SpjCharlesSpjCharles

Kampuni ya ubashiri na burudani SportPesa, imeendeleza jadi yake ya kuwawezesha watanzania kupitia bidhaa yake ya Jackpot ya kati kati ya wiki na Jackpot ya mwisho wa wiki yaani Supa Jackpot kupitia  Supa Jackpot bonus zake.

Wiki hii imeshuhudia washindi wawili wakijishindia zaidi ya milioni 15 ya bonus za Supa Jackpot.

Wakwanza ni Oliveira John Tarimo, huyu ni mkazi wa Iringa mjini, eneo linaloitwa Ihesa, yeye alijishindia kitita cha Sh 10,570,787 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13 za Supa Jackpot.

Wa pili ni huyu ni Charles Mukiza Kabwebwe mkulima wa Alizeti kutoka Tabora yeye alijishindia kitita cha Sh 5,423,697 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 14 kati ya mechi 17 za Supa Jackpot za wiki iliyopita.

Wakizungumza katika ofisi za SportPesa, Oysterbay jijini Dar-Es-Salaam, Oliviera anasema alianza kucheza na SportPesa miezi saba iliyopita, baada ya kuona marafiki, jamaa na ndugu zake wawili Aggrey na David wakicheza na kushinda kiasi cha Sh 2,000,000.

‘’Mimi nilijifunza na kuanza kucheza na SportPesa Mwaka 2022 Mwezi wa 11. Nilikuwa nakaa na washikaji nawaona wanacheza muda mwingine walikuwa wanaongea namna walivyokuwa wanashinda au muda mwingine wamekosa labda mechi moja au mbili.

Sasa kilichonifanya nikaanza kucheza nakumbuka ilikuwa wakati wa kombe la dunia ambapo nina ndugu zangu mmoja anaitwa Aggrey na mwingine David. Hawa katika kipindi hicho walishinda milioni mbili.

Kwa kuwa nilikuwa niko nao karibu, kitendo kile kilinisukuma kuamini kwamba hata mimi naweza, hivyo niliwaomba wanifundishe. Sikuchukua muda mrefu nikaanza kucheza huku siku nyingine nikiwafuatisha kwa namna ambavyo wameweka mikeka yao’’. Anasema Oliviera.

Anaendelea kusema kuwa anamshukuru mungu wakati anajifunza kwa mara ya kwanza alishinda Sh 15,000. Anasema hali ile ilimsukuma kuendelea kuweka jitihada zaidi katika kucheza michezo mbali mbali ya SportPesa.

Naye mshindi wa SportPesa bonus ya Sh 5,423,697 Charles Mukiza Kabwebwe anasema kwa upande wake alianza kucheza na SportPesa miaka kama sita iliyopita. Nakumbuka bado nilikuwa nasoma na pale shule kulikuwa na vijana wenzangu ambao walikuwa wanabashiri na kushinda.

Sasa kule kushinda kwao kulitupa hamasa sisi wengine ambao kwa wakati ule tulikuwa hatubashiri wala kucheza aina yoyote ya michezo ya kubeti au Kasino ya mtandao.

‘’Mimi nilianza kucheza mwaka 2017, Nakumbuka wakati ule mimi nilikuwa bado nipo shule, sasa rafiki zangu karibu nane wote walikuwa wanapenda kubeti. Mara nyingi walikuwa wakipata hivi vihela vidogo vidogo vya kawaida.

Sasa si unajua wenzako wakishinda wanakuja kututambia na kutupa mizuka pengine na sisi au mimi naweza kucheza na kushinda hela kama wao. Ki ufupi kilichonivutia pia ni namna mtiririko wa washindi walivyokuwa wanatajwa, hasa hasa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii na kwenye magazeti’’. Anasema Charles

Kuhusu mikeka yao ambayo imeshinda Oliviera anasema yeye aliweka mkeka wake siku ya Jumatano ya Tarehe 19 2023. Baada ya kuweka siku ya ijumaa alipata timu 8 kati ya timu 13. Siku iliyofuata yaani Jumamosi usiku wa Tarehe 22 alipata timu nne.

‘’Kwanza mimi huwa na tabia ya kuweka zaidi ya mkeka mmoja katika kila Jackpot ya SportPesa.  Nina wastani wa kuweka kuanzia mikeka mitatu mpaka mitano kila wiki.

