SIMBAMed na Benchikha

 

Mguda
JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba. Source: Simba

SIMBA wanafanyia kazi makosa yao yaliyopita ili kuwa imara kwenye mechi za ushindani ndani ya dakika 90 za kazi uwanjani katika kuvuja jasho. Ipo wazi kwamba timu hiyo ndani ya tatu bora haijawa kwenye mwendo mzuri.

Watani zao wa jadi Yanga ambao wanadhaminiwa na SportPesa walikomba pointi sita mazima mbele ya Simba msimu wa 2023/24. Kwa sasa ipo chini ya Juma Mgunda ambaye ameweka wazi kuwa wanafanyia kazi makosa yaliyopita.

“Makosa ambayo yamepita katika mechi zetu tunayafanyia kazi ili kuwa bora kwa mechi zinazofuata. Kikubwa ni kuona kwamba ushindi unapatikana wachezaji wapo tayari na wanapambana kuona tunashinda.”

WANAPAMBANIA KUREJEA KWENYE UBORA

INONGA
Beki wa Simba, Henock Inonga kwenye moja ya mazoezi. Source: Simba.

Ndani ya kikosi cha Simba kuna wachezaji wapo ambao hawajawa fiti kutokana na kusumbuliwa na maumivu ambayo walipata kwenye mechi za ushindani na wengine ilikuwa kwenye mazoezi.

Ipo wazi kwamba kwa sasa kikosi cha Simba kipo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda akishirikiana na Seleman Matola wote ni wazawa ndani ya kikosi cha Simba kinachopambania malengo yake.

Katika mchezo wa kwanza wa Mgunda kukaa kwenye benchi kukinoa kikosi hicho alishuhudia ubao wa Uwanja wa Majaliwa ukisoma Namungo 2-2 Simba.

Ni pointi mojamoja waligawana kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa. Mwamba Kibu Dennis alikwama kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo huo kutokana na kupata maumivu kwenye mchezo huo.

Kibu kwa sasa anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na timu ya Simba kuhusu maboresho ya mkataba wake pamoja na kuwa kwenye uangalizi mkubwa ili kurejea katika ubora wake.

Nyota huyo mwenye rasta kichwani ni bao moja amefunga ndani ya ligi alifunga kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa kwanza ilikuwa dakika ya 9 akitumia pasi ya Saido Ntibanzokiza.

Shomari Kapombe hajawa uwanjani kwa muda mrefu akipambania kurejea kwenye majukumu yake. Ni beki wa kupanda na kushuka bado hajawa fiti kwa sasa.

Clatous Chama. Kiungo huyu alipata maumivu kwenye Kombe la Muungano 2024 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya KVZ ambapo alikosekana kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC.

Chama baada ya kukosekana kwenye mchezo wa fainali alibainisha kwamba alipata maumivu makubwa kukosekana kwenye fainali lakini wachezaji wenzake walifanya kazi kubwa kutafuta ushindi.

“Habari mabingwa wa Muungano 2024, niliumia kukosekana kwenye mchezo wa fainali kutokana na kuumia lakini wachezaji walifanya kazi kubwa na tumepata ushidi.”

Ukiweka kando kutokuwa fiti Chama atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Tabora United kwa kuwa amefungiwa mechi tatu kwa kosa la kumchezea faulo nyota wa Yanga, Nickson Kibabage.

Katika fainali Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilifungwa na kiungo mkabaji Babacar Sarr ilikuwa dakika ya 77 kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Henock Inonga. Beki wa kupanda na kushuka ndani ya kikosi cha Simba alipata maumivu kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 20 2024.

Kwenye mchezo huo Inonga alikwamakukamilisha dakika 90 na alikuwa shuhuda wakipoteza pointi tatu mazima kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 2-1 Simba.

Ameanza mazoezi na timu kwa ajili ya kuendelea kupambania malengo ya timu hiyo kwenye mechi za ushindani msimu wa 2023/24.

Aishi Manula. Kipa namba moja wa Simba hajawa fiti kwa muda mrefu hivyo amekuwa shuhuda wa wachezaji wenzake wakipambania kombe ndani ya uwanja. Hakuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki Muungano 2024 na katika mechi za ligi dhidi ya Yanga Kariakoo Dabi mzunguko wa pili hakuweza kucheza.

Ni shuhuda wa mwamba Ayoub Lakred akiwa ndani ya uwanja alipotunguliwa mabao mawili kwenye mchezo huo. Joseph Guede na Aziz KI hawa walifunga mabao ya Yanga na Michael Fred alifunga bao kwa upande wa Simba.

MIAMBA IMEREJEA UWANJANI

MNYAMA
NYOTA wa Simba Saido na Luis kwenye moja ya mazoezi. Source: Simba.

Saido Ntibanzokiza hakuwa fiti na alikosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo lakini kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar alirejea uwanjani kutimiza majukumu yake.

Nyota huyo alitoa pasi ya bao kwa Fred walipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakikomba pointi tatu Uwanja wa Azam Complex.

Sadio Kanoute. Kiungo huyu mgumu naye alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Namungo tayari karejea kwenye ubora wake taratibu baada ya kuwa nje kwa muda akipambania hali yake.

Mzamiru Yassin. Nyota huyu alikosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano hilo limekwisha karejea uwanjani alianza kazi kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Share this: