Siku ya Alhamisi ya wiki hii, barani ulaya patakuwa hapatoshi , wakati timu ya taifa ya Italia itakapoikaribisha timu ya taifa ya Uingereza kwenye Uwanja wa Diego Armando Maradona katika mji wa Napoli, majira ya saa 4: 45 usiku.
Timu hizi mbili, zitavaana katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Euro 2024, baada ya timu zote mbili kutofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa waliyoshiriki siku za karibuni. Uingereza pamoja na kushiriki kombe la dunia, hakufanya vizuri kabisa ikiishia hatua ya makundi.
Italia wao kwa upande wao, mambo yalikuwa magumu zaidi, ambapo hawakuweza hata kufuzu, kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia, Mwaka 2022 kule nchini Qatar. Mechi hii ya kufuzu Euro 2024, inawakutanisha mafahari hawa wawili, ni muhimu kwa timu yoyote kati yao ili kupata ushindi katika pambano hilo gumu.
Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kubwa, ni moja kati ya mechi kubwa za kusisimua utakaowakunaisha wachezaji wengi kutoka klabu kubwa za Ulaya.
Timu hizo kwa siku hivi karibuni zimekutana mara tatu, kati ya hiyo mmoja pekee Italia ilipata ushindi wa bao 1-0 katika Ligi ya Taifa ya UEFA.
Ilikuwa ni Septemba 23, 2022 wakati Italia wakiwa wenyeji wakiwakaribisha Uingereza. Timu hizo zikakutana tena, Juni 11 mwaka 2022 ambazo zilitoka suluhu.
Wakaja kukutana tena Juni 11, 2021 katika michuano ya Uefa , 2021 na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Kuelekea mchezo huo, timu yoyote ina nafasi ya kupata ushindi kutokana na ubora, maandalizi ya kila timu ambayo wameyafanya.
Hivyo ni nafasi kwako, mchezaji wa SportPesa kuweka mkeka wako kwa kuangalia historia ya michezo, ambayo timu hizi zimekutana.
Katika mchezo huu muhimu kwa pande zote mbili, Uingereza huenda wakamkosa mshambuliaji wao tegemeo Marcus Rashford anayeichezea klabu ya Manchester United.
Staa huyo, ataukosa mchezo huu pamoja na ule dhidi ya Ukraine kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa anaitumikia klabu yake ya Manchester United, wiki iliyopita dhidi ya Fulham.
Kukosekana kwa kiungo huyo, huenda kukawa pengo kubwa kwa Uingereza kutokana na mchango umuhimu mkubwa aliokuwa nao katika katika siku za hivi karibuni kupitia timu yake ya Manchester United ambapo mpaka sasa ameshafunga jumla ya magoli kikosi hicho.
Rashford alipata majeraha hayo katika mchezo wa mwisho wa Nusu Fainali ya kombe la FA waliocheza dhidi ya Fulham.
Nyota huyo alifunga mabao matatu pekee katika Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Qatar, mwaka wa jana, akiwa na magoli sawa na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa na Arsenal Bukayo saka.
Kwa upande wa Meneja wa Italia, Roberto Mancini yeye ana matarajio ya kupata ushindi katika mchezo huo baada ya kikosi chake kuchanganya damu changa na wakongwe.
Mancini ataingia uwanjani katika mchezo huo, akiwa na rekodi ya kutofungwa katika michezo 25, akishinda 20 huku mingine akitoka sare .
Meneja huyo anajivunia kucheza michezo mingi ya kirafiki ya kimataifa na timu kubwa, akiamini vijana wake aliowaita katika kikosi chake kupata uzoefu na kutengeneza hali ya kujiamini.
“Ili upate ushindi katika, ni lazima uchezemichezo mingi ya kirafiki ya kimataifa kwa ajili ya kuwaongezea hali ya kujiamini na uzoefu wachezaji wako,” alizungumza hivi karibuni Mancin.
Wachezaji baadhi vijana walioitwa katika kikosi hicho ni, Gianluigi Donnarumma (AC Milan goalkeeper), Nicolo Barella (Inter Milan midfielder), kiungo mchezeshaji Manuel Locatelli na winga Federico Chiesa wote wanaoichezea Juventus.
Mancini anatumia mfumo wa 4-3-3, kikubwa anaangalia katika kumiliki mpira muda mrefu akiowatumia viungo wake wawili wachezeshaji ambao ni Jorginho and Marco Verratti.
Wakati wakimiliki mpira, wanafanya mashambulizi ya kushitukiza katika goli la wapinzani wao ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ya ushindi na sio kitu kingine.
Kwa upande wa Uingereza ambao wao wamezoeleka na mfumo sawa na wa Italia wa 4 -3- 3 kikosi chao kina mabadiliko kidogo ambapo Kocha Gareth South Gate amemchagua beki wa kulia wa Manchester City Kyle Walker kuzuia upande wa kulia, akimuacha Kieran Tripper.
Akizungumza na waandishi wa Habari siku ya Alhamisi iliyopita Gareth alisema Uingereza kama timu ipo tayari kupambana na Italia na tayari kwa kuwaangalia vijana wake kama Henderson na Harry Kane anaona namna walivyo na njaa ya kupata ushindi.
Wengine waliochaguliwa ni pamoja na Ivan Toney,mchezaji wa Manchester city ambaye anachukua nafasi ya Cullum Wilson ambaye kiwango chake kimetetereka kutokana na majeruhi.
Waliothibitishwa kwamba hawatakuwepo kabisa kwenye mechi hii, ukiachia Marcus na Cullum ni pamoja na Ben Whites, Trent Alexander Arnold Raheem Steerling.
Tunategemea mchezo wa ushindani kwa timu zote mbili. SportPesa tayari tumeshakuwekea mechi hii kati tovuti yetu sportpesa.co.tz

