MAOKOTO Deilee yanazidi kupasua anga huku washindi wakizidi kukomba zawadi zao kila baada ya droo kufanyika.
Leo Oktoba 2 watatu wamesepa na zawaid zao baada ya kushinda.
Ni Mwinyi Milevu na Fednand Kisanga hawa walishinda simu huku mshindi mmoja akikomba zawadi ya fedha taslimu.
Anaitwa Yassin Mfalla kashinda milioni moja ambayo ni zawadi kwake kwa kushiriki Maokoto Deilee.
Hivi karibuni washindi watatu Yasinta Kilumule (Njombe), Emmanuel Ngusa(Dumila), walisepa na simu janja.
Droo hii ni sehemu ya promosheni ya Maokoto Deilee iliyoandaliwa na SportPesa kwa kushirikiana na Tigo Pesa, na pia ni muendelezo wa zawadi ambazo zinatolewa kila siku kwa washindi 10 ambao hujishindia kiasi cha TZS 20,000.
Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa makao makuu ya SportPesa, Jijini Dar-Es-Salaam, Afisa wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Lydia Solomon anasema leo ikiwa ni siku ya huduma kwa wateja, sisi kama Sportpesa tunafurahia kuwazawadia washindi wa droo ya sita katika promosheni ya Maokoto Deilee ambapo wateja wa Tigo pesa na SportPesa wamejishindia simu janja na shilingi milioni 1.
‘’Kama mnavyofahamu leo imechezeshwa droo yetu ya sita ya Maokoto Deilee, ambapo wateja watatu kutoka Chamanzi,Morogoro na Mbagala, wameshinda simu janja na shilingi milioni moja kwa mmoja, baada ya kubashiri na na kuibuka washindi wa Maokoto Deilee ya Sportpesa na Tigo pesa.
Akiongea kwa niaba ya Tigo, Meneja Msaidizi Biashara wa Tigo pesa, Fabian Felician alisema imebaki wiki moja kupatikana kwa mshindi wa 15,000,000, tunatoa rai kwa wateja wetu kuaendelea kucheza na kuingia kwenye droo ili na wao washinde.
‘’Ninapenda kuwahamasisha watanzania wenzangu hususani wateja wetu wa Tigo pesa kuchangamkia fursa hii. Nitoe rai kwa wateja wetu kuendelea kushiriki na kucheza promosheni hii ambayo imebakiza wiki moja.
Ili kuweka bashiri yako kupitia TigoPesa, wateja wanaweza kupiga *150*87#, kuchagua namba 4, na kuweka kiasi anachotaka, kisha kuweka PIN yako ya Tigopesa ili kukamilisha muamala.
Ikumbukwe promosheni hii ilizinduliwa rasmi siku ya tarehe 21 Agosti ya wiki iliyopita inajumuisha zawadi za shilingi elfu 20 kila siku, zawadi za milioni moja moja kwa mshindi mmoja kila wiki, simu janja kwa washindi wawili kila wiki na zawadi ya milioni 15,000,000 siku ya kufunga kampeni.

