Kesho Jumatano ya Juni 7,2023 majira ya saa nne usiku katika dimba la Eden Arena kwenye Jiji la Prague, Czech utapigwa mtanange wa fainali ya michuano ya kombe la Uefa Conference League ukizikutanisha Fiorentina ya Italia dhidi ya West Ham United ya Uingereza.
Fiorentina watashuka dimbani Jumatano hii wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kutochukua taji lolote kubwa tangu msimu wa 1960/61 wakati West Ham United wamefikia hatua hiyo na ni mafanikio makubwa kwao tangu wafanye hivyo 1995.
Kikosi cha Fiorentina maarufu kama ‘’Viola’’ wanaingia katika Fainali hii wakiwa na takwimu bora zaidi katika michuano hiyo msimu huu. Takwimu zinaonyesha Fiorentina, wamefunga jumla ya mabao 36 katika michezo 14 waliyocheza, huku wakiwa na kinara wa kupachika mabao Arthu Cabral mwenye mabao 7.
West Ham United nao kwa upande wao wana rekodi ya karibuni zaidi, ambapo walicheza nusu fainali ya ya Europa League msimu uliopita. West Ham wana kila sababu ya kufanya vizuri kutokana na uzoefu wa msimu uliopita, huku wakichagizwa na nyota wake wawili Tomas Sousec na Vladmir Coufal ambao walicheza kwenye Uwanja wa Eden Arena walipokuwa wakiitumikia timu ya Slavia Praha.
Katika Ligi zao za nyumbani, Fiorentina imemaliza kwenye nafasi ya 8 katika Serie A msimu huu, wakati West Ham United, imemaliza msimu wa 2022/23 ikiwa nafasi ya 14 katika ligi kuu ya EPL.
Kwa namna ambavyo West Ham amemaliza ligi msimu huu, ni dhahiri hawana nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya, mpaka hapo ambapo watakapofanikiwa kutwa taji hili, ndipo watajipatia tiketi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao.
Kwakuwa fainali hii ya Europa, kwao ni mchezo mkubwa na wa umuhimu sana katika michuano ya Ulaya baada ya miaka 33, bila shaka vijana wa Kocha Montella Italiano, Fiorentina watakua na shinikizo kubwa la kufanya vizuri.
Timu hii inaonekana ipo katika kiwango bora kwakuwa wameonekana kufanya vizuri ndani ya Uwanja katika mechi walizocheza. Timu imetengeneza nafasi 259 na kufunga mabao 83 katika mashindano yote .
West Ham United ambayo ilifika nusu fainali ya Europa msimu uliopita hawana shinikizo kubwa kwa sasa, ingawaje zipo taarifa zinazomhusisha Kocha wao David Moyes ambaye huenda akatimuliwa kazi iwapo atashindwa kutwaa taji siku ya kesho.
Ikumbukwe shinikizo kwa David Moyes ni kutokana na wagonga nyundo kutokuwa na mwenendno mzuri katika EPL hivyo, ili ajiokoe na kutopoteza kibarua chake, ni lazima abebe kombe hilo litakalowarejesha katika michuano ya Ulaya msimu ujao. (Europa League hatua ya makundi moja kwa moja ).
Duru za kimichezo zinaarifu kuwa, hii ni Fainali ya kwanza kwa West Ham United tangu miaka 40 kupita. Wameingia katika hatua hii wakiwa na rekodi bora ya kutopoteza mchezo, wakiwa wameshinda michezo yote na sare moja.
Wakizungumza kuelekea mchezo wa kesho Kocha wa Fiorentina, Vicenzo Italiano amesema ’’Ni msimu wangu wa kwanza barani Ulaya na hii ni fainali yangu ya kwanza.
Nimeridhika na nilichofanikisha kwa sasa, tumefika hatua hii ni jambo kubwa lakini tunayo kazi moja tu ya kukamilisha mpango ambao ni kutwa Kombe. Naweza kusema tumekuwa na timu tatu katika Fainali za Ulaya,Inter Milan,AS Roma na sisi ni sifa kubwa kwa mpira wa Italia na nadhani sote tuna jambo la kufanya katika Fainali’’.
Upande wa David Moyes amesema ’’ tumefurahi kufika fainali na ni mafanikio makubwa kwetu na sasa si muda wa kuzungumza sana bali tunapaswa kuhakikisha tunashinda taji’’.
Katika mechi sita za mwisho kwenye mashindano yote timu hizi zimekuwa na matokeo yanayoshabihiana kwa ubora.
Fiorentina imeshinda mechi nneimepoteza mmoja na sare moja wakati West Ham United yenyewe imeshinda michezo minne na kupoteza miwili.
Kwenye mashindano ya Europa Conference League katika mechi 6 za mwisho, Fiorentina imeshinda minne huku ikipoteza miwili wakati West Ham United imeshinda mitano na sare mmoja.
West Ham United inao mastaa ambao wanaonekana kuwa sehemu kubwa ya kikosi kilichowafikisha hapa wakiwemo Kipa Alphonse Areola, mabeki Aaron Cresswell, Kurt Zouma, Vladmir Coufal,washambuliaji kama Michai Antonio, Said Benrahma, Jarrod Bowen, Manuel Lanzini na Dany Ings.
Upande wa Fiorentina wapo Giacomo Bonaventura, Nikola Milenkovic, Lucas Martinez, Lorenzo Venuti, Alessandro Bianco, Arthur Cabral, Christian Kouame, Luka Jovic na Josip Brekalo wanatarajiwa kubeba jahazi la waitaliano hao.
Mechi hii tayari ipo kwenye tovuti yetu. Kubashiri au kucheza tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

