Polisi Tanzania 1-0 Geita Gold | Kiakala apiga msumari dakika za jiooni, NBC Premier League, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

Polisi Tanzania vs Geita GoldPolisi Tanzania vs Geita GoldPolisi Tanzania vs Geita Gold

Polisi Tanzania 1-0 Geita Gold | Kiakala apiga msumari dakika za jiooni, NBC Premier League, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

  • Mshambuliaji, Tariq Kiakala amefunga goli la maumivu limefungwa dakika za jiooni na kupelekea matokeo ya Polisi Tanzania FC 1-0 Geita Gold.
  • Kiakala alifunga bao hilo dakika ya 90+3 kufuatia mpira mrefu uliopigwa kwenye lango la Geita Gold, huku safu yao ya ulinzi ikijichanganya.
  • Mchezo huu ulipigwa katika Uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro 1/11/2026.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu za mchezo huu.

Tariq Kiakala mshambuliaji wa Polisi Tanzania amepeleka maumivu makali kwa Geita Gold, baada ya kuwafunga bao la dakika za jioni na kupelekea matokeo ya Polisi Tanzania FC 1-0 Geita Gold. Bao hilo lilifungwa dakika ya 90+3 kufuatia mpira mrefu uliopigwa kwenye lango la Geita Gold, huku safu yao ya ulinzi ikijichanganya. Mchezo huu ulipigwa katika Uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro Jumapili 1/11/2026.

SOMA HII PIA: Polisi Tanzania 1-0 Geita Gold FC NBC Premier League 01/11/2026 | Higlights | SportPesa Blog

Kipindi cha kwanza Polisi Tanzania 0-0 Geita Gold

Polisi Tanzania --- Geita Gold
Polisi Tanzania vs Geita Gold

Mchezo huu ulishuhudia mashambulizi mazito kwa kila timu langoni mwa wapinzani wake katika dakika za awali. Jitihada hizo hazikuweza kuzaa matunda, kwani mpaka dakika 45 zinakamilika matokeo yalisalia 0-0. Polisi Tanzania wakiwa nyumbani matokeo haya yalionekana kuwaumiza zaidi.

SOMA HII PIA: Simba SC vs Namungo FC 2/11/2026: NBC Premier League, Live score, h2h

Shinda mpaka shilingi Milioni 800 sasa, cheza kindege ‘aviator’ ya SportPesa gusa hapa chini

image
Win big with Sportpesa Aviator

Kipindi cha pili Polisi Tanzania 1-0 Geita Gold

Polisi Tanzania vs Geita Gold FC
Polisi Tanzania vs Geita Gold FC

Kipindi cha pili timu zote ziliongeza nguvu ya mashambulizi ya piganikupige, hii ni kutokana na maelekezo ya makocha wa timu hizo wakati wa mapumziko. Huku mchezo ukiaminika kuwa unaweza kuisha kwa matokeo ya sare, Polisi Tanzania walifanikiwa kupata pigo la faulo. Mpira mrefu uliopigwa moja kwa moja langoni, ulikutana na Tariq Kiakala ambaye aliusukuma langoni.

SOMA HII PIA: Polisi Tanzania: Ratiba, Matokeo na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27

Hitimisho

Matokeo ya Polisi Tanzania 1-0 Geita Gold yanaifanya polisi Tanzania kukwea mpaka nafasi ya 6 kwenye msimamo, na pointi zao 15. Geita Gold wao wanaporomoka mpaka nafasi ya 13 na pointi zao 9 walizokusanya katika mechi 11. Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.