YANGA YATOA TAMKO ZITO KESI YA KUMUONDOA RAIS INJINIA HERSI

ByJoel Thomas

July 17, 2024
Rais wa Yanga Injinia Hersi SaidRais wa Yanga Injinia Hersi SaidRais wa Yanga Injinia Hersi Said
YANGA
Ally Kamwe

Uongozi wa Yanga leo Jumatano umetoa ufafanuzi mzito kuhusiana na sintofahamu iliyozuka kutokana na maamuzi ya mahakama kuhusu maamuzi ya kesi ya watu wawili waliojitambulisha kuwa Wanachama wa Yanga, ambao wameshinda kesi ya kutoutambua uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said.

NINI KIMETOKEA?

YANGA
Mama, Fatma Karume (kushoto) na Injinia Hersi (kulia)

Taarifa ambayo iliripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari jana Jumanne ni kuhusu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, ambayo imeamuru Uongozi wa timu ya Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye timu hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.

Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Injinia Hersi na wenzake ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.

Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.

Injinia Hersi alianza kuiongoza timu hiyo kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko, ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne (hadi 2026) kwa mujibu wa Katiba ya timu hiyo.

Maadhimio ya kesi hiyo ambayo  ilikuwa dhidi ya Baraza la wadhamini wa Yanga ni kuhusu kuikabidhi klabu kwa mtu wasiyemjua wala asiyekuwa Mwanachama wakati kesi inafunguliwa mwezi Mei mwaka 2022 siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa klabu uliomuweka madarakani Rais wa Yanga Eng Hersi Said.

Awali walifungua kesi hiyo Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kinyerezi jijini Dar, kabla ya kushauriwa kuihamishia katika Mahakama ya Kisutu.

Walipinga kutumika kwa katiba ya mwaka 2020 ambayo ilitumika kwenye uchaguzi Mkuu uliouweka uongozi uliopo madarakani wakisema Katiba hiyo sio halali. Inasemekana RITA waliitwa kutoa ushahidi na wakasema wanaifahamu Katiba ya mwaka 2011 ambayo ipo ofisini kwao na hiyo ya mwaka 2020 hawaitambui.

Baada ya kupata hukumu yao mwezi Agosti mwaka 2023 Juma Magoma na Geofrey Mwaipopo wameona hakuna utekelezaji wa hukumu hiyo hata baada ya kuwasilisha kwa wahusika wakaamua kufungua kesi ya kukazia hukumu ambapo itatolewa maamuzi mwezi Agosti tarehe 5 mwaka 2024, ili hukumu hiyo ianze kufanya kazi.

Hii inategemewa Mkutano Mkuu wa Yanga kuitwa ambao utajumuisha Wanachama wote hai sio wawakilishi wa matawi pekee (kama ilivyo sasa), na kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa klabu kwa kufuata katiba ya mwaka 2011. Kama hili litatokea maana yake Rais wa sasa Injinia Hersi na timu yake watakuwa wameondoshwa madarakani kwakuwa watakuwa wameingia isivyo halali.

WALICHOSEMA YANGA

YANGA
Wakili, Simon Patrick

Yanga kupitia kwa Mkuu wa kitengo cha sheria wa klabu hiyo, Wakili Simon Patrick wametolea ufafanuzi wa sakata hilo ambapo Wakili Simon Patrick amesema: “Wanachama wawili wanojiita wanachama wa Yanga Juma Ally na Mwaipopo walifungua kesi kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu dhidi ya bodi ya wadhamini wa Yanga (mlalamikiwa namba moja ) Mama Fatma Karume ( mlalamikiwa namba mbili ) , Abeid Abeid (mlalamikiwa namba tatu) madai makubwa waliyonayo ni matatu.

“Kwanza, hawalitambui baraza la wadhamini wa Yanga, pili wanadai wanachama wote sio halali kwa sababu hawaitambui hii katiba ya 2010 kwa maana hiyo viongozi wote ambao ni wanachama chini ya hii katiba hatufai na wanaiomba Mahakama ituondoe wote.

“Lalamiko la tatu ni kwamba kazi zote zilizofanywa na viongozi waliopo madarakani ni batili. Jopo la wanasheria wa timu hiyo limepanga kupeleka maombi kuomba kuongezewa muda wa kuomba kufanya mapitio ya kesi, hii ambayo iliamuliwa mwaka 2013, sisi kama klabu hatukuwa tunajua nini kinaendelea na muda wa kuomba mapitio umeshapita.

“Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho tumefanya na muda wowote kuanzia kesho tutaitwa kusikiliza na tunaimani Mahakama itatutendea haki kwa sababu hatukuwa tumeshirikishwa.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.