
SportPesa Yamtambulisha Rasmi “Jol Master” kama Balozi mpya kutangaza bidhaa zao.
Dar es Salaam, Juni 27, 2024 Kampuni ya burudani na michezo ya kubahatisha inayoongoza katika soko la ubashiri ya SportPesa rasmi wamemtambulisha balozi wao mpya ‘Jol Master’ ambae atakuwa anatangaza bidhaa za mbalimbali za kampuni hiyo.
Jol Master ambaye ameibuliwa na jukwaa la kuchekesha la cheka tu, analeta uzoefu na ujuzi wake mkubwa wa tasnia ya sanaa , ambao utasaidia katika kukuza kampuni na bidhaa za Sportpesa nchini Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari, Sabrina Msuya, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa amesema: “Tunafuraha kuwa na Jol Master kama balozi wetu mpya, Jol analeta uzoefu wa muda mrefu katika Tasnia ya sanaa na ameonyesha chachu ya kufanya kazi kwa bidii, katika kukuza tasnia ya sanaa Tanzania, Sisi tukaona ni vyema kufanya kazi nae ili kuendelea kukuza Tasnia ya Sanaa nchini .
Kama balozi, Jol Master atafanya kazi kwa ukaribu na timu ya masoko ya SportPesa ili kukuza bidhaa na huduma za kampuni yetu,kama vile SupaJackpot, Jackpot ya Katikati ya wiki, Casino na bidhaa zingine nyingi, kwa kutumia kipaji chake cha sanaa ya kuchekesha maarufu kama’komedi’.
ALICHOSEMA JOL MASTER

Akizungumzia kujiunga kwake na Kampuni hii, Jol Master amesema: “Nimefurahi kujiunga na timu ya SportPesa na kuchangia ukuaji wa bidhaa zake nchini Tanzania. “Ninatarajia kufanya kazi na timu ili kukuza michezo ya kubahatisha na ningependa sana kuwashukuru uongozi wa kampuni hii Tanzania kwa kuendelea kutoa mchango wao wa kukuza michezo na sanaa, na ninawahaidi kuwaletea mashabiki wa michezo nchini mambo mengi na mazuri kutoka SportPesa, na kwa kuanza leo nimewaletea bidhaa ya Aviator ambayo inakupa uhakika wa ushindi wa zaidi ya mara 20,000 ya dau lako, kwa kiasi cha TZS 20 tu unaweza ukawa mshindi wa Aviator. “
Ili Kucheza Aviator, Tembelea tovuti ya www.sportpesa.co.tz au piga *150*87#, pia unaweza ukapakua APP ya SportPesa kupitia simu zinazotumia mifumo ya Android na IOS.
Kwa uteuzi huu, SportPesa Tanzania Limited inaendelea kuimarisha nafasi yake kama kinara katika tasnia ya michezo ya kubahatisha mtandaoni nchini Tanzania.

