skip to Main Content
SportPesa Waiongezea Mkataba Namungo FC 
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas na Afisa Mtendaji wa Namungo FC Omari Kaaya wakiweka sahihi kwenye maadhimisho ya kuongeza mkataba na timu wa Namungo jijini Dar es Salaam

SportPesa waiongezea mkataba Namungo FC 

SportPesa waiongezea mkataba Namungo FC 

Mkataba wa Sportpesa na NamungoKAMPUNI ya michezo na Burudani ya SportPesa Tanzania, imeongeza mkataba wa mwaka mmoja wa  udhamini timu ya Namungo ya Ruangwa, Lindi.

SportPesa imeingia makubaliano hayo ya kuendelea na udhamini Namungo baada ya pande mbili zote kufikia muafaka mzuri wa kuongeza mkataba.

Namungo ni kati ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambayo hivi sasa ipo katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 13 ikicheza michezo kumi pekee.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa SportPesa, Mheshimiwa Tarimba Abbas alisema kuwa wana furaha kubwa kufikia makubaliano mazuri ya kuendelea na udhamini Namungo.

Tarimba alisema kuwa mkataba wa mwaka mmoja wameingia na Namungo baada ya ule wa awali ukitarajiwa kumalizika mapema Januari, 2022.

“Tunafuraha kubwa kufikia makubaliano mazuri na Namungo baada ya kufanya mazungumzo yaliyotushawishi kuendelea na udhamini timu ya Namungo”.

“Tunaamini kwa kupitia udhamini huu tulioutoa Namungo utasaidia katika masuala ya maendeleo katika timu hiyo inayoshiriki ligi Kuu ya NBC”.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas na Afisa Mtendaji wa Namungo FC Omari Kaaya wakiweka sahihi kwenye maadhimisho ya kuongeza mkataba na timu wa Namungo jijini Dar es Salaam

“Kama SportPesa tutaendelea kuunga mkono mchezo wa soka kwa kupitia udhamini ambao tunaoutoa kutoka katika klabu mbalimbali zikiwemo klabu kubwa za Simba na Yanga,”alisema Tarimba.

Kwa upande wa Namungo, Mtendaji Mkuu (C.EO) wa timu hiyo, Omary Kaya alisema kuwa “Tunaishukuru SportPesa kwa udhamini ambao imekuwa ikitupatia tangu ilipoanza kutudhamini”.

“Hivyo tutaendelea kufanyakazi pamoja na SportPesa kwa kutimiza masharti ya kimkataba ikiwemo kuwatangaza vizuri”.

“Nichukue nafasi hii kuwapongeza SportPesa kwa juhudi kubwa wanazoendelea katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha mchezo wa soka unapiga hatua kupitia udhamini wanaoutoa,”alisema Kaya.

Taarifa zaidi kutusu Sportpesa bonyeza hapa

Mwisho

Share this:
Back To Top