Simba SC 2-1 Yanga SC: Kariakoo dabi Mnyama atawala kila kitu! Takwimu zote hizi hapa

ByJoel Thomas

October 11, 2026
Simba SC --- Yanga SCSimba SC --- Yanga SCSimba SC --- Yanga SC

  • Mchezo wa Kariakoo Dabi wa mkondo wa kwanza NBC Premier League umemalizika huku matokeo yakiwa Simba SC 2-1 Yanga SC.
  • Mchezo huu uliopigwa jana Jumamosi ulifanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  • Mabao ya Elie Mpanzu na Neo Maema ndiyo yaliyopeleka kilio Jangwani, huku Mpanzu akitajwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo ambao Simba walifanikiwa kuutawala kwa asilimia 100.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu za mchezo huu.

Hatimaye mchezo wa Kariakoo Dabi wa mkondo wa kwanza NBC Premier League umemalizika, huku matokeo yakiwa Simba SC 2-1 Yanga SC. Mchezo huu uliopigwa jana Jumamosi ulifanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ni mabao ya, Elie Mpanzu na Neo Maema ndiyo yaliyopeleka kilio Jangwani, huku Mpanzu akitajwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo ambao Simba walifanikiwa kuutawala kwa asilimia 100. Hizi hapa takwimu, na makala hii inachambua kwa ufupi takwimu za mchezo huu.

SOMA HII PIA: Simba SC 2-1 Yanga SC Kariakoo Dabi 2026/27 | Highlights | SportPesa Blog

Umiliki wa mpira Simba SC 62 vs Yanga SC 38

Simba SC 0-1 Yanga SC NBC Premier League
Boka vs Gueye

Simba SC ilikuwa bora katika eneo la umiliki wa mpira ambapo katika takwimu za ujumla waliweza kumiliki mpira kwa asilimia 62, dhidi ya asilimia 38 za Yanga SC. Hii ilichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio katika kujenga na kufanikisha mashambulizi. Mbinu za kocha wa Simba SC na Yanga SC zilichangia kwa kiasi kikubwa.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Yanga SC: Anayefungwa Dabi ya Kariakoo huyu hapa! Mbinu za kiufundi, ratiba, msimamo, usajili na maandalizi

Shinda mpaka milioni 800 leo, cheza kindege cha SportPesa

Screenshot ---------- ------

Nafasi zilizotengenezwa: Simba SC 14 vs Yanga SC 3

Mpaka dakika 90 zinakamilika, Simba SC ndio walikuwa vinara wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga wakifanya hivyo mara 14. Yanga SC walifanikiwa kuandikisha majaribio matatu tu. Takwimu hizi zinatoa taswira halisi ya matokeo yaliyopatikana.

Pasi Simba SC 512 vs Yanga SC 355

Simba SC 2-1 Yanga SC
Mapambano

Umiliki wa asilimia 62 walioupata Simba SC umetokana na kiwango cha pasi 512 ambazo walipiga katika mchezo huo, ambapo pasi 372 zilifika. Yanga SC waliandikisha pasi 355 tu ambapo 236 kati ya hizo zilifika. Yanga SC kwa kiasi kikubwa walionekana kucheza kwa kuzuia hali ambayo iliwahukumu.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Young Africans: Wachezaji wa kuangaliwa kwenye Dabi ya Kariakoo

Usahihi wa pasi Simba SC 72 vs Yanga SC 66

Katika mfululizo wa matukio ya utawala wa Simba SC katika mchezo wa jana, Simba SC walifanikiwa kuwa na usahihi mkubwa wa pasi. Simba SC walifanikiwa kuwa na usahihi wa pasi kwa asilimia 72. Yanga SC wao walikuwa na asilimia 66 pekee.

1UP, 2UP, 3UP haina kusubiri

Screenshot ---------- ------

Mipira ya kuingilia Simba SC 27 vs Yanga SC 12

Simba SC vs Yanga SC
Simba SC vs Yanga SC

Ndani ya dakika 90 Simba SC walikuwa bora katika kushinda mapambano ya moja kwa moja. Katika mapambano yote Simba SC walifanikiwa kushinda mapambano 27 ya mipira, huku Yanga SC wao wakifaniwa kushinda mapambano 12 tu. Hii ilifanya iwe rahisi kwa Simba kuanzisha mashambulizi mengi kupitia ‘transition’

Hitimisho

Baada ya tambo za muda mrefu za watani, hatimaye mchezo umepigwa jana Jumamosi na matokeo ni Simba SC 2-1 Yanga SC. Bila shaka kila timu imepata nafasi ya kupima kiwango chao na kuangalia nafasi za kurekebisha. Endelea kufuatilia taarifa za papo kwa hapo kupitia SportPesa Blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.