Simba SC 3-2 Namungo FC | Dakika za jiooni Oura, Rushine wapindua meza, NBC Premier League, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

Simba SC --- Namungo FCSimba SC --- Namungo FCSimba SC --- Namungo FC

Simba SC 3-2 Namungo FC | Dakika za jiooni Oura, Rushine wapindua meza, NBC Premier League, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

  • Dakika 90 zimetamatika na matokeo ni Simba SC 3-2 Namungo FC.
  • Ni katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao umepigwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
  • Ni kiungo mshambuliaji Anicet Oura aliyefunga mabao 2 na Rushine de Reuck, ndio waliopeleka kilio kwa Namungo.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu za mchezo huu.

Simba SC 3-2 Namungo FC, ndivyo ambavyo ubao wa matokeo wa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam umeonyesha mara baada ya dakika 90 kutamatika. Mchezo huu wa Ligi Kuu ya NBC umepigwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Ni mastaa wawili wa Simba, Anicet Oura aliyefunga mabao 2 na Rushine de Reuck, ndio waliopeleka kilio kwa Namungo.

SOMA HII PIA: Simba SC imepangwa Kundi C CAF: RS Berkane, Orlando Pirates na Colombe Sportive

Kipindi cha kwanza Simba SC 1- 2 Namungo FC

Simba SC vs Namungo FC (-)
Simba SC vs Namungo FC 

Simba iliuanza mchezo hu kwa kasi kubwa na kufanikiwa kupata bao la uongozi dakika ya 3 tu ya mchezo. Bao hili lilifungwa na Anicet Oura aliyeunganisha kwa Kichwa mpira wa kona ambao hapo awali uliguswa na Elie Mpanzu. Kufuatia bao hilo Namungo FC waliamka na kuanza kusukuma mashambulizi ya kujibu, ili kusawazisha. Mashambulizi hayo yalizaa matunda baada ya Rymond Lulendi kuifungia Namundo mabao 2 dakika ya 35 na 43 matokeo ambayo yalisalia mpaka kipindi cha kwanza kinaisha.

SOMA HII PIA: Simba SC vs 15 de Agosto: Doumbia Day CAF Champions League | Livescore

Shinda mpaka shilingi Milioni 800 sasa, cheza kindege ‘aviator’ ya SportPesa gusa hapa chini

image
Win big with Sportpesa Aviator

Kipindi cha pili Simba SC 3-2 Namungo FC

Simba SC --- Namungo FC
Simba SC 3-2 Namungo FC

Kipindi cha pili Simba SC walikuja kwa nguvu zaidi wakisaka nafasi ya kusawazisha, lakini mambo yalikuwa magumu na ilibidi wasubiri mpaka dakika ya 79 ambapo nahodha wao Rushine aliifungia bao la Penalti. Dakika 10 baadaye Oura alirudi tena kambani kwa kuifungia Simba bao la 3 na la ushindi.

SOMA HII PIA: Simba SC ni Unbeaten NBC Premier League 2026/27 | Msimamo

Hitimisho

Matokeo ya Simba SC 3-2 Namungo FC yamempa mnyama nafasi ya kutanua zaidi pengo la pointi, dhidi ya watani zao Yanga SC na kusalia pointi 5. Simba SC sasa wamefikisha pointi 30 kileleni mwa msimamo wakifuatiwa na Yanga SC ambao wana pointi 25.  Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.