
NJAA kali inawatesa Yanga ndani ya msimu wa 2023/24 kwa mujibu wa Kocha Mkuu Miguel Gamondi kwenye msako wa ushindi ni kufikia malengo yao ya kupata matoke mazuri sio kwa wachezaji pekee mpaka benchi la ufundi.
Gamondi masta wa mipango ndani ya kikosi cha Yanga kinachodhaminiwa na SportPesa amebainisha kuwa njaa kubwa iliyopo ni kupata mafanikio kwenye mechi ambazo wanacheza kila wakati ndani ya uwanja.
“Tuna njaa yakupata mafanikio kwenye mechi ambazo tunacheza hilo lipo wazi. Wachezaji wanatambua kwamba ushindani ni mkubwa nasi tupo tayari kuona kwamba matokeo yanakuwa mazuri kwenye mechi ambazo tunacheza.
“Mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye mechi zetu hili ni kubwa hivyo waendelee kujitokeza kwa wingi tunajua kwamba wanapenda matokeo mazuri hapo ndipo njaa yao ilipo nasi tunapambana kufanya vizuri,”.
NAHODHA NENO LAKE HILI HAPA

Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto ambaye alikuwa sehemu ya kikosi kilichopata ushindi dhidi ya Mashujaa kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wakiwa ugenini amebainisha kuwa kikubwa wanachohitaji kwenye mechi zao ni pointi tatu.
Yanga baada ya kucheza mechi 25 ndani ya ligi ina mechi tano mkononi kukamilisha mzunguko wa pili na kufunga mazima msimu wa 2023/24 ambapo inapambania taji la ligi ililotwaa msimu wa 2023/24.
Kwenye mechi ambazo walicheza Yanga walipata ushindi kwenye Kariakoo Dabi ilikuwa dhidi ya Simba na walishinda nje ndani ule wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga na mzunguko wa pili ilikuwa Yanga 2-1 Simba.
Mwamnyeto amesema kuwa kikubwa ambacho wanakihitaji kwenye mechi ambazo wanacheza ni pointi tatu muhimu kwa kuwa ili kufikia malengo yao ni muhimu kushinda mechi zao zote ambazo wanacheza.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Mashujaa, nahodha huyo alipata nafasi ya kucheza ilikuwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Mei 5 2024 baada ya dakika 90 Yanga walikomba pointi tatu mazima.
Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa 0-1 Yanga na bao la ushindi likifungwa na Joseph Guede ilikuwa dakika ya 41 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
“Tunafurahi kuona kwamba tunapata ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza ushindani upo hilo tunatambua mbinu ambazo tunapewa na benchi la ufundi tunazitumia na kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi.
“Kikubwa ni alama tatu kwenye mechi ambazo tunacheza tunatambua ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi nasi tunapambana kupata matokeo mazuri. Benchi la ufundi linatupa mbinu na wachezaji tunafanya kazi kwa kushirikiana kwenye mechi zote ambazo tunacheza.”
YANGA MOTO

Yanga ni moto kwenye ligi kutokana na kasi yake inayoendelea nayo kwa kupata matokeo kwenye mechi zake za ligi iwe nyumbani ama ugenini.
Timu pekee ambayo haijapoteza mechi ikiwa nyumbani ni Yanga kwa msimu wa 2023/24 ambapo baada ya kucheza mechi 25 ni mechi mbili iliambulia kichapo dhidi ya Ihefu na Azam FC zote ilikuwa ugenini kwa kufungwa mabao 2-1.
Yanga kwenye msimamo ni namba moja ikiwa na pointi 65. Mbele ya Mashujaa nje ndani iliambulia ushindi kwa kukomba pointi zote sita na kufunga mabao mawili ndani ya dakika 180.
Kwa upande wa utupiaji timu hiyo washambuliaji wake wamefunga jumla ya mabao 56 ikiwa ni namba moja kwa timu namba moja katika ufungaji wa mabao msimu huuu kwenye ligi.
Kinara wa utupiaji ndani ya ligi ni Aziz KI ambaye kafunga jumla ya mabao 15 akifunga mabao 13 kwa mguu wa kulia na mabao mawili kwa mguu wa kushoto hivyo mguu wake wenye nguvu ni ule wa kushoto akiwa uwanjani.
UKUTA BALAA ZITO
Ukiweka kando uimara wa ushambuliaji wakiwa na viungo washambuliaji wenye njaa ya kufunga mabao wakiongozwa na Aziz KI upande wa ukuta ni balaa zito.
Yanga inayodhamiwania na SportPesa ni namba moja kwa timu iliyoruhusu mabao machache ndani ya uwanja ambayo ni 12 kwenye mechi za ligi msimu huu kipa namba moja akiwa ni Djigui Diarra.
Diarra amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na mabeki wakiongozwa na Dickson Job mtu wa kazi ngumu ndani ya uwanja. Ipo wazi kwamba Job kafunga bao moja ndani ya ligi.
Chaguo la kwanza kwa Migue Gamondi ni yeye alifungua ukurasa wa kufunga Yanga alipofunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
MNYAMA KAONEWA
Watani wa jadi wa Yanga, Mnyama Simba ameonewa na Yanga kwenye mechi zote mbili msmu wa 2023/24 kwa kufungwa nje ndani walipokutana na katika msako wa pointi sita zote zimekwenda Yanga. Katika pointi 65 zilizopo Yanga sita walikomba mbele ya Simba.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba 1-5 Yanga na mchezo wa ligi mzunguko wa pili ilikuwa ni Yanga 2-1 Simba. Ni mabao 7 Yanga wamefunga mbele ya Simba iliyofunga mabao mawili ndani ya dakika 180.

