Mchezaji wa Manchester City Erling HaalandMicrosoftTeams-image-

Jiji la Instabul lililopo katika nchi ya Uturuki litakuwa mwenyeji wa fainali ya Klabu bingwa barani Ulaya itakayopigwa kesho Jumamosi ya Juni 10, 2023 kati ya timu ya Manchester City ya Uingereza dhidi ya Inter Milan ya Italia.

Mechi hii itapigwa katika uwanja wa Ataturk, uliopo Magharibi mwa jiji la istanbul, katika wilaya ya Ikitelli.  Uwanja huu una uwezo wa kukusanya mashabiki  mpaka 75000, unakuwa mwenyeji wa fainali ya aina hii kwa mara ya pili, ambapo mara ya mwisho ilishuhudiwa Liverpool ya England ikitwaa taji la Uefa Champions League mbele ya AC Milan ya Italia, kwa ushindi uliopatikana kwa mikwaju ya penati, baada ya sare ya maajabu ya 3-3 ndani ya dakika 120.

Tafsiri yake ni kwamba kwa mara ya kwanza Uwanja wa Ataturk kuwa mwenyeji wa fainali ya klabu bingwa ilizikutanisha timu kutoka England na ya Italia na bahati ilikuwa kwa timu kutoka EPL, unaweza kutumia kigezo hicho pia kutabiri matokeo kupitia Sportpesa,lakini pia unaweza kutabiri huenda timu ya Italia ikatumia nafasi hiyo kulipa kisasi baada ya AC Milan kuduwazwa na Liverpool enzi hizo.

Fainali hii ni ya pili kwa Manchester City ambayo tangu kampuni ya Abu Dhabi United Investment Group walipoichukua timu hiyo mwaka 2008.

Matajiri hao wametumia gharama kubwa kuitoa Manchester City kutoka kuwa timu ya daraja la kati na kuifanya iwe tishio kwa sasa ambapo wametumia takribani euro bilioni 1.45 kwa ajili ya usajili lakini bado hawajafanikiwa kutwaa taji la UCL na hii ndio inaonekana ni nafasi kwao kutimiza ndoto zao.

The Citizen walicheza fainali yao ya kwanza ya UCL miaka miwili iliyopita lakini wakakutana na kadhia kutoka kwa timu ya matajiri wa London, Chelsea walioibuka mabingwa kwa goli 1-0.

Safari hii Man City ya Kocha Pep Guardiola wanakutana na Inter Milan ambao ni mabingwa mara tatu wa michuano hiyo na mara ya mwisho kulitwaa taji ilikuwa ni mwaka 2010 kipindi hicho walikuwa chini ya Kocha mwenye majivuno, Jose Mourinho (msimu ambao pia walitwaa Treble).

The Citizen inaelekea katika mchezo huu ikiwa na motisha ya kutwaa mataji ya ndani(EPL na FA) na wanaisaka nafasi ya kutwaa mataji matatu ,na mara ya mwisho kwa Klabu ya England kufanya hivyo ni Manchester United mwaka 1998.

Katika mechi ya nusu fainali, Manchester City waliwapa kipigo cha fedheha mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Real Madrid kwa jumla ya bao 5-1 wakati Inter Milan waliwaondosha mabingwa wa pili mara nyingi zaidi katika michuano hiyo, AC Milan walipowaadhibu bao 3-0 katika mechi zote mbili.

Zipo taarifa ambazo si za kufurahisha kutoka Manchester City ambapo Kocha wake, Pep Guardiola amesema beki Kyle Walker ana maumivu ya mgongo na hakufanya mazoezi siku ya Jumanne sawa na Manuel Akanji.

Upande wa Inter Milan mchezaji ambaye yupo mashakani kucheza fainali hiyo ni Henrikh Mkhitaryan ambaye alikuwa majeruhi sambamba na Joaquin Correa lakini Kocha Simone Inzaghi anatarajiwa kumtumia Romelu Lukaku kwenye idara ya ushambuliaji ili kupata mabao.

Wachezaji wa Inter MilanKwa mujibu wa takwimu kutoka kwa majarida mbalimbali zilizokusanywa zinaonyesha kuwa Manchester City ndio timu inayopewa nafasi kubwa ya kushinda fainali na hii ni kutokana na matokeo ya michezo iliyopita na kiwango kilichoonyeshwa na Klabu hizo.

The Citizen imepewa asilimia 42.21 wakati Inter Milan inamiliki asilimia 31.03 wakati sare ikipewa asilimia 24.75.

Ushindi wa bao 1-0 kwa Manchester City umepewa (9.14%), ushindi wa 2-1 umepewa(9.13%) na ushindi wa 2-0 umetabiriwa kuwa ni (7.15%).

Upande wa Nerrazurri ushindi wa bao 1-0 umepewa(7.43%), huku sare ya bao 1-1 imepewa (11.64%).

Mwenendo wa timu hizi katika michuano yote kwa siku za karibuni zinaonyesha katika mechi 6 za mwisho, The Citizen wameshinda mechi 4, sare 1 huku wakipoteza 1 wakati Inter wao kati ya mechi 6 za mwisho wameshinda 5 na sare 1.

Katika mechi 6 za mwisho za klabu bingwa ulaya, Man City wameshinda 3 na sare 3 wakati Inter Milan wao wameshinda 4 na sare 2.

Klabu ya Man City wamekuwa bora sana katika safu ya ushambuliaji,wamefunga magoli 93 katika mashindano yote huku wakiwa na kinara wao ni Erling Haaland  ambaye amefunga mabao 54.  Huko Inter Milan wao wamepachika mabao 71 huku mkali wao wa mabao ni Lautaro MartinezEdin Dzeko akichagiza katika hayo.

Hii ni moja ya fainali ambayo siyo tu itatukumbusha yale yaliyotokea miaka 18 iliyopita, bali inategemewa kuonyesha ubora wa kimbinu na kimchezo baina ya makocha na wachezaji wa timu zote mbili, hasa hasa Inter Milan ambao mpaka sasa wana clean sheet 5 mfululizo.

Tayari baadhi ya wachezaji nguli kama Kylian Mbappe wa PSG na Trent Alexander Arnold wa Liverpool ambao wiki iliyopita walikuwa wakishuhudia formula one huko nchini Hispania wameitabiria Manchester City kutwaa Ubingwa wa michuano hiyo.

Je wewe unafikiri timu gani itachukua ubingwa siku ya kesho baina ya mafahari hawa wawili. Weka utabiri wako na kisha weka mkeka kupitia sportpesa.co.tz or piga *150*87#

 

Share this: