda Wilson wa Yanga Princess

Violeth Nicholaus wa Simba Queens

Vivian Corazone wa Simba Queens

KOCHA BORA LIGI YA WANAWAKE

JUMA Mgunda
JUMA Mgunda, yupo kwenye orodha ya wanaowania tuzo 2023/24. Source: Simba.

Juma Mgunda wa Simba Queens

Ester Chabruma wa JKT Queens

Noah Kanyonga wa Ceasiaa Queens

Best Eleven, (11) itatangazwa ukumbini siku ya usiku wa tuzo, Masaki.

 

 

Share this: