
Bayern Munich 6-1 RB Leipzig: Luis Diaz afunga hat trick Bundesliga 2026/27
- Bayern Munich 6-1 RB Leipzig matokeo kwenye pambano kali la Bundesliga, Oktoba 17,2026.
- Luis Diaz alifunga hat trick huku bao la kufutia machozi wa RB Leipzig likifungwa na Andrija Maksimovic.
- Harry Kane alipachika bao moja timu yake ikijikita kileleni ikifikisha pointi 14 baada yakucheza mechi 6.
- Makala hii inachambua baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu za mchezo huu.
Msimu mpya wa Bundesliga unazidi kuchanja mbunga, Bayern Munich 6-1 RB Leipzig ni matokeo rasmi ya mchezo uliochezwa Oktoba 17,2026.Mabao yamefungwa na Luis Diaz dakika ya 12, 47, 69, Aleksandar Paviovic dakika ya 26, Michael Olise dakika ya 34 na Harry Kane dakika ya 53.Bao pekee la RB Leipzig limefungwaa na Andrija Maksimovic dakika ya 90+1.Pambano hili kali limepigwa Allianz Arena, Munich.
SOMA HII PIA:Brentford 1-2 Liverpool: Alexander Isak afunga bao la ushindi ugenini | Highlights
Shinda milioni 800 sasa, cheza kindege ‘aviator’ ya SportPesa gusa hapo chini
Kuna mamilioni yanakusubiri sasa hivi kwa kupaisha kindege.Huku kuna fedha nyingi kuliko kule hatukuongopii ni kweli kabisa.Bofya link hapa chini rubani uvune mkwanja wako:-

Bayern Munich 6-1 RB Leipzig
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | Bundesliga |
| Matokeo | Bayern Munich 6-1 RB Leipzig |
| Uwanja | Allianz Arena, Munich |
| Tarehe | 17/10/2026 |
| Timu mwenyeji | Bayern Munich |
Takwimu
| Kipengele | Bayern Munich | RB Leipzig |
| Mashuti | 26 | 8 |
| Mashuti yaliyolenga lango | 15 | 4 |
| Umiliki | 59% | 41% |
| Faulo | 15 | 6 |
| Kona | 11 | 3 |
| Kadi nyekundu | 0 | 0 |
| Kadi ya njano | 1 | 0 |
Msimamo
Bayern Munich wanaongoza ligi wakiwa na pointi 14 baada ya mechi 6.Vinara hawa wamepata ushindi kwenye mechi 4 sare 2 wakiwa hawajapoteza.Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 22 ikiwa inaongoza.Inafuatiwa na Dortmund ambayo ipo nafasi ya pili na pointi 14 safu ya timu hii imefunga mabao 11 baada ya mechi 6.
RB Leipzig ipo nafasi ya 7 kwenye msimamo. Imekusanya pointi 9 baada ya mechi 6.Timu hii imepata ushindi katika mechi 3ikipoteza mechi 3.Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 16.
SOMA HII PIA:Manchester City 3-2 Ipswich Town | Haaland atikisa EPL, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu
Hitimisho
Bayern Munich 6-1 RB Leipzig yamefungwa mabao 7 katika dakika 90 zilizokuwa na ushindani mkubwa.Burudani ya Bundesliga imekuwa na mvuto wa aina yake kutokana na upinzani uliopo.Bado vita ya ubingwa ni mbichi kwa kuwa msimu unazidi kushika kasi.

