- Baada ya kuwepo kwa sintofahamu kubwa kuhusu usajili wa Mpanzu, hatimaye taarifa mpya imewashtua wengi.
- Hii ni baada ya uongozi wa Simba SC leo Jumatatu kutangaza rasmi kuwa nyota huyo amesaini mkataba wa miaka 2 kusalia Msimbazi.
- Mpanzu alihusishwa kwa muda mrefu na watani wa Jadi wa Simba SC yaani Yanga SC. Swali ni Je, ni kweli Yanga walimpelekea mkataba Mpanzu?
- Makala hii inakupitisha kwa ufupi kwenye ‘Saga’ ya Nyota huyu kama ifuatavyo;
Baada ya kuwepo kwa sintofahamu kubwa kumhusu kiungo mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu hatimaye sakata lake limefikia mwisho. Hii ni baada ya uongozi wa Simba SC leo Jumatatu kutangaza rasmi kuwa nyota huyo bado yupoyupo sana Msimbazi. Hii ni baada ya kuthibitisha kuwa mchezaji amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo.
SOMA HII PIA: Tetesi za usajili: Ellie Mpanzu, Jean Ahoua, Mzamiru Yassin kuondoka Simba SC? Orodha hii hapa
Je, wajua kuwa ‘Kindege’ cha Sportpesa kinakupa mamilioni leo?
Kumbuka unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza sasa mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Taarifa rasmi ya Simba SC kuhusu usajili wa Mpanzu
Mapema leo Jumatatu, Simba SC walichapisha taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza: “Elie Mpanzu amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia Simba SC. Pongezi nyingi kwa Rais wetu, Mohammed Dewji kwa kufanikisha kumbakisha nyota huyu wa kimataifa kutoka nchini DR Congo.”
Usichokijua kuhusu usajili wa Elie Mpanzu na kuhusishwa na Yanga SC

Hivi karibuni taarifa za uchunguzi kutoka vyanzo mbalimbali ziliripoti kuwa, Yanga walikuwa kwenye mpango thabiti wa kumtaka Mpanzu. Taarifa hiyo ilieleza kuwa, tayari mabosi wa Yanga SC walianza mpango wa kumnasa nyota huyo raia wa DR Congo. Baadhi ya machapisho mbalimbali ya viongozi wa Yanga SC waliongeza uzito wa madai hayo kupitia jumbe zao kwenye mitandao.
Kufuatia machapisho hayo, iliibuka vita ya maneno isiyo rasmi mitandaoni. Vita hii iliwahusisha baadhi ya viongozi wa Simba SC na Yanga SC, ambao walirushiana maneno. Hali hii iliwaweka kwenye sintofahamu mashabiki wa timu zote mbili juu ya nini cha kuamini.
SOMA HII ZAIDI: Ellie Mpanzu kusaini RS Berkane ama Yanga SC | Simba SC yatoa masharti mazito | Magoli na rekodi zake CAF
Semaji la Simba SC Ahmed Ally lawasha moto!

Kufuatia taarifa hiyo iliyotolewa leo, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amerusha vijembe mtandaoni akisema: “Wakati unamvizia vizia Mpanzu ili uboreshe kikosi chako, MO Dewji anapita nae asubuhi tuu, Wakati wao wanasubiri kiive ndo wale wenzao tumekula kibichi.”
Hii sio mara ya kwanza kwa, Ahmed kutuma jumbe tata kumhusu Mpanzu, mwishoni mwa mwaka jana Semaji alinukuliwa akisema: “Wapinzani wetu wamepambana sana kumpata Elie Mpanzu, wamehangaika kumrubuni kwa kumuahidi ahadi nyingi za uongo. Mbaya zaidi walidanganywa kuvunja mkataba wake ni Milioni 300. Hivyo wakapata imani ya kumpata na hapo wakaanza tambo na matangazo.”
SOMA HII PIA: YANGA YAIONYA TP MAZEMBE, MPANZU AIPA JEURI SIMBA TUNISIA
Hitimisho: Swali kubwa kwenye usajili wa Mpanzu ni hili

‘Saga’ ya usajili wa Mpanzu hatimaye imefikia tamati, baada ya kuwepo kwa sintofahamu kubwa kumhusu kiungo huyo mshambuliaji wa Simba SC. Baada ya uongozi wa Simba SC leo Jumatatu kuthibitisha staa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili, ambapo ni wazi ni kama unatuma ujumbe usemao nyota huyo bado yupoyupo sana Msimbazi. Swali sasa limebaki kuwa Je, Nyota huyo ataweza kulipa thamani ya watu waliomwamini mpaka kuelezwa anapiganiwa? Majibu yanasubiriwa uwanjani.

