
Baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Aughsburg katika mchezo wao wa kwanza wa maandalizi ya kabla ya msimu, kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga Jumatano hii wanashuka tena uwanjani.
Wananchi wanatarajia kuvaana na kikosi cha TS Galaxy katika mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Kanyamazane nchini Afrika Kusini.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa pili kwao ambapo kama ilivyoi mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa saa 9:00 Alasiri sawa na sasa 10:00 Jioni kwa saa za hapa Nyumbani Tanzania.
Yanga Jumamosi iliyopita dhidi ya Aughsburg inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ujerumani, ambao ulipigwa kwenye dimba la Mbombela nchini Afrika Kusini huku goli pekee la Yanga likifungwa na straika, Jean Baleke.
Wakiwa nchini Afrika Kusini, Yanga wanatarajiwa kucheza mechi tatu za kirafiki ambapo pia watashiriki mashindano ya Kombe la Toyota huku miongoni mwa timu watakazovaana nazo ni Kaizer Chiefs ya kocha Nasreddine Nabi.
PACOME ASHUSHA PRESHA YANGA

Wakati kikosi cha timu hiyo kikiondoka Dar es Salaam Alhamisi ya wiki iliyopita, miongoni mwa nyota ambao walizua hofu kubwa ni Zouzoua Pacome ambaye alionekana kukosekana kwenye msafara.
Lakini habari njema ni kuwa tayari staa huyo amemalizana na tatizo la pasi yake ya kusafiria na muda wowote ataonekana akiuwasha moto ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Kikosi cha Yanga ambacho kinadhaminiwa na Kampuni ya michezo ya Kubashiri ya SportPesa kimelazimika kukatisha kambi yake ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Pre-season’ ambayo ilikuwa ikiendelea Avic Town, Kigamboni Dar es Salaam.
Msafara wa wachezaji wa kikosi hicho ambao Alhamisi iliyopita ni kama ifuatavyo;
Makipa
Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Khomeiry
Walinzi
Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Yao Attohoula Kouasi, Nickson Kibabage, Chadrack Boka, Kibwana Shomari.
Viungo
Khalid Aucho, Salum Abubakar, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Maxi Nzengeli, Aziz Andembwile
Viungo washambuliaji
Stephane Aziz Ki, Farid Mussa, Denis Nkane, Clatous Chama, Duke Abuya
Washambuliaji
Clement Mzize, Kennedy Musonda, Prince Dube
Jean Baleke (Anasubiri kutambulishwa)
Mwaliko huu ni kutoka ndani ya kikosi cha timu ya Kaizer Chiefs ambao wamekuwa na mahusiano nao ya ukaribu katika masuala ya kiuongozi na uendeshaji wa klabu.
Msimu uliopita Kaizer Chiefs walialikwa na Yanga kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kuadhimisha kilele cha wiki ya Wananchi, mchezo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
YANGA WAITEKA SAUZ
Unaweza kusema Yanga sasa wameiteka Afrika Kusini kwani achana na shughuli za maandalizi ya kikosi chao ndani ya uwanja, lakini pia uongozi wa timu hiyo umeendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuitangaza zaidi klabu yao kupitia kuandikisha Wanachama wapya.
Ikumbukwe msimu uliopita walifanikiwa kuanzisha Tawi jipya linalofahamika kama ‘Tawi la Yanga Afrika Kusini’.
Hii ni wakati timu hiyo ilipoenda kuvaana na Mamelodi Sundowns Ijumaa ya Aprili 5, mwaka huu katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2023/24 ambapo Yanga waliingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya matokeo ya suluhu katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Tawi hili limeendelea kutoa sapoti kubwa kwa timu hiyo tangu watue Afrika Kusini.
KOCHA YANGA JEURI TUPU

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi amesema: “Ukubwa wa timu yetu ndio umeifanya leo hii tumepata mialiko mikubwa nje ya Tanzania ambapo tunacheza michezo ya kirafiki.
“Kwa jinsi ambavyo tulicheza na FC AUGSBURG nadhani tulionyesha kiwango bora na kuwakumbusha watu ni wapi ukuaji wa soka Afrika umefikia, nadhani watanzania wote wanapaswa kujivunia Yanga hii.”
“Michezo hii kwetu ni sehemu ya maandalizi ya Kampeni yetu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao ambapo malengo yetu makubwa ni kuhakikisha tunaandika rekodi ya kufika mbali katika mashindano hayo na ikiwezekana kushinda ubingwa.
“Kikosi chote kina ari kubwa ya kuandika historia katika ziara hii na najivunia maingizo ya wachezaji wetu wapya ambao ni sehemu ya maboresho ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa 2024/25.”
INJIA HERSI ASHUKURU
Kufuatia matukio hayo, Rais wa Yanga Injina Hersi Said alisema: “Niweke rekodi sawa, sisi tuna matawi lukuki nje ya mipaka ya Tanzania. Kwa Mfano kule Marekani tunalo tawi la uanachama. Tunasisitiza mashabiki wetu nje ya Tanzania kutumia fursa hii ya kufungua account ya Tanzanite ya CRDB ambapo imetufanya kuwa karibu sana na Wanachama wetu wa diaspora.
“Niwapongeze sana idara ya habari na Wanachama kwa kuweka mipango mikakati madhubuti ya kampeni yasafari yetu. Nichukue nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana mashabiki wa wetu hapa Afrika Kusini.”

