MAJIBU-Yanga bingwaYanga bingwa

 

Aziz KI
Aziz KI kiungo mshambuliaji wa Yanga, mfungaji bora msimu wa 2023/24 mabao 21. Source: Yanga.

MAJIBU yaliyokuwa yakisubiriwa msimu wa2023/24  yamepatikana hivyo kwa sasa ipo wazi kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa mbali na taji la Ligi Kuu Bara wanaye mfungaji bora ambaye ni Aziz KI akiwa kafunga jumla ya mabao 21 na mshindani wake mkubwa Feisal Salum wa Azam FC akiwa katupia jumla ya mabao 19.

Azam FC imemaliza ubishi wa nani atakuwa namba mbili kwenye msimamo ikiwaacha nafasi ya tatu Simba kwenye msimamo wa ligi wote wakiwa na pointi 69 baada ya mechi 30 tofauti kwenye mabao ya kufunga na kufungwa. Azam FC imefunga mabao 63 huku Simba ikifunga mabao 59 na kwenye upande wa kuruhusu mabao ni 21 Azam FC imefungwa na Simba mabao 25.

MATOKEO YA FUNGA MSIMU

Mgunda
JUMA Mgunda Kocha Mkuu wa Simba na Chasambi. Source: Simba

Uwanja wa Mkapa ilikuwa Simba 2-0 JKT Tanzania mabao ya Simba yalifungwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 88 kwa mkwaju wa penalti, Willy Onana dakika ya 90’+2. Simba ilikomba pointi tatu ikiwa nyumbani inagotea nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 69 baada ya kucheza mechi 30 msimu wa 2023/24. Hivyo itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

GEITA GOLD NA MTIBWA SUGAR ZIMESHUKA 

Geita Gold ikiwa Uwanja wa Nyankumbu ilishuhudia ubao ukisoma Geita Gold 0-2 Azam mabao yakifungwa na Yeison dakika ya 58 na kiungo mshambuliaji Feisal Salum, dakika ya 71 kwenye mchezo huo.

Azam Vibe
NYOTA wa Azam FC wakiwa kwenye furaha baada ya kufunga moja ya bao mchezo wa ushindani. Source: Azam FC

Azam FC inamaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo ikiishinda ilive vita ya msako wa mshindi wa pili. Pointi 69 kibindoni ikiwa na uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika huku Geita Gold ikishuka daraja na pointi zake ni 25 inaungana na Mtibwa Sugar.

MAJIBU YA AZIZ KI 

Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Yanga 4-1 Tanzania Prisons ambapo kiungo Aziz Ki alifunga mabao matatu kwenye mchezo huo na kusepa na mpira wake alifanya hivyo dakika ya 11, 12 na 79  huku bao moja likifungwa na Kenned Musonda dakika ya 52 bao pekee la ufunguzi kwa Prisons lilifungwa na  Ngassa dakika ya 5.

Baada ya ushindi huo Aziz KI ambaye ni mfungaji bora amesema: “Ninamshukuru Mungu kwa haya yote ilikuwa ni msimu wenye ushindani mkubwa na kila mmoja ameona. Mashabiki, benchi la ufundi na wachezaji wenzangu ni muhimu kuwashukuru.”

NAMUNGO 10 BORA

Ubao wa Uwanja wa Majaliwa ilikuwa Namungo 3-2 Tabora United  mabao ya Namungo yakifungwa na Pius Buswita dakika ya 19 na 28 kwa mkwaju wa penalti, Manyanya alipachika bao moja dakika ya 77. Yale ya Tabora United yalifungwa na  Abbas pamoja na Moses.

Matokeo hayo yanaifanya Namungo kugotea nafasi ya 6 ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 30 huku Tabora United ikigotea nafasi ya 14 na pointi 27. Tabora United ina kazi ya kucheza play off ili kutafuta nafasi ya kubaki ndani ya ligi msimu wa 2024/25.

COASTAL UNION WAKIMATAIFA

Ubao wa Uwanja Coastal Union 0-0 KMC, wababe hao waligawana pointi mojamoja ndani ya dakika 90 za jasho la msako wa pointi tatu. Coastal Union nafasi ya nne ikiwa na pointi 43, KMC nafasi ya 5 pointi 37.

Ni Coastal Union itakwea pipa kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku KMC ikiwa ndani ya tano bora msimu wa 2023/24 uhakika kushiriki ligi msimu ujao.

MASHUJAA NI MASHUJAA KWELI

Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma ilikuwa Mashujaa 3-0 Dodoma Jiji mabao ya Relliats Lusajo dakika ya 6 na 47 moja lilijazwa kimiani na mwamba Ulomi  dakika ya 84.

Nafasi ya 8 Mashujaa wanamaliza msimu wa 2023/24 pointi kibindoni ni 35 huku Dodoma Jiji ikiwa nafasi ya 12 pointi 33 ina uhakika wa kujipanga na kushiriki kwa mara nyingine ndani ya ligi.

IHEFU WAITULIZA MTIBWA SUGAR

Uwanja wa Liti mchezo pekee uliokusanya mabao mengi kwenye funga kazi ambayo ni sita ndani ya dakika 90 na hat trick ilipatikana pia kwenye mchezo huo wa mwisho. Ihefu SC 5-1 Mtibwa Sugar ni Bola alipachika bao dakika ya 5, Chukwu dakika ya 16 na mwamba Ismail Mgunda alifunga tatu dakika ya 41, 62na 74.

Bao pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa na Seif Karihe ilikuwa dakika ya 37. Mtibwa Sugar imeshuka daraja itashiriki Championship msimu wa 2024/25 kusaka nafasi ya kurejea kwa mara nyingine ndani ya Ligi Kuu Bara.

SINGIDA FG YAPOTEZA NYUMBANI

Singida Fountain Gate 2-3 Kagera Sugar mabao ya Kidemile dakika ya 19, Deus Kaseke dakika ya 84 kwa mkwaju wa penalti  na Kagera Sugar walifunga kupitia kwa Deogratius Mafie dakika ya 40, Mbaraka Yusuph dakika ya 46 na Mhilu dakika ya 82.

Singida Fountain Gate inamaliza msimu ikiwa nafasi ya 11 pointi 33 kibindoni huku Kagera Sugar ikimaliza msimu ikiwa nafasi ya 10, pointi 34 zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 30.

WALINDA MILANGO

Diarra
Diarra Djigui kipa namba moja wa Yanga. Source: Yanga

Walinda milango wawili walikuwa kwenye vita yao ya kusaka nyota ambaye atamaliza msimu akiwa hajafungwa kwenye mechi nyingi na mwisho imefahamika nani ni nani baada ya msimu kukamilika.

Ley Matampi kipa wa Coastal Union baada ya kucheza jumla ya mechi 24 kakusanya clean sheet 15 huku Dijigui Diarra wa Yanga baada ya kukaa langoni kwenye mechi 21 hajafungwa kwenye mechi 14.

Share this: