Mchezo wa jackpot kutoka SportPesa, unaonekana ukiendelea kunufaisha vijana wengi na kuwaongezea nafasi ya kuboresha Maisha yao.
Safari hii, Bwana Omary Ibrahim Mugisha, amejishindia kitita cha Tsh 4,273,156, kama Jackpot bonus baada ya kucheza Jackpot ya mechi 13, na kuweza kupatia kwa usahihi mechi 11.

Mshindi huyu, anatokea maeneo ya Tabata, Kisukuru jijini Dar-Es-Salaam anajihusisha na shughuli za ujasiriamali.
Akizungumza katika ofisi za SportPesa Oysterbay, Dar Es Salaam, Omary anasema alianza kucheza na SportPesa zaidi ya mwaka sasa na amefanikiwa kushinda zawadi ndogo ndogo.
“Nimeshawahi kushinda laki, laki 5 na laki 7 kwenye Multibet” Alisema Omary. Hiki ndio kiasi kikubwa nimeshawahi kushinda kwa mara ya kwanza.
Omary aliendelea kusimulia kuwa alifahamu SportPesa kupitia matangazo ambayo alikuwa akiyaona kwenye Luninga na mitandao ya kijamii.
“Nilishawishika kucheza na SportPesa baada ya kuona zawadi zinazotolewa, hivyo nikaona ili niweze kushinda ni lazima na mimi niwe nacheza hasa michezo ya Jackpot”.
Kwa kawaida huwa nacheza mikeka kuanzia 15 hadi 20 kwa wiki, na huwa nacheza michezo yote miwili,yani Mid- Jackpot na Supa Jackpot, kwa hiyo inanipa wigo mpana wa kuweza kushinda.
Kuhusu mkeka wa Jackpot ya katikati ya wiki alioshinda Omary, aliweka mikeka 20, na kwa kawaida huwa anapenda kuangalia mechi zote hadi mechi zinapokaribia kuisha.
“Nilifungua mkeka mmoja, nikaona michezo yote nane imetiki, ikawa imebakiwa mikeka 5, nikasema hapa kuna uwezekano wa kushinda hata nikipata michezo 10 nina uhakika wa kupata bonus”.
Zillisha mechi 8, zikaja ya tisa ikakubali, ikaja mechi ya 10, zikawa zimebaki mechi 3, nikawa na amani kwani nilijua hata nisiposhinda ile Jackpot ya zaidi ya milioni 600, basi nitaondoka na mzigo wa maana”.

Anaendelea kusema ilikuwa ni mida ya saa tano usiku, wakati nasubiria mechi ziiishe, wakati huo nilikuwa sijajua ni kiasi gani ningeweza kushinda, kwa sababu kuna kanuni ambayo inaonyesha hata kama umepata mechi 11, huwezi jua umeshinda kiasi gani hadi SportPesa watakapotangaza.
“Baada ya hapo nilizima simu, na kwenda kulala, nikasema nitaangalia kesho majibu kuwa nimeshinda kiasi gani, nilivyoamka asubuhi niliangalia balance kwenye akaunti yangu ya SportPesa, na kuona kiasi ambacho nilikuwa nimeshinda, hapo ndipo furaha yangu ilikamilika”.
Omary alifurahi kuongea na mtoa huduma kwa kuwa alipata uhakika wa malipo na baada ya hapo nilianza mchakato wa kuja ofisi za SportPesa, kwa ajili ya kufanya hatua zote za uhakiki, kujaza fomu na pia kupiga picha ya makabidhiano ya mfano wa hundi”.
Naweza kusema ushindi huu wa Jackpot ya katikati ya wiki sio kitu kidogo,mpaka kuweza kufika kwenye ofisi za SportPesa, ni lazima uwe mshindi wa japo bonus au zawadi zingine,cha muhimu ni kuendelea kucheza na kutokukata tamaa.
Huwezi kushinda kila siku, mwanzoni unaweza ukashinda zawadi ndogo ndogo lakini ukafanikiwa kushinda Jackpot”.
Omary anasema pesa aliyoshinda ataweka sehemu ya pesa ya ushindi wake katika ujenzi wa mji wake na pia pesa nyingine atawekeza kama mtaji kwenye shughuli zake za ujasiriamali.
“Ningependa kuwashukuru sana SportPesa kwa kuanzisha hii michezo, inatupa nafasi wajasiriamali kuweza kuboresha maisha yetu kibiashara na kuanza kukuza ndoto zetu ili kuweza kufanya maendeleo”.
Zipo kampuni nyingi za kubashiri lakini, hakuna kampuni inayotoa Jackpot kubwa ya milioni 600 au bilioni 1 na zaidi.
‘’Mimi napenda kuwaasa watanzania haijalishi umeshacheza kwa muda gani au umepoteza kiasi gani. Cha umuhimu ni kwamba tumia kiasi kidogo cha buku buku kila wiki kucheza hizi Jackpot na mambo yanaweza kukuendea vizuri kama mimi.
Akizungumzia ushindi wa Omary, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya alimpongeza Omary kwa ushindi wa bonus ya Jackpot na kumtaka aendelee kupambania ndoto yake ya kushinda Supa Jackpot ya bilioni moja.
“Kwanza karibu SportPesa. Pili nachukua nafasi hii kukupongeza kwa ushindi wa bonus ya Jackpot na tatu napenda kukuasa uendelee kucheza kadri uwezavyo, kwani kama walivyokuwa washindi wengine waliopita, unaweza kushinda zaidi ya mara.”
Kuna ya mechi 17, 16,15,14 na 13. Jackpot zote hizi kila moja ina kiwango chake cha ushindi. Haufungwi na vigezo wala masharti kwani unaweza ukacheza zote kwa mpigo na ukapata ushindi au bonus kwenye Jackpot zote.
Mid- Jackpot ya wiki hii imesimamia 658,716,950

