VITAAziz KI na Guede
  • SportPesa Dabi Yanga baba lao nje ndani yapeta mbele ya Singida Fountain Gate
  • Yawaacha mbali watani zao wa jadi Simba ndani ya Ligi Kuu Bara kwa pointi 9
  • Kariakoo Dabi mlangoni itafahamika Uwanja wa Mkapa

 

Aziz KI na Guede
Aziz KI na Guede wachezaji wa Yanga wakishangilia moja ya bao mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate. Source: Yanga

SPORTPESA Dabi mbabe wake kwa 2023/24 ni mabingwa  watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi  kwa mara nyingine tena mbele ya Singida Fountain Gate katika mchezo huo kwa timu zote mbili ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya SportPesa 2023/24  ambapo ni Yanga tena walikomba pointi zote tatu mazim.

Ipo wazi kuwa baada ya dakika 90 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Singida Fountain Gate 0-3 Yanga wakiibuka wababe ugenini kwenye mchezo wa ligi wakiwaacha mbali watani zao wa jadi Simba kwenye upande wa pointi na nafasi.

Ndani ya dakika 180 Singida Fountain Gate msimu wa 2023/24 katika SportPesa Dabi wamekwama kuifunga Yanga huku katika msako wa pointi sita ndani ya uwanja wakipoteza zote mazima.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kirumba, Mwanza Singida Fountain Gate inayofundishwa na Kocha Mkuu, Jamhuri Kihwelo, (Julio) ilionyesha ushindani wake ndani ya dakika 40 za mwanzo kwa kuwa imara katika kulinda lakini ngoma ilikuwa ngumu kugota dakika ya 45 kwa kuwa waliruhusu bao.

HAWA HAPA WAFUNGAJI SPORTPESA DABI

Katika mchezo huo Singida Fountain Gate walianza kwa mbinu ya kujilinda zaidi huku wakishambulia kwa kushtukiza na Yanga wao walikuwa wanashambulia mwanzo mwisho walipoanza na washambuliaji wawili ambao ni Clement Mzize na Joseph Guede wote walianza kikosi cha kwanza.

 

Ni Guede alianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 41 akiwa ndani ya 18 kwa mguu wake wa kulia hilo lilidumu mpaka muda wa mapumziko Yanga walikwenda wakiwa vifua mbele kwenye mchezo huo.

Huo ulikuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa SportPesa Dabi kuchezwa katika Ligi Kuu Bara hivyo kila timu hesabu zake ilikuwa ni kukomba pointi tatu mazima na kuwa wababe kwenye dabi.

 

Kipindi cha pili Aziz Ki alipachika bao la pili dakika ya 66 dakika mbili nyingine mwamba Guede alipachika bao lake la pili kwenye mchezo ilikuwa ni dakika ya 68 na kufanya ubao usome Singida Fountain Gate 0-3 Yanga na hayo yote yalidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Pasi zote za mabao ya pili kwa Yanga zilitoka kwenye miguu ya mshambuliaji mzawa chaguo la kwanza la Gamondi, Mzize ambaye alikuwa anawachagulia washkaji zake namna ya kuwapa pasi huku lile bao la Aziz KI likifungwa kwa shuti kali akiwa nje ya 18.

 AZIZ KI NAMBA MOJA

Aziz KI v Singida
Aziz KI kiungo mshambuliaji wa Yanga akiwa kwenye majukumu yake dhidi ya Singida Fountain Gate. Source:Yanga

Aziz KI anafakisha mabao 14 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni namba moja kwa watupiaji wa mabao msimu wa 2023/24 baada ya timu hiyo kucheza jumla ya mechi 21 na safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga mabao 52.

Kiungo huyo mshambuliaji amekuwa kwenye ubora wake ambapo mguu wake wenye nguvu ni ule wa kushoto kwenye kufunga mabao akiwa kafunga jumla ya mabao 12 kwa mguu wa kushoto na katumia mguu wa kulia kufunga mabao mawili.

Anayemfuatia kwa mabao mengi kwa sasa ndani ya ligi ni kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ambaye bao lake la 13 alifunga kwenye Mzizima Dabi walipokutana na Yanga Uwanja wa Mkapa.

SINGIDA SIO KINYONGE

Katika mchezo wa SportPesa Dabi Singida Fountain Gate hawakuwa wanyonge walifanya majaribio yao kupitia kwa Habib Kyombo, Deus Kaseke ambaye alifanya moja ya jaribio dakika ya 80 likaokolewa na kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 55 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi msimu wa 2023/24 na kasi hiyo imezidi kuwafanya kuwa kwenye mwendo bora ndani ya ligi.

Singida Fountain Gate wanabakiwa na pointi zao 24 naafasi ya 9 wakiwa wamecheza jumla ya mechi 22 ambapo kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana na Yanga walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 2-0 Singida Fountain Gate.

Mchezo huo ulichezwa Oktoba 27 2023 hivyo jumla wamefungwa mabao matano na Yanga ndani ya ligi msimu wa 2023/24.

WATANI WA JADI WAMEACHWA MBALI

 Yanga sasa imewaacha watani zao wa jadi Simba kwa tofauti ya pointi 9 kwa kuwa Simba wana pointi 46 na Yanga wao ni pointi 55 kibindoni wanatarajiwa kukutana Aprili 20 2024,  Uwanja wa Mkapa kwenye Kariakoo Dabi.

Simba wao mchezo wao uliopita waligawaa pointi mojamoja waliposhudia ubao wa Uwanja wa Liti ukisoma Ihefu 1-1 Simba.

Share this: