Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ASFCYangaSimbaSingidaAzam

Nusu fainali ya kwanza ya Klabu bingwa Afrika inanguruma leo Jumamosi ya Mei 13,2023 ambapo majira ya saa 4 usiku katika uwanja wa Stade Mohammed V, mabingwa mara 3, Wydad Athletic Club watakuwa wenyeji wa mabingwa mara moja Mamelodi Sundown kutoka Afrika Kusini wakati huo huo mechi itaakayoipa jina la mabingwa Yanga inachezwa pale Taifa saa 10 jioni.

Mechi yenye hadhi ya fainali kwa Klabu zote hizi zina mataji ya michuano hii lakini pia zimedhihirisha ubora wao katika soka la Afrika.

Ubora huo unadhihirika kupitia takwimu katika michuano hii vilevile hata kwenye Ligi wanazotoka mfano Mamelodi ndio vinara katika ligi ya PSL wakiwa na alama 69 wakati Wydad wanakamata nafasi ya pili kwenye Ligi ya Batola nchini Morocco na wana alama 53 ikiwa moja nyuma ya vinara AS FAR yenye alama 54.

Ukiachana katika Ligi zao,turejee namna walivyofika katika hatua hii ambapo hatua ya makundi, Wydad ambao walikuwa kundi A,walifuzu kibabe kama vinara kwa kukusanya alama 15 ,na kuwaacha Js Kabylie,Petro Atletico na As Vita na Wydad ilikuwa ni timu ya pili kwa kufuzu ikiwa na alama nyingi zaidi nyuma ya Raja Casablanca katika hatua ya makundi.

Mamelodi ambao walikuwa kwenye kundi la kifo, lakini walimaliza vinara wakiwa na alama 14, wakiwa juu ya mabingwa wa kihistoria wa kombe la klabu bingwa Africa ,Al Ahly ,Al Hilal Omdurman na Cotton Sports.

Baada ya kufuzu robo fainali, Wydad waliitungua Simba ya Tanzania kwa penati 4-2 baada ya matokeo ya jumla ya 1-1 ,lakini Mamelodi waliwasambaratisha CR Belouzdad ya Algeria jumla ya bao 6-2.

Mamelodi ndio timu ambayo hadi sasa haijapoteza mchezo katika michuano hii,kwani wamecheza mechi 10, wameshinda 8, sare 2, wamefunga mabao 35 na kuruhusu bao 10, wamekusanya alama 26 na hawakuruhusu bao katika michezo miwili.

Wanakutana na Wydad ambao wamepoteza mechi 3,sare 1, wamefunga mabao 15 na kuruhusu bao 4, wamekusanya alama 19 na hawakuruhu wavu wao kuguswa katika mechi 7.

Takwimu zinaonyesha Mamelodi imeshinda mechi 5 nyumbani na 3 ugenini,lakini Wydad wao wameshinda mechi 5 nyumbani lakini ugenini wameshinda 1 pekee ambapo huko wamepoteza mechi 3, hivyo vijana wa kocha Sven Vandebroeck watahitaji kuondoka na ushindi nyumbani kabla ya mchezo wa marudiano huko Afrika Kusini.

WydadTakwimu zinaonyesha kuwa Mamelodi wanafunga sana mabao (35), ingawa Wydad wameruhusu mabao machache sana(4) ,vilevile wana Clean Sheet (7), hivyo ni kipimo kati ya safu bora ya ushambuliaji na ya ulinzi.

Nyota wa kuchungwa wa Mamelodi ni Cassius Mailula ambaye ndiye kinara wao wa mabao katika michuano hii (7) akifuatiwa na Peter Shalulile (5) na Thopeko James(3) lakini upande wa Wydad wanajivunia mshambuliaji wao Bouly Junior Sambou mwenye mabao (7) pamoja na Yahya Jabrane mwenye magoli (3).

Vilevile Mamelodi wana mpishi wa mabao Aubrey Maphosa Modiba (2) na Haashim Domingo (1) wakati Wydad wana Attiaj Allah na Saif Eddie (1) kila mmoja.

Kuelekea mchezo huu timu hizi zilicheza mechi 5 zilizopita katika mashindano yote ambapo Mamelodi imeshinda 4 na sare 1, mchezo wa mwisho Mamelodi wamewachapa Marumo Gallants kwa bao 2-0, wakati Wydad wameshinda 3, wamepoteza moja na sare moja,na mchezo wa mwisho wameichapa Chabab Mohammed bao 3-1 tena chini ya Kocha mpya Sven Vandebroeck.

Historia inatuambia miamba hii ya soka imekutana mara 10 katika michuano hii ya Klabu bingwa Afrika, Wydad imeshinda mechi 4, Mamelodi imeshinda 3 na sare 3, huku katika mechi 5 za mwisho kukutana tangu 2017, Wydad imeshinda 3, sare 1 na Mamelodi imeshinda 1.

Je historia ambayo inaonekana kuibeba Wydad dhidi ya Mamelodi itajirudia?

Tabiri mchezo huu kupitia Sportpesa zipo odds za nono na machaguo mengi ujishindie dau la kushiba.

Kundi walilotokea Mamelodi ndilo limeingiza timu 2 hatua ya nusu fainali,wao na Al Ahly na ikumbukwe pia Wydad ndio mabingwa watetezi wa michuano hii.

Mechi hii inaweza kutupa taswira ya kuurejesha pengine mechi ya kisasi kati ya Wydad na Al Ahly ambao wao watakipiga na Esperance ya Tunisia.

Vilevile inaweza turejeshea kwenye kumbukumbu ya mechi ya marudiano ya makundi kati ya Mamelodi na Al Ahly ambao walipokutana mabingwa wa kihistoria walichapika kisawasawa katika mchezo uliopigwa Afrika Kusini.

Tayari mechi hii ipo kwenye tovuti yetu. Ili kucheza au kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

Share this: