Kikosi cha StarsKikosi cha Stars
  • Leo Jumapili Machi 29, 2026 ratiba ya mashindano ya FIFA Series, ambayo ni mashindano maalum yanayoratibiwa na Shirikisho la soka Duniani FIFA itaendelea tena.
  • Baada ya kupokea kipigo cha kushangaza cha bao 1-0 kutoka kwa Liechtenstein, Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itajiuliza tena kwenye mchezo wa Macau vs Tanzania.
  • Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele. Huu ni uchambuzi mfupi kuhusu mchezo huo;

Ratiba ya mashindano ya FIFA Series, ambayo ni mashindano maalum yanayoratibiwa na Shirikisho la soka Duniani FIFA itaendelea tena leo Jumapili. Baada ya kupokea kipigo cha kushangaza cha bao 1-0 kutoka kwa Liechtenstein, Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itajiuliza tena kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Macau vs Tanzania. Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele. Huu ni uchambuzi mfupi kuhusu mchezo huo;

SOMA HII PIA: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) 2025/26, kimataifa ni Al Ahly vs Yanga SC

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Kuhusu mchezo wa Macau vs Tanzania

Huu ni mchezo wa pili kwa timu zote mbili katika mashindano haya ya FIFA Series group B Rwanda. Ikumbukwet imu zote mbili zimetoka kupoteza mechi zao za kwanza, Tanzania ikifungwa 1-0 ma Liechtenstein huku Macau wakikubali kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Aruba. Mashindano haya ya FIFA Series, yanalenga kuziandaa timu na mashindano mengine makubwa. Kwa wasiofahamu Macau ni sehemu ya Taifa la China ambayo kwa kiasi kikubwa inajisimamia kiutawala.

Macau vs Tanzania h2h

FIFA Series International Friends
FIFA Series International Friends

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuvaana na Macau kutokea barani Asia. Kwa sababu hiyo, hii ni nafasi ya kila upande kuandika historia mpya katika rekodi ya soka la kimataifa. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele Stadium uliopo Kigali, Rwanda kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba, hizi hapa timu zilizofuzu hatua ya mtoano (16 bora)

Fomu ya Tanzania katika mechi 5 zilizopita

Mwalimu vs Liechtenstein
Mwalimu vs Liechtenstein

Tanzania 0-1 Liechtenstein

Morocco 1-0 Tanzania

Tanzania 1-1 Tunisia

Uganda 1-1 Tanzania

Nigeria 2-1 Tanzania

Habari za timu

Tanzania vs Leichtestein
Tanzania kambini

Tanzania imesafiri na kikosi cha mastaa 23 kwa ajili ya mashindano hayo, mastaa hao walitajwa na Kocha mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi. Ikumbukwe Tanzania inaingia katika mashindano haya ikitoka kufanya vizuri katika mashindano ya AFCON 2025, ambapo iliandika rekodi ya kucheza hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili.

Kama ilivyo kwa mashindano ya FIFA Series, safari ya Tanzania katika mashindano hayo ya AFCON ilianza vibaya kwa kupoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Nigeria, katika mchezo wa kwanza wa mashindano hayo. Lakini vijana wa kocha Miguel Gamondi wakafanya kweli katika michezo miwili iliyosalia, ambapo walifanikiwa kuvuna pointi 2 dhidi ya Uganda na Tunisia. Hii iliwafanya kuandika rekodi ya kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo.

Kwa ujumla Tanzania haijawa katika fomu nzuri katika ujumla wa takwimu. Kipigo kutoka kwa Liechtenstein kwenye mechi iliyopita, kimewafanya waandikishe mechi zaidi ya 5 bila ushindi. Kocha Miguel Gamondi atakuwa na kazi kubwa kurejesha kasi ya vijana wake.

SOMA HII PIA: TAIFA STARS HIYO AFCON 2025, MAMA AWAPA TANO

Taarifa za majeraha

Macau vs Tanzania
Kocha Gamondi

Tanzania ilitangaza mapema kabla ya kuanza kwa mashindano haya ya FIFA Series kuwa wana changamoto kubwa ya majeraha ya baadhi ya Nyota wao muhimu wawili wa ulinzi. Tanzania inaendelea kuwakosa kiungo, Yusuph Kagoma na mlinzi wa Kati, Ibrahim Baka ambao wote ni majeruhi. Nyota mwingine ambaye ameshindwa kujiunga na kambi ni Simon Msuva kutokana na changamoto ya usafiri.

Hitimisho na Utabiri

Macau vs Tanzania ni mtihani mwingine kwa kocha mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi. Baada ya kipigo cha aibu kutoka kwa Liechtenstein, wengi wanatarajia kuona mabadiliko makubwa katika mchezo wa leo. Ni wazi mchezo hautakuwa rahisi kutokana na ukweli kwamba hakuna upande ambao unawajua vizuri wapinzani zaidi. Ni mara ya kwanza timu hizi kuvaana, ninafasi kwa kila timu kuandika historia. Dakika 90 ndizo zitatupa majibu, ikiwa Tanzania au Macau watarekebisha makosa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.