MILIONI 56,383,640 ZA SUPA JACKPOT BONUS YA SPORTPESA ZAENDA BAGAMOYO.
Ukisikia bahati ya mtende ndio hii. Mfugaji kutoka kata ya Migude, Bagamoyo Abibu Mauridi Omari, ameshinda Sh 56,383,640, kama bonasi ya Supa Jackpot ya SportPesa, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 16 kati ya mechi 17 za Supa Jackpot iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
KUCHEZA
Akizungumza katika ofisi za SportPesa, Dar-Es-Salaam, Abibu anasema alianza kucheza na SportPesa mwaka 2022, baada ya kukutana na mfanyakazi mwenzake ambaye alijiunga naye katika kampuni ya Kazi Ranch, iliyopo Bagamoyo, mwaka mmoja uliopita.
‘’Mimi nilianza kucheza SportPesa mwaka jana, baada ya kukutana na Nurdin Kizenga. Huyu jamaa alijiunga na kampuni yetu na kuajiriwa kama afisa mifugo, mwanzoni mwa mwaka jana.
Sasa kilichokuwa kinanishangaza, wote tuna simu janja, lakini yeye mara nyingi alipokuwa yuko huru alikuwa bize na simu yake.
Mara kwa mara nilijiuliza ni nini kinamfanya awe busy na simu yake kila mara anapopata nafasi. Siku moja nilimuuliza ebana, mwenzangu mbona uko busy sana na simu yako. Bwana Nurdin alitabasamu na kuniambia yeye anabeti sana, kama njia nyingine ya kutafuta kipato cha ziada’’. Anasema Abibu.
TOFAUTI YA SPORTPESA NA WENGINE
Anaendelea kwa kuelezea Nurdin anacheza na makampuni mengi ya kubeti, SportPesa ikiwa moja wapo. Yeye Abibu omari ilibidi aanze kufuatilia kuhusu hayo makampuni kuhusu huduma na bidhaa zao.
‘’Nilijaribu kufuatilia kwa maana kampuni nyingi zipo mitandaoni na nikabaini SportPesa wanatangaza washindi wao karibu kila siku au kwa wiki hadi mara tatu. Nilipoendelea nikajakujua washindi wengi ni wa Jackpot bonus, na wanashinda vitita vikubwa vikubwa, kama milioni 4, 5, 7, 9, 20, 30 na hata 40 na ushehe.
Viwango hivyo vya bonus, pamoja na odds kubwa za SportPesa zilinivutia mimi kubakia na SportPesa pekee. Niwe mkweli sijawahi kushinda kiasi chochote tangu nimeanza kucheza, ila nilikuwa nina imani ipo siku nitashinda hela nyingi’’.
Akiongelea mkeka wake wa Supa Jackpot bonus, Abibu anasema yeye huwa na kawaida ya kufuatilia mechi za Jackpot kila zinapotoka. Sasa kwa wiki iliyopita mkeka ulipotoka yeye alikuwa barabarani peke yake anaendesha boda boda.
Najua hamuwezi amini ni kwa namna gani niliweka huu mkeka ulionipa Supa Jackpot Bonus ya mil 56 na ushehe. Ni hivi kwenye simu nilikuwa na kama 5000 ambayo mara nyingi huwa naweka ili nisubiri kuweka mikeka ya Jackpot.
Nilihamisha Sh 3000 kwenye akaunti ya SportPesa na kuweka mikeka mitatu ya Jackpot siku ya Alhamisi. Ilipofika siku ya Jumamosi. Mechi za Supa Jackpot zilianza kucheza. Wakati mechi zimeanza kucheza mimi na mshkaji wangu Nurdin ingawa hatukuwa pamoja tulikuwa tunawasiliana kwa simu kujuzana kinachoendelea kwenye mechi’’. Anasema Abibu
Anaendelea kwa kusema kwa siku hiyo ya Jumamosi, mpaka mechi ya mwisho ya mwisho inacheza ambapo Lazio alikuwa anacheza na alishinda jumla ya mechi 7. Siku iliyofuata, yaani Jumapili kama kawaida yeye na Nurdin waliendelea kufuatilia matokeo mpaka pale ambapo ilikuwa imecheza Lazio ambapo alikuwa tayari amepatia mechi 15.
