
- Oktoba Mosi 2026, Wales vs Norway UEFA Nations League
- Pambano hili litapigwa Uwanja wa Cardiff City, nyumbani kwa Wales,
- Huu ni mchezo wa 3 kwa Kundi D, Norway ipo nafasi ya 2 na pointi 3, Wales nafasi ya 4 ikiwa haijakusanya pointi
- Makala hii inachambua kwa ufupi mchezo huu.
Wales vs Norway wanakutana katika mchezo muhimu wa UEFA Nations League utakaofanyika Oktoba Mosi, 2026. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali huku timu zote zikihitaji pointi muhimu katika kampeni zao za Nations League. Mtanange huu utachezwa katika Uwanja wa Cardiff City, nyumbani kwa Wales, na unatarajiwa kuanza saa 3:45 usiku kwa Afrika Mashariki.
SOMA HII PIA: UEFA Champions League results, fixtures and table
Unaweza kuweka mkeka wako wa mechi hii Wales vs Norway kupitia SportPesa kwa kubonyeza hapa chini

Habari za timu na majeraha
Kwa upande wa Wales, Kocha Mkuu Craig Bellamy anatarajia kukosa huduma ya Harry Wilson na Joe Rodon. Anatarajiwa kufanya mabadiliko kwenye mchezo dhidi ya Norway ili kupata matokeo chanya. Josh Sheehan anatarajiwa kuanza eneo la kiungo.
Norway, Kocha Mkuu Stale Solbakken anatarajiwa kufanya mabadiliko kwa upande wa Oscar Bobb ambaye alianzia benchi walipopoteza dhidi ya Portugal. David Wolfe anarejea uwanjani lakini kuna nafasi ndogo kuanza. Wakati huohuo Alexander Sorloth hatakuwa sehemu ya kikosi. Martin Odegaard kuna matumaini kwamba atakuwa imara licha yakupata maumivu siku ya Jumapili.
Msimamo Kundi D
| Timu | Mechi | Ushindi | Pointi |
| 1. Portugal | 2 | 2 | 6 |
| 2. Norway | 2 | 1 | 3 |
| 3. Denmark | 2 | 1 | 3 |
| 4. Wales | 2 | 0 | 0 |
Takwimu za ana kwa ana (h2h) na hali ya timu
Katika mechi 3 zilizopita walipokutana Wales alipata ushindi mechi mbili. Norway ilipata ushindi mchezo mmoja.
| Tarehe | Matokeo |
| 12 Novemba 2021 | Wales 4-1 Norway |
| 6 Februari 2008 | Wales 3-0 Norway |
| 5 Septemba 2001 | Norway 3-2 Wales |
Wachezaji muhimu na mbinu
Kwa Wales, wachezaji kama vile nahodha wao na viungo muhimu watakuwa na jukumu kubwa la kuongoza mashambulizi na kuimarisha ulinzi. Mbinu yao itategemea zaidi mashambulizi ya kushtukiza na kutumia mipira mirefu.
Norway, kwa upande mwingine, wanategemea zaidi wachezaji wao wenye kasi na uwezo wa kufunga mabao. Mbinu yao inaweza kuwa ya kushambulia zaidi na kutumia uwezo wa wachezaji wao wa mbele kuleta madhara.Haaland ana rekodi zakufunga akiwa amefikisha mabao 65 na timu ya taifa.
SOMA HII PIA: Ujerumani vs Serbia UEFA Nations League | H2H | Prediction | Latest news
Utabiri na mtazamo wa wahariri
Kutokana na hali ya sasa ya timu na matokeo ya hivi karibuni, Wales wanaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kushinda mchezo huu. Norway wamekuwa wakifunga kwenye mechi ambazo wanacheza hivyo wataongeza ushindani. Ni Wales 2-1 Norway matokeo yanaweza kuwa hivi. Haya ni maoni ya mhariri sio matokeo rasmi.
Hitimisho
Ni Wales vs Norway mchezo wa hatua ya makundi ambao utapigwa leo. Wenyeji wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri. Norway, kwa upande wao, wanatafuta kuendeleza kasi yao na kujihakikishia nafasi nzuri katika kundi.