Sasa unajua baada ya kuweka mikeka ile nilianza kuzifuatilia timu siku ya ijumaa. Kitu kizuri ni kwamba siku hiyo nilibahatika kupata matokeo kwenye timu nane. Ilipofika kesho yake sikufuatilia timu hata moja kwa kuwa nilikuwa bize sana.

Nakumbuka ilikuwa usiku nilipata sms ya hongera. Lakini muda ule sms inaingia sikuitilia maanani, kwakuwa nilikuwa nachati na watu kama watatu tofauti. Ilipopita muda wa kama dakika 40 hivi na ushehe nikakumbuka kuna sms iliingia ila sikuitilia maanani.

Sasa baada ya kuifungua ndio niliona kiwango cha Sh 10,570,787.

Jackpot Bonus WinnerAanaendelea kuelezea kuwa muda huo alikuwa amekaa na mwanae sebuleni na baada ya kuiona sms ile na kuthibitisha kwa macho kwamba ni milioni kumi na ushehe alinyanyuka kwa furaha kutoka kwenye kochi alilokuwa amekalia na kuanza kushangilia.

‘’Kwa kweli kwa wakati ule siwezi kuelezea furaha niliyokuwa nayo. Na hata mwanangu hakuwelewa kwa usahihi furaha yangu ilitokana na nini zaidi ya kuona nikimkumbatia na kushangilia pamoja nae’’.

Naye Charles Kabwebwe anaelezea kuhusu mkeka wake wa Supa Jackpot ulioshinda, kwamba siku ambayo alibashiri aliweka jumla ya mikeka mitatu, lakini yeye hakusumbuka kuzifuatilia timu alizoziweka katika mikeka yake.

‘’Unajua mimi baada ya kuweka ile mikeka mitatu niliendelea na mishe zangu. Sikutaka kujipa presha, kufuatilia hizo timu. Nashukuru Mungu siku ya nne usiku baada ya kuwa nimeweka mikeka yangu nilipata sms ikinipa hongera kwa kushinda Supa Jackpot bonus kwa mechi 14 kati ya mechi 17.

Unajua sisi wa mikoa ya mbali na Dar-es-Salaam mzunguko wa hela sio mkubwa ki hivyo. Na hata matumizi yetu kwa siku, wiki na mwezi ni madogo. Kwa hivyo ilivyoingia sms ile ya Sh 5,423,697 ilinishtua sana.

Ilibidi niwasiliane na wazazi wangu na tushauriane. Nashukuru Mungu waliniunga mkono na leo nipo hapa kwenye uhakiki na makabidhiano wa mfano wa hundi na kutoa ushuhuda wangu.

Wote Oliveira na Charles wanawashauri watanzania kucheza na SportPesa hasa hasa jackpot zao kwani sio lazima mkeka wako ushinde kwa asilimia 100 ndio upate pesa.

Oliviera ‘’Mimi napenda kuwaasa watanzania haijalishi umeshacheza kwa muda gani au umepoteza kiasi gani. Cha umuhimu ni kwamba tumia kiasi kidogo cha buku buku kila wiki kucheza hizi Jackpot na mambo yanaweza kukuendea vizuri kama mimi.

Charles ‘’Mimi kwa upande wangu niwaambie wasikate tamaa. Kama ambavyo nilikuwa naona washindi wengine wakitangazwa na mimi leo nimetangazwa na kuingia katika historia ya washindi wa Jackpot bonus ya Supa Jackpot na wao wanaweza kushinda kama mimi. Hivyo wasichoke kubashiri.

Akiwapongeza washindi hawa wawili Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya SportPesa, Sabrina Msuya aliwataka wasibweteke na waendelee kucheza kwani wanaweza wakaja kushinda Jackpota kubwa au wakaendelea kushinda Jackpot bonus kwa viwango vya juu zaidi ya hivi walivyopata sasa.

Supa Jackpot

Niwaase tu kwamba ushindi huu usiwe ndio mwisho wa kucheza. Endeleeni kupambania mahela hayo yaliyopo kwenye Jackpot zetu. Si mnafahamu kwenye supa Jackpot kuna Jackpot mbali mbali za viwango tofauti.

Kuna ya mechi 17, 16,15,14 na 13. Jackpot zote hizi kila moja ina kiwango chake cha ushindi. Haufungwi na vigezo wala masharti kwani unaweza ukacheza zote kwa mpigo na ukapata ushindi au bonus kwenye Jackpot zote.

Supa Jackpot wiki hii imesimamia 1,109,975,029

 

Share this: