Yanga SC vs Simba SC NBC Premier LeagueNew Amaan
  • Nassoro Mwinchui mwamuzi wa kati Kariakoo Dabi, TPLB yataja sababu kupewa mchezo namba 54
  • Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League, Pacome kamili kuwavaa Simba SC, New Amaan Complex
  • Yanga SC 5-0 JKT Tanzania, Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC matokeo ya mechi zilizopita kabla hawajakutana.

Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League ni Machi Mosi 2026. Mwamuzi ni Nassoro Mwinchui kutoka Tanga katika Kariakoo Dabi. Yanga SC 5-0 JKT Tanzania matokeo ya mchezo uliopita huku Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC kabla ya kukutana.

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC: Pacome ashtua, msimamo, Ratiba, Moto utawaka Kariakoo Dabi ya ‘Damaro Day’

Je, unataka kushinda mamilioni ya SportPesa?

Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Aviator

Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League, nani atashinda?

Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League ni mchezo wenye presha kubwa. Wenyeji Yanga SC wanapewa nafasi kubwa kupata matokeo. Hii inatokana na mwendo wat imu hiyo.

Msimu wa 2025/26 baada ya mechi 10, Yanga SC haijapoteza. Inakutana na Simba SC iliyocheza mechi 10 ikipoteza mchezo mmoja dhidi ya Azam FC. Ingawa wenyeji wanapewa nafasi kupata ushindi dakika 90 zitakuwa na majibu kamili.

Msimamo Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League

 MPWDLPTS
Yanga SC1091028
3. Simba SC1072123

Yanga SC vs Simba SC waamuzi hawa hapa

Waamuzi Dabi
Waamuzi Dabi Machi Mosi 2026.

Mchezo wa Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League unatarajiwa kuchezwa saa 2:15 usiku. Bodi ya ligi imewatambulisha waamuzi wa mchezo huo. Orodha ipo namna hii:-

Mwamuzi wa kati

Nassoro Mwinchui

Mwamuzi msaidizi namba 1

Kassim Mpanga

Mwamuzi wa akiba

Ramadhan Kayoko

Mtathimini wa mchezo

Israel Mjuni

SOMA HII:  Yanga SC vs Simba SC joto linazidi kupanda/ Ratiba, msimamo

image

TPLB yatoa sababu za Mwinchui kupewa Dabi

Karim Boimanda Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) ametaja sababu za Mwinchui kupewa Dabi.

“Nassoro Mwinchui ni miongoni mwa waamuzi ambao waliteuliwa mwanzoni mwa msimu nakupewa hadhi ya kucheza michezo ya NBC. Kuwa miongoni mwa waamuzi wa mechi ni hadhi ya juu. Kamati ya Waamuzi ya TFF inapoona mwamuzi husika anahitajika kusimamia mchezo fulani itafanya hivyo.

“Hakuna mtu hafahamu ukubwa wa mchezo umuhimu wa mchezo kwa hiyo kamati inayoundwa na wataalamu kufikia hatua ya kumteua Mwinchui maana yake amebebeshwa kioo cha ligi.Walitathimini uwezo wake na waliona kwamba anastahili kupewa mchezo wa Yanga SC vs Simba SC,” alisema Boimanda.

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC kazini leo NBC/ Ratiba NBC Premier League na msimamo hii hapa

image

Hitimisho

Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League ni mchezo namba 54. Timu zote zimeshatia kambi Zanzibar kwa maandalizi ya mwisho. Huu ni mchezo wa kwanza kwa watani wa jadi msimu wa 2025/26.




Share this: