Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kutoka ZanzibarPedro Yanga SC
  • Pacome Zouzoua hatma yake kujulikana leo kutokana na kuumia kwenye mchezo wa CAF Champions League
  • Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kutoka Zanzibar ikitajwa kuwa dabi ngumu
  • Steve Barker Kocha Mkuu wa Simba SC kwenye mtihani mzito dhidi ya Pedro Goncalves wa Yanga SC
  • Taarifa kuhusu vikosi na presha kwa mnyama Simba SC tumekosegezea hapa

Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kutoka Zanzibar zinaeleza wageni wapo kwenye presha. Ni leo Machi Mosi 2026, Uwanja wa New Amaan Complex unaobeba mashabiki 15,000. Pedro Goncalves Kocha Mkuu wa Jangwani amebainisha Pacome Zouzoua hatma yake itafahamika leo. Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema wataingia kwa tahadhari.

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC: Pacome ashtua, msimamo, Ratiba, Moto utawaka Kariakoo Dabi ya ‘Damaro Day’

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Bado hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Sportpesa Aviator Rain Free Bets- Mil

Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kutoka Zanzibar, mnyama presha

Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kutoka Zanzibar
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC. Source: Simba SC.

Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kutoka Zanzibar zinabainisha wageni wana presha. Ni mnyama Simba SC kutokana na kufungwa katika mechi sita mfululizo za NBC Premier League. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC aliweka wazi suala hilo.

“Tunakabiliwa na presha kubwa ya mchezo na sisi Simba SC tuna msongo wa mawazo. Kutokana na matokeo mabaya ambayo tulikuwa nayo katika mechi zetu zilizopita.

“Licha ya hayo tupo tayari hii ni mechi mpya ni mechi ambayo tumejipanga kwenda kupata matokeo mazuri.Haitakuwa rahisi hata kidogo lakini tupo tayari,”.

SOMA HII: Yanga SC 1-0 Simba SC: Highlights, magoli yote, h2h – Ngao ya jamii 2025

Sportpesa Aviator Rain Free Bets- Mil

Matokeo ya mechi zilizopita

Yanga SC yaichapa 5-0 JKT Tanzania
Zimbwe Jr beki wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Namungo FC 0-1 Yanga SC

Yanga SC 5-0 JKT Tanzania

Tanzania Prisons 0-2 Simba SC

Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC

Ali Kamwe afichua siri ya kambi

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amefichua siri kwa kubainisha kuwa wamefuta matokeo yote yaliyopita.

“Tulipata ushindi kwenye mechi zilizopita hilo lipo wazi.Huu ni mchezo mpya na wachezaji wanajua kwamba wana deni kuelekea mchezo mpya kutafuta ushindi mbele ya timu bora,”.

Rekodi za mechi 10

Msimu wa 2025/26 baada ya mechi 10, Yanga SC haijapoteza. Inakutana na Simba SC iliyocheza mechi 10 ikipoteza mchezo mmoja dhidi ya Azam FC. Ingawa wenyeji wanapewa nafasi kupata ushindi dakika 90 zitakuwa na majibu kamili.

Msimamo Yanga SC vs Simba SC

 MPWDLPTS
Yanga SC1091028
3. Simba SC1072123

Yanga SC vs Simba SC kikosi cha wenyeji

Langoni

Djigui Diarra

Mabeki

Israel Mwenda

Mohamed Hussen

Dickson Job

Ibrahim Bacca

Viungo

Damaro

Maxi Nzengeli

Duke Abuya

Pacome

Okello

Mshambuliaji

Depu

Kocha Mkuu ni Pedro Goncalves, raia wa Ureno

Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa kuanza

De
Rushine beki wa Simba SC. Source: Yanga SC.

Langoni

Kassali

Mabeki

Shomari Kapombe

Kibabage

Rushine

Toure

Viungo

Yusuph Kagoma

Gueye

Loemba

Clatous Chama

Oura

Mshambuliaji

Seleman Mwalimu

Kocha Mkuu ni Steve Barker, raia wa Afrika Kusini

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC joto linazidi kupanda/ Ratiba, msimamo

Hitimisho

Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya zinaeleza kuwa kila timu imechukua tahadhari kubwa kabla ya mchezo. Mwamuzi wa kati wa mchezo ni Nassoro Mwinchui kutoka Tanga atasimamia sheria 17 za mchezo. Dakika 90 zitaamua nani atavuna pointi tatu ama watagawana pointi mojamoja.




Share this: