- Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), yataendelea tena leo Jumatano.
- Leo ni zamu ya Barcelona vs Atletico Madrid pale Camp Nou, huku mabingwa watetezi PSG wakiikaribisha Liverpool nchii Ufaransa.
- Hii ni baada ya jana kushuhudia vilio na shangwe, pale mbao za matangazo zilipoonesha Real Madrid 1-2 Bayern Munich, na Sporting Lisbon 0-1 Arsenal baada ya dakika 90.
- Makala hii inachambua dondoo muhimu kuhusu mechi ya Barcelona na Atletico.
Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), itaendelea tena leo Jumatano. Mechi mbili za jana ziliisha kwa vilio na furaha, Real Madrid 1-2 Bayern Munich na Sporting Lisbon 0-1 Arsenal ndiyo yalikuwa matokeo. Leo ni zamu ya Barcelona vs Atletico Madrid pale Camp Nou, huku mabingwa watetezi PSG wakiikaribisha Liverpool nchii Ufaransa. Makala hii inachambua mechi ya Barceola na Atletico.
SOMA HII PIA: Barcelona vs Atletico Madrid: Live Score, h2h, line-up, utabiri
Je, bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mpaka milioni 800 sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Barcelona vs Atletico Madrid H2H

Timu hizi zimekutana mara 252 katika historia yao, ambapo Barcelona wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 115. Atletico Madrid wao wameshinda mechi 80, huku mechi 57 zikimalizika kwa matokeo ya sare. Vigogo hawa wanaingia katika mchezo huu wakiwa wametoka kuvaana siku 4 tu, zilizopita katika mashindano ya ligi ambapo matokeo yalikuwa Atletico 1-2 Barcelona.
Vikosi vinavyotarajiwa
Barcelona
Kipa: J Garcia
Walinzi: Kounde, Cubarsi, E Garcia, Cancelo
Viungo: Martin, Pedri, Yamal, F Lopez, Rashford
Mshambuliaji: Lewandowski
Atletico Madrid

Kipa: Oblak
Walinzi: Llorente, Le Normand, Hancko, Ruggeri
Viungo: Simeone, Koke, Baena, Lookman
Washambuliaji: Alvarez, Griezmann
Habari za timu

Barcelona wataikaribisha Atletico Madrid katika dimba la Camp Nou leo Jumatano usiku, Hii ni katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Timu hizi mbili zilipambana katika mfululizo wa mechi za La Liga Jumamosi iliyopita, ambapo Barcelona walipata ushindi wa dakika za mwisho kwa bao la, Robert Lewandowski. Ushindi ambao umeifanya Barcelona kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 7.
Barcelona wana kumbukumbu mbaya dhidi ya Atletico katika hatua hii ya Ligi ya Mabingwa, wakipoteza robo fainali ya msimu wa 2013-14 kwa mabao 2-1, na pia kufungwa 3-2 katika msimu wa 2015-16. Katika mechi nne za mwisho za Ulaya dhidi ya Atletico, Barcelona wameshinda moja tu na kufunga mabao matatu pekee. Hata hivyo, wamekuwa bora katika mechi za hivi karibuni kwa ujumla, wakishinda mechi 5 kati ya 6.
Barcelona iliwatoa Newcastle United kwa kipigo cha jumla cha mabao 8-3 katika hatua ya 16 bora, huku wakishinda 7-2 katika mchezo wa marudiano nyumbani. Mabingwa hao watetezi wa La Liga hawajapoteza mechi yoyote katika mashindano yote kwa karibu miezi miwili. Ubora wa safu yao ya ushambuliaji inaonekana kuwa tishio.
Atletico wanaingia kwenye mechi hii wakiwa wametoka kupoteza michezo mitatu mfululizo, ikiwemo mechi iliyopita dhidi ya Barcelona. Kikosi cha Diego Simeone kipo nafasi ya nne katika msimamo wa La Liga, kikiwa mbele ya Real Betis kwa pointi 12. Kwa sasa hawako kwenye mbio za ubingwa wa ligi, hivyo wanaonekana kuweka nguvu zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa na fainali ijayo ya Copa del Rey dhidi ya Real Sociedad. Atletico Madrid waliiondosha Tottenham Hotspur katika hatua ya 16 bora, ambapo walifuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-5.
SOMA HII ZAIDI: Atletico Madrid vs Barcelona – A Battle for Supremacy in La Liga
Taarifa za majeruhi
Barcelona

Mpaka sasa, Andreas Christensen, Raphinha, Frenkie de Jong na Marc Bernal wamethibitishwa kukosekana kutokana na majeraha. Hata hivyo, Ronald Araujo yuko fiti kucheza, huku Jules Kounde akitarajiwa kuanza baada ya kurejea kutoka majeraha. Straika Lewandowski anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza, wakati Marcus Rashford ana nafasi ya kuendelea kuanza upande wa kushoto.
Atletico Madrid
Kipa, Jan Oblak amerejea mazoezini pamoja na wachezaji wengine, lakini Pablo Barrios bado ni majeruhi. Julian Alvarez anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza, sambamba na Antoine Griezmann na wengine muhimu.
SOMA HII PIA: Barcelona FC- Latest news, fixtures, results, table standings, squad players, transfer news and statistics
Utabiri na hitimisho
Barcelona vs Atletico Madrid sio mechi ya kawaida, bali imebeba taswira ya vita ya ubora na rekodi. Licha ya Atletico kupoteza mchezo wa Jumamosi wa La liga, inatarajiwa itatoa ushindani mkubwa kwa kuwa hii ni nafasi ya kufika Nusu Fainali, tangu walipofanya hivyo mwaka 2017. Atletico wana uwezo wa kupata matokeo mazuri ugenini, lakini Barcelona wanaonekana kuwa na ubora wa kutosha kushinda mchezo huu, hivyo inatabiriwa ushindi kwa Barca.

