Simba SC(6) vs (1) Mashujaa FC, NBC Premier League | 13/10/2026 | SportPesa Blog
- Ushindi mkubwa wa kwanza 2026/27 umepatikana 13/10/2026, Simba SC 6-1 Mashujaa FC.
- Mabao 7 yamefungwa katika pambano kali Uwanja wa Uhuru muda wa mapumziko ilikuwa Simba SC 2-0
- Ellie Mpanzu alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo NBC Premier League
- Makala hii inachambua kwa ufupi jinsi matokeo ya mchezo iliyokuwa, msimamo na wafungaji.
Simba SC(6) vs (1) Mashujaa FC, NBC Premier League

Simba SC iliendeleza rekodi yake ya ushindi mnono katika Ligi Kuu NBC kwa kuichapa Mashujaa FC mabao 6-1. Mchezo huu uliopigwa Oktoba 13,2026 Uwanja wa Uhuru.Ni ushindi mkubwa kwa vinara hawa wa ligi msimu wa 2026/27 wakifikisha pointi 24 kwenye msimamo.
Nyota Ellie Mpanzu ameonyesha mwendelezo wake wa ubora.Akiwa shujaa kwenye mchezo uliopita wa Kariakoo Dabi, Oktoba 10,2026 uboa uliposoma Simba SC 2-1 Yanga SC.Mchezo dhidi ya Mashujaa FC alifunga mabao mawili na kuchaguliwa kuwa nyota wa mchezo.Kiungo wa Simba SC, Yusuph Kagoma alipewa majukumu ya kuwa beki wa kati.
SOMA HII PIA:Simba SC 6-1 Mashujaa FC NBC Premier League | Highlights | Ellie Mpanzu
Bado hujashinda? Cheza na ushinde mpaka milioni 800 ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege.Rubani huku mkwanja upo wakutosha unakusubiri.Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Mwenendo wa mchezo na mabao
Tangu mwanzo wa mchezo, Simba SC ilionyesha nia ya kushambulia na kutafuta mabao ya haraka. Libase Gueye alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 16, Ellie Mpanzu alifunga mabao mawili dakika ya 33 na 58.Oura alifunga dakika ya 52, Abraham Morice dakika ya 61 na Toure dakika ya 68.Seleman Bwenzi alifunga bao pekee la kufutia machozi kwa Mashujaa FC dakika ya 63.
Wachezaji wa Simba walitumia vyema nafasi walizopata, wakipiga pasi za uhakika na kumalizia mashambulizi kwa ufanisi. Ushirikiano mzuri kati ya washambuliaji na viungo ulichangia pakubwa katika ushindi huu wa kihistoria.Nyota Hassan Dilunga wa Mashujaa FC alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 45 kwa kumchezea faulo nyota wa Simba SC.
Msimamo wa NBC Premier League
Matokeo haya yanaifanya Simba SC kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC. Ushindi wa mabao mengi pia unaimarisha tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, jambo ambalo linaweza kuwa muhimu mwishoni mwa msimu iwapo timu zitafungana pointi.Mashujaa FC ipo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 12.

Steve Barker Kocha Mkuu wa Simba SC kuhusu ushindi
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker amesema ushindi dhidi ya Mashujaa FC unatokana na kutumia nafasi vizuri.Ameongeza kuwa wachezaji wanazidi kuimarika kila wakati.Amewaomba mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi katika mechi za kitaifa na kimataifa.
“Pongezi kwa wachezaji kutokana na kutumia nafasi ambazo tunazitengeneza.Tumeona makosa katika mechi zilizopita hivyo tunazidi kufanyia kazi kwa kila mchezo.Mashabiki tunawaomba wazidi kujitokeza kwa wingi kwenye mechi zetu kitaifa na kimataifa.
SOMA HII PIA:Simba SC vs Mashujaa FC 13/10/2026: Matokeo ya mechi kuamuliwa hapa, NBC Premier League, Live score, h2h,
Hitimisho
Simba SC imecheza mchezo mmoja na Mashujaa FC kwenye NBC Premier League msimu wa 2026/27. Matokeo ya mchezo wa mzunguko wa kwanza Uwanja wa Uhuru ilikuwa Simba SC 6-1 Mashujaa FC.Ushindi huo unamfanya mnyama azidi kuongoza msimamo akiwa na pointi 24 huku Mashujaa FC nafasi ya 4 na pointi 12.

