Cristiano Ronaldo afunga goli la 982: Saudi Pro League Al Faisaly 1-3 Al Nasr, Highlits

Cristiano CR-Cristiano CR-Cristiano CR-

Cristiano Ronaldo afunga goli la 982: Saudi Pro League Al Faisaly 1-3 Al Nasr, Highlits

  • Ligi Kuu nchini Saudi Arabia yaani Saudi Pro League imeendelea jana Ijumaa, ambapo Cristiano Ronaldo ameendeleza moto, baada ya kufunga bao moja na bao lake la 982 katika mfululizo wa rekodi zake.
  • Bao hilo lilipatikana katika mchezo wa Al Faisaly 1-3 Al Nasr kwenye Saudi Pro League.
  • Ronaldo sasa amesalia mabao 18 tu, ili kutimiza ndoto yake ya kufunga mabao 1000
  • Makala hii inachambua kwa ufupi kumhusu Ronaldo na matokeo ya mchezo huo.

Saudi Pro League imeendelea jana Ijumaa, ambapo Cristiano Ronaldo ameendeleza moto, baada ya kufunga bao moja na bao lake la 982 katika mfululizo wa rekodi zake. Bao hilo lilipatikana katika mchezo wa Al Faisaly 1-3 Al Nasr kwenye Saudi Pro League. Ronaldo sasa amesalia mabao 18 tu, ili kutimiza ndoto yake ya kufunga mabao 1000. Makala hii inachambua kwa ufupi kumhusu Ronaldo na matokeo ya mchezo huo.

SOMA HII PIA: World Cup 2026 Top Scorers: Final Golden Boot Standings, Player Stats and Records

Cristiano Ronaldo aendelea kuandika rekodi

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo ameendelea kuandika historia katika soka la dunia baada ya kufunga bao muhimu lililoisaidia Al Nassr kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Al Faisaly. Bao hilo alilifunga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia uliochezwa Oktoba 23, 2026. Ushindi huo uliwapa Al Nassr alama tatu muhimu, katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo, bao hilo linakuwa la 982 katika maisha yake ya soka.

Mchezo ulikuwaje?

Ronaldo na mfungaji wa bao la kwanza wakishangilia
Ronaldo na mfungaji wa bao la kwanza wakishangilia

Al Nassr ilianza vizuri mchezo huo na kupata bao la kuongoza dakika ya nne kupitia Abdullah Al-Hamdan, aliyemalizia pasi ya Sadio Mané na kuipa timu yake uongozi wa mapema. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi, ambapo Ronaldo aliandika jina lake kwenye ubao wa matokeo dakika ya 49, akifunga  kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na João Félix. Bao hilo liliifanya Al Nassr kuongoza kwa mabao 2-0 na kuongeza matumaini ya kupata ushindi.

Hata hivyo, Al Faisaly haikukubali kushindwa kirahisi. Theo Bongonda aliifungia timu hiyo bao la kufutia machozi dakika ya 66, na kuifanya mechi kuwa na ushindani zaidi huku wenyeji wakitafuta bao la kusawazisha. Lakini matumaini ya Al Faisaly yalizimwa dakika ya 79, baada ya Ângelo kufunga bao la tatu la Al Nassr akimalizia pasi ya Al-Hamdan na kuhakikisha wageni wanaondoka na ushindi wa mabao 3-1.

SOMA HII ZAIDI: Ratiba ya Portugal FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika | Je, Ronaldo atabeba ubingwa?

Ronaldo aendelea kukaribia rekodi ya mabao 1,000

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo

Jambo lililovuta zaidi hisia katika mchezo huo ni bao la Ronaldo, ambalo lilikuwa la 982 katika maisha yake ya soka kwa mujibu wa rekodi rasmi za soka duniani. Hiyo inamwacha akisaliwa na mabao 18 pekee kufikia alama ya kihistoria ya mabao 1,000. Ingawa kulikuwa na mjadala kuhusu iwapo mpira huo uliguswa na beki wa Al Faisaly kabla ya kuingia wavuni, lakini Ligi Kuu ya Saudi Arabia ilimhesabu Ronaldo kuwa mfungaji wa bao hilo.

Hitimisho

Kwa matokeo hayo, Al Nassr imeendelea kuweka presha kwa wapinzani wake katika mbio za ubingwa, huku Cristiano Ronaldo akiendelea kuthibitisha kuwa bado ni mchezaji mwenye mchango mkubwa katika mafanikio ya timu yake hata akiwa na umri wa miaka 41. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.