BENCHIKHAsimbasctanzania------------------------------------------
BENCHIKHA
Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchika

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha hatimaye amefunguka mazito kuhusu kikosi chake kuonekana kupoteza muelekeo ambapo ameweka wazi kuwa changamoto kubwa ya kikosi chake ni kwa sasa ni wachezaji wake kushindwa kumalizia nafasi wanazotengeneza.

 

Kocha huyo ameweka wazi kuwa ukiangalia kwa umakini utagundua kila mchezo ambao timu hiyo wamekuwa wakicheza wamekuwa wakifanya umiliki mzuri wa sehemu kubwa ya mechi lakini wanashindwa kuzitumia nafasi wanazozipata.

 

Benchikha ameongeza kuwa pamoja na kushindwa kupata ushindi katika mechi zilizopita, lakini hawajakata tamaa kupambania ubingwa kwakuwa tumebakiwa na michezo 10.

 

“Kila mtu anajua, tunacheza vizuri tunatengeneza nafasi nyingi, lakini tunashindwa kuzitumia na hilo ndilo tatizo kubwa.”

 

“Bado hatujakata tamaa kuendelea kupambania ubingwa kwakuwa, tukishinda mechi zote 10 zilizobaki tunakusanya alama 30 kwa hiyo bado tuna nafasi ya kuchukua ubingwa,” amesema Benchikha.

BENCHIKHA NDANI YA DAKIKA 360 NGUMU SIMBA

https://sportpesa.co.tz/BENCHIKHA
Kocha wa Simba, Abdelihak Benchikha

Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu FC uliopigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya kufungana bao 1-1 ulikuwa ni mchezo wa nne mfululizo kwa Benchikha akiiongoza Simba katika mashindano yote bila kupata matokeo ya ushindi.

Katika mchezo huo Simba ilianza kwa kasi, huku viungo wa timu hiyo wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini itabidi wajilaumu wenyewe kwani walishindwa kuzitumia.

Timu wenyeji Ihefu walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Duke Abuya dakika ya 41, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Elvis Rupia.

Baada ya bao hilo Simba waliongeza kasi ya kutaka kusawazisha, lakini Ihefu walikuwa imara kwenye ulinzi na kusababisha kwenda mapumziko wakiwa mbele.

 

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama aliipatia Simba bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 71 baada ya Kibu Denis kuchezewa madhambi ndani ya 18.

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha alifanya mabadiliko ya kuwatoa Said Ntibazonkiza, Fred Michael na Clatous Chama na kuwaingiza Pa Omar Jobe, Luis Miqussone na Willy Onana.

Pamoja na mchezo huo ambao Simba waliowahi kupewa shavu la SportPesa hawakupata matokeo ya ushindi michezo mitatu mingine ni ile dhidi ya Al Ahly kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kuondoshwa kwenye mashindano ya Kombe la CRDB Federation Cup 2024 mbele ya mashujaa kwa changamoto ya mikwaju ya Penalti baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 kwenye dakika 90 za mchezo.

 

AHMED AITAJA YANGA

https://sportpesa.co.tz
Meneja wa Simba, Ahmed Ally

Baada ya kikosi cha Simba kushuka katika Uwanja wa Liti mkoani Singida kuikabili Ihefu FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, sasa kibarua kizito kwao ni cha mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ‘Dabi ya Kariakoo ambao unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo uongozi wa Simba waliowahi kunufaika na udhamini wa SportPesa kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema wanaingia kwenye mchezo wa huo wakiwa wanafahamu wanaenda kukutana na timu bora yenye wachezaji wazuri na wenye uzoefu.

Licha ya ugumu wa mchezo huo, lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata pointi tatu kwa kuwa kwao kila mechi ni fainali.

Ahmed amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo kwa ajili ya kuisapoti timu nao wanaahidi kuwalipa furaha.

Ahmed amesema anajua mashabiki hawana furaha hasa baada ya timu kupitia kipindi kigumu.

“Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi, tunajua wameumizwa na matokeo yetu ya mechi zetu zilizopita lakini tumejipanga, tunawaahidi tutawapa furaha,” amesema Ahmed

WACHEZAJI WATOA AHADI

Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari kupambana na kila mmoja yupo kamili.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo ujao, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tutajiandaa vya kutosha,” amesema Zimbwe Jr.

MAJERUHI FITI

Mlinzi wa Henock Inonga ambaye alikosa mchezo na Mashujaa na kurejea kwenye mchezo dhidi ya Singida  ambao wanadhaminiwa na Sportpesa ameendelea kusalia kuwa fiti akiendelea na  mazoezi ya mwisho chini ya kocha Benchikha.

Inonga alipata maumivu katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

 

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.