SportPesa watangaza mshindi wa Supa Jackpot ya zaidi ya Bilioni.
- Baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13/13 za Supa Jackpot na kuondoka na 265,780,681 TZS.
- Washindi wa bonasi zaidi ya 8700, Jumla ya Bil 1.028 zatolewa.
Dar es Salaam. 15 Februari, 2024. KAMPUNI ya kubashiri Michezo na Burudani SportPesa imemtangaza mshindi wa Jackpot ya shilingi 265,780,681 TSH David Mwenge Nyantora (27). David ambaye ni mfanyabiashara, alibashiri kwa usahihi mechi 13 kati ya 13 kwenye mechi za Supa Jackpot ambayo ina mgawanyiko wa Jackpot za mechi 17,16,15,14 na 13 iliyopata mshindi.
Akimtangaza mshindi huyo wa awamu ya kumi Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas alianza kwa kumpongeza David kwa ushindi wake na kuwa milionea mpya mjini.
“Kwa niaba ya kampuni ni furaha yangu kubwa sana kumtangaza kwenu, David Mwenge Nyantora kuwa ni mshindi rasmi wa Supa Jackpot yetu ya mechi 13 akiwa amejishindia shilingi 265,780,681. Ikiwa ni takribani miezi 11 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Supa Jackpot mechi hizihizi 13 ambapo hii ni awamu ya pili kupata mshindi wa Supa Jackpot tangu ianzishwe rasmi.
“Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashiri kupata zaidi ya washindi wa Jackpot 10 na kuwatangaza kwa miaka 6 mfululizo. Supa Jackpot ya wiki hii imeweza kutoa washindi wa bonasi jumla ya 8708 huku jumla ya bonasi zilizotolewa ikiwa ni zaidi ya milioni 756.
KUHUSU MSHINDI WA SUPA JACKPOT
Akizungumza katika hafla hiyo maalum iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, Dar-Es-Salaam, David anasema alianza kucheza na SportPesa mwaka 2018, baada ya kuifahamu kupitia usomaji wa magazeti.
“Mimi nilianza kucheza SportPesa mwaka 2018, baada ya kuifahamu kupitia usomaji wa magazeti, hii ni kutokana na urahisi ambao SportPesa imeuweka kwa kuorodhesha zile timu ambazo unaweza kuzichagua, hivyo nami nikaamua niingie na kuanza kubeti.
“Nimekuwa nikishiriki mara kwa mara na kushinda viwango tofauti vya fedha, lakini hii ni mara ya kwanza nimeshinda kiasi kikubwa kama hiki kupitia Supa Jackpot ya timu 13 ambayo inachukua timu 17. Mimi huwa natengeneza mkeka wangu kwa kutumia siku tatu kuchagua timu, na mara nyingi huwa nacheza mikeka miwili hadi mitatu, japo kwa hii Jackpot niliweka mkeka mmoja.

“Sikutarajia kushinda kiasi hiki kikubwa cha pesa hivyo, kwa sasa siwezi kusema nitaifanyia nini, nahitaji kwanza kutuliza akili na kufanya maamuzi kama niwekeze kwenye biashara au kununua nyumba kwa ajili ya familia kwa kuwa naishi na mtoto wangu mmoja na baadhi ya ndugu.” Amesema David.
Akiongelea mkeka wake wa Supa Jackpot, David amesema: “Nimekuwa na kawaida ya kufuatilia mechi za Supa Jackpot na wakati nashinda nilikuwa nikifuatilia mchezo wa Atalanta, kwa kweli hatukuamini na ilibidi turudie mara mbilimbili, lakini tulipopata SMS tukajua ni kweli na hapo shangwe lilikuwa kubwa kiasi kwamba tulishindwa kulala usiku,” amesema David.
TOFAUTI YA SPORTPESA NA WENGINE KWENYE SUPA JACKPOT
David anaendelea kuelezea kuwa licha ya kuwepo makampuni mengi ya kubeti amekuwa akibashiri na SportPesa pekee kwa kuwa ni kampuni kubwa, kampuni mama na haina ubabaishaji.
“Kwa ambao wanatamani kushinda na kutimiza malengo yao nawashauri waendelee kucheza na SportPesa, waamini kuwa ipo siku watashinda kama mimi nilivyoshinda. Hata mimi bado naendelea kucheza kwani malengo yangu ni kushinda ile Bilioni 1.1 na naamini nitaipata,” amesema David.
Naye Mkuu mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa, Sabrina H. Msuya alimpongeza mshindi na kumhimiza kuwa balozi kwa wengine. ‘’Kwanza nikupongeze kwa ushindi huu wa Supa Jackpot. Wewe ni mmoja wa watanzania wengi wanaoshinda mamilioni ya Shilingi kila siku na SportPesa na kuona manufaa yake ambapo bila shaka wewe ni shuhuda.
“Niwakumbushe watanzania Supa Jackpot ipo na itaendelea kuwepo kutegemeana na matokeo ya kila wiki. Endeleeni kutuamini kama ambavyo, David ametuamini na matokeo ya ushindi mtayapata’’
Ni miaka saba sasa tangu kuanzishwa kwa kampuni ya SportPesa ikiwa imetangaza jumla ya washindi 10 wa Jackpot na maelfu ya washindi wa bonasi kila wiki.
Mwisho!

