AFCON ----AFCON ----AFCON ----

AFCON 2027: Ratiba, Matokeo, Msimamo wa Makundi

  • Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027 yanaendelea kwa kasi ambapo kwa sasa yapo katika hatua ya kusaka tiketi ya kufuzu.
  • Mashindano haya yanatarajiwa kufanyika kwa mashirikiano ya maandalizi ya nchi tatu za Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda.
  • Katika mchakato huo timu 48 zimepangwa katika makundi 12 kuanzia kundi A mpaka kundi L.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi mwenendo wa mashindano haya

Hatua za awali za kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027, zinaendelea kwa kasi ambapo kwa sasa yapo katika hatua ya kusaka tiketi ya kufuzu. Mashindano haya yanatarajiwa kufanyika kwa mashirikiano ya maandalizi ya nchi tatu za Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda. Timu 48 zimepangwa katika makundi 12 kuanzia kundi A mpaka kundi L.

SOMA HII PIA: Africa Cup of Nations 2027: Fixtures, Teams, Groups & Dates

Mchakato wa kufuzu afcon 2027

AFCON 2027
AFCON 2027

Mchakato wa kufuzu kwa AFCON 2027 umekuwa na ushindani mkali, huku timu kutoka kote barani Afrika zikipambana kusaka nafasi ya kushiriki fainali hizo za Mwakani. CAF imeweka wazi vigezo na hatua mbalimbali zitakazotumika kuchuja timu zitakazofuzu. Timu zimeangwa katika makundi tofauti, na kila kundi itakuwa na mechi za nyumbani na ugenini. Matokeo ya mechi hizi yataamua msimamo wa kila kundi, na timu zitakazofanya vizuri zitapata tiketi ya kushiriki AFCON 2027.

SOMA HII PIA: Matokeo ya Tanzania vs Nigeria : AFCON 2027 Qualifier highlights, Ratiba, Matokeo na Historia ya Mechi

Ratiba ya mechi za kufuzu

Kibu X Iwobi
Kibu X Iwobi

Ratiba kamili ya mechi za kufuzu bado ipo katika kurasa rasmi za Shirikisho la soka Afrika. Mpaka sasa timu zote zimefanikiwa kucheza mechi 4, hivyo zinasaliwa na mechi 2 tu ili kumaliza hatu hiyo. Mechi zinazofuata za kufuzu zinatarajiwa kufanyika mwezi Machi mwakani. Hii hapa ni ratiba ya mechi za mzunguko wa 5 ambazo zitachezwa mwezi Machi mwakani.

Group A & B:

Gabon vs. Morocco, Lesotho vs. Niger, Angola vs. Egypt, and South Sudan vs. Malawi

Group C & D:

Ghana vs. Ivory Coast, Somalia vs. Gambia, Eritrea vs. Kenya, and Guinea vs. South Africa

Group E & F:

Equatorial Guinea vs. DR Congo, Zimbabwe vs. Sierra Leone, Benin vs. Burkina Faso, and Central African Republic vs. Mauritania

Group G & H:

Comoros vs. Cameroon, Congo vs. Namibia, Botswana vs. Libya, and Uganda vs. Tunisia

Group I & J:

Burundi vs. Togo, Zambia vs. Algeria, Ethiopia vs. Sudan, and Mozambique vs. Senegal

Group K & L:

Cape Verde vs. Mali, Liberia vs. Rwanda, Guinea-Bissau vs. Tanzania, and Madagascar vs. Nigeria

SOMA HII PIA: Matokeo ya Tanzania vs Nigeria : AFCON 2027 Qualifier highlights, Ratiba, Matokeo na Historia ya Mechi

Makundi na msimamo wa sasa

AFCON ---- Makundi ya kufuzu
AFCON 2027 Makundi ya kufuzu

Kuendana na mfumo wa mashindano hayo, kwenye kila kundi zitafuzu timu 2 kwa ajili ya mashindano hayo. Timu hizo 2 ni zile ambazo zimemaliza katika nafasi za juu kwenye makundi yao. Timu moja tu kutoka makundi matatu yenye timu waandaaji yaani Tanzania, Kenya na Uganda ndio

Matarajio kwa Tanzania (Taifa stars)

tanfootball------------------------------------------
Kibu X Msuva

Tanzania, kupitia timu yake ya Taifa, Taifa Stars, inatarajiwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kufuzu licha ya kwamba tayari wamekata tiketi kutokana na kuwa timu mwandaaji. Baada ya uzoefu wa kushiriki AFCON zilizopita, matarajio ni makubwa kwa Taifa Stars kufanya vizuri na kujitahidi kufuzu tena. Wachezaji kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) kama vile wale wa Yanga SC na Simba SC wanatarajiwa kuunda uti wa mgongo wa timu ya Taifa ambayo pia itakuwa na maingizo ya nyota wanaocheza soka la kimataifa.

Hitimisho

AFCON 2027 inatoa fursa nyingine kwa mataifa ya Afrika kuonyesha vipaji vyao vya soka. Mchakato wa kufuzu utakuwa safari ndefu na yenye changamoto, lakini kwa maandalizi sahihi na ari ya ushindani, timu nyingi zitajitahidi kufikia fainali. Tutaendelea kukuletea taarifa zote muhimu kadri zinavyotolewa na CAF na endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa uchambuzi, live score, ratiba na matokeo ya AFCON 2027.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.