- Jumapili, Machi 22,2026 Uwanja wa Meja General Isahmuyo, Simba SC vs TRA United NBC Premier.
- Simba SC na kibarua kuikabili TRA United.
- Steve Barker kavurugwa bado na matokeo ya Pamba Jiji FC.
Simba SC na kibarua kuikabili TRA United, NBC Premier League, Uwanja wa Meja General Isahmuyo. Mchezo huo unafuata wakitoka kuvurugwa vs Pamba Jiji FC kwa kufungana 1-1. Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC alibainisha walikuwa wanahitaji pointi tatu ugenini wakaambulia moja.
SOMA HII: TRA United vs Simba SC nani atashinda?/ H2H, Standings, live score
Je bado hujashinda mamilioni ya SportPesa? Cheza Aviator ushinde muda huu
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Simba SC na kibarua kuikabili TRA United, Jumapili

Baada ya safari kutoka Mwanza Simba SC na kibarua kuikabili TRA United ratiba inayofuata. Matokeo yaliyopita hayakumpendeza Barker, kazi kubwa inatarajiwa kufanyika kesho. Wapinzani wao wamebainisha watapambana kupata matokeo mazuri.
Maoni ya Steve Barker wa Simba SC
“Tumetoka kupata alama moja mchezo uliopita. Ni matokeo ambayo hayatupendezi kutokana na nafasi ambazo tulipata. Majaribio mawili hayakuwa na matokeo mazuri kwetu na tulikuwa kwenye nafasi ya kupata ushindi.
Christina Mwagala, Ofisa Habari wa TRA United maoni

“Tulikuwa na mchezo dhidi ya Simba SC nyumbani ila uliahirishwa kwa kuwa maandalizi tulifanya hakuna tatizo. Tunaendelea pale tulipoisha ili kupata matokeo mbele ya mpinzani wetu, tupo tayari kwa mchezo,”.
H2H Simba SC vs TRA United
Februari 2,2025, TRA United 0-3 Simba SC, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Agosti 18,2024- Simba SC 3-0 TRA United, Uwanja wa KMC Complex
Mei 6,2024- Simba SC 2-0 TRA United, Uwanja wa Azam Complex
Februari 6,2024- TRA United 0-4 Simba SC, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
SOMA HII: Ratiba ya Simba SC 2025/26 Machi dakika 450 za kazi/ Msimamo, matokeo

Msimamo wa Simba SC vs TRA United
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 3.Simba SC | 13 | 8 | 4 | 1 | 28 |
| 10. TRA United | 15 | 5 | 5 | 5 | 20 |
Hitimisho
Simba SC na kibarua kuikabili TRA United iliyotoka kuvuna pointi moja dhidi ya Yanga SC. Mnyama kwenye mechi mbili mfululizo aliruhusu magoli. Je nani ataibuka shujaa mchezo wa kesho?