Kikawaida Supa Jackpot ya mechi 17, ukipata mechi 15 unakuwa tayari umepata Jackpot, hivyo yeye alikuwa na furaha na kuingiwa na kiwewe zikiwa bado mechi mbili hazijacheza.
‘’Unajua kaka muda ule ninajua nimepata timu 15, nilimpigia Nurdin na kumwambia -nimeshafikisha kiwango cha Supa Jackpot bonus, na kichwa kilishaanza kuniuma kwa wenge nililonipata. Baadae niliendelea kuangalia matokeo na mechi ya 16, ikawa imemaliza kucheza ambayo nayo nilipata.
Hapo nilichanganyikiwa zaidi kwani nilikuwa nimebakiza mechi moja, ambayo ndio ilikuwa Rotherham VS Cardif. Mimi sikujua kama mechi ile imeahirishwa, kwa kuwa nilienda kulala kutuliza mizuka ambayo tayari ilikuwa imepanda.
Ilipofika Jumatatu, Nurdin aliniambia, ile mechi niliyokuwa naisubiria ya Rotherham na Cardif imeahirishwa na kwamba itachezeshwa droo mubashara kwenye TV. Nilimpelekea Nurdin simu yangu kwa kuwa sikutaka presha.
Anamalizia kwa kusema droo ilipangwa kurushwa mubashara saa nane na dakika arobaini na tano, lakini muda huo Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu alikuwa anahutubia hivyo, ilipelekwa mbele mpaka baada ya baada ya Rais kumaliza.
Droo ile ilifanyika saa tisa alasiri na baada ya matokeo kutangazwa Rotherham alikuwa ndio ameshinda, hivyo nilipata hiyo mechi na ikawa ndio ya 16. Baada ya dakika kama 10 nilipata SMS ya hongera kutoka SportPesa ikinitaarifu nimeshinda Supa Jackpot bonus ya Sh 56,383,640.
Abibu anasema baada ya kupokea sms ile hakujua ni Milioni hamisini na sita bali alijua ni Milioni tano.
Nilienda mbio kumfuata Nurdin na kumwambia nimeshinda milioni tano na baada ya Nurdin kucheki vizuri alianza kuruka ruka kwa furaha na kuniambia kijana umekuwa Tajiri. Kwa kweli sikumwelewa ana maanisha nini kwa kuwa mtu hawezi kuwa Tajiri kwa milioni tano.
Nurdin aliniambia nimeshinda milioni 56, na hivyo shangwe lilianza hapo. Baadae kidogo mtoa huduma kutoka SportPesa alipiga simu na kunipa maelekezo ya namna ya kuja ofisi za SportPesa ambapo ndio nipo sasa.
Akizungumza kwa niaba ya SportPesa mkuu wa kitengo cha mawasiliano Sabrina Msuya alimpongeza mshindi na kumtaka atumie ushindi wake kwa staha na awe balozi kwa wengine. ‘’Kwanza nikupongeze kwa ushindi huu wa Supa Jackpot Bonus, ambao naona umekujia katika wakati muafaka.
‘’Wewe ni mmoja wa watanzania wengi wanaoshinda mamilioni ya Shilingi kila siku na SportPesa. Ni majuzi tu nimetoka kuwaasa watanzania waiamini SportPesa na manufaa yake watayaona. Wewe ni shuhuda, na umepata kitita kikubwa kwenye kampuni nyingine huwezi kupata kama bonasi.
‘Niwakumbushe watanzania Supa Jackpot ipo na itaendelea kuwepo kila wikiendi kutegemeana na lini haswa inatoka. Endeleeni kutuamini kama ambavyo Abibu ametuamini na matokeo ya ushindi mtayapata’’
Akimalizia Abibu anasema pesa aliyoipata atanunulia nyumba na nyingine atafanyiabiashara.

