- Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), limemteua mkaguzi wa maadili na nidhamu kuchunguza tuhuma za kauli ya kibaguzi ‘Racism’ dhidi ya mshambuliaji wa Real Madrid, Vinícius Júnior.
- Tukio hilo kati ya Gianluca Prestianni vs Vinicius Jr limekuwa gumzo kubwa, kwenye majukwaa mbalimbali ya Habari.
- Yote hayo yalitokea wakati wa mechi ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Benfica jana Jumanne.
- Mbappe, Seedorf, Henry, Infantino ni baadhi ya watu mbalimbali maarufu kwenye medani ya soka waliojitokeza kukemea. Kwa ufupi Makala hii inaangazia tukio hilo.
Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), limemteua mkaguzi wa maadili na nidhamu kuchunguza tuhuma za kauli ya kibaguzi ‘Racism’ dhidi ya mshambuliaji wa Real Madrid, Vinícius Júnior. Tukio hilo lililowahusisha Gianluca Prestianni vs Vinicius Jr limekuwa gumzo kubwa kwenye majukwaa mbalimbali ya Habari. Yote hayo yalitokea wakati wa mechi ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Benfica, jana Jumanne. Watu mbalimbali wamejitokeza kutoa maoni yao. Kwa ufupi Makala hii inaangazia tukio hilo.
SOMA HII PIA: BARCELONA MABINGWA COPA DEL REY 2025, WAICHAPA MADRID 3-2
Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Nini kilitokea kwa Gianluca Prestianni vs Vinicius Jr?

Vinícius alifunga bao pekee katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa mtoano uliochezwa Estádio da Luz. Wakati staa huyo akishangilia bao hilo, alijihusisha na mabishano na wachezaji wa Benfica, akiwemo Gianluca Prestianni. Katika purukushani hizo Vinicius alimtuhumu kiungo huyo wa Argentina kwa kumbagua kwa misingi ya rangi.
Tukio hilo lilipelekea mchezo huo kusimamishwa kwa takribani dakika 10, baada ya mwamuzi kuanzisha itifaki ya UEFA dhidi ya ubaguzi wa rangi. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20, anaweza kufungiwa hadi mechi 10 endapo atapatikana na hatia kulingana na kanuni za nidhamu za UEFA. Mpaka sasa kila upande umeonyesha mvutano mkubwa.
SOMA HII ZAIDI: Real Madrid vs Juventus UEFA Champions League 22 Oct 2025: live score, H2H, vikosi, utabiri
Taarifa ya UEFA kuhusu Racism vs Vinicius

Mara baada ya tukio hilo, UEFA ilisema katika taarifa yake: “Mkaguzi wa Maadili na Nidhamu wa UEFA ameteuliwa kuchunguza tuhuma za tabia ya kibaguzi, wakati wa mechi ya mchujo ya hatua ya mtoano ya UEFA Champions League 2025/2026, mechi hiyo ni kati ya Club Benfica na Real Madrid CF tarehe 17 Februari 2026.”
Rais wa FIFA ashtushwa
Rais wa FIFA Gianni Infantino alisema: “Nimeshtushwa na kuhuzunishwa na tukio hilo la madai ya ubaguzi wa rangi. Nampongeza mwamuzi kwa kuanzisha itifaki ya kupinga ubaguzi wa rangi. Hakuna kabisa nafasi ya ubaguzi wa rangi katika mchezo wetu na katika jamii. Tunahitaji wadau wote husika kuchukua hatua na kuwawajibisha wanaohusika.”
Prestianni akanusha, Mbappe apigilia msumari

Prestianni, mwenye umri wa miaka 20, alikanusha tuhuma za Vinícius kupitia mitandao ya kijamii akisema kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alielewa vibaya kile anachodhani alisikia. Staa wa Madrid, Kylian Mbappé, alisema alimsikia Prestianni akimwita Vinícius ‘tumbili’ mara tano. Vyanzo mbalimbali vya ndani vimethibitisha kwamba, Vinícius yuko salama na anashukuru kwa uungwaji mkono aliopata kutoka kwa klabu yake na wachezaji wenzake.
Mbappé ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kwanza kumtetea Vinicius, alinaswa na kamera akimkabili Prestianni uwanjani muda mfupi baada ya tukio hilo. Baada ya mechi, Mbappé alisisitiza hatua zichukuliwe dhidi ya Prestianni. Kwa upande mwingine, Benfica ilidai kuwa wachezaji wa Madrid wasingeweza kusikia maneno ya kibaguzi yaliyodaiwa kutokana na kelele za uwanjani na umbali kati ya wachezaji. Nahodha wa zamani wa Benfica, Luisão alikuwa miongoni mwa waliokosoa msimamo huo wa timu ya Ureno. Benfica watamenyana tena na Madrid katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Bernabéu 25 Februari. Katika mchezo huo watahitaji kupindua meza kufuatia kipigo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza.
SOMA HII PIA: Real Madrid vs RB Leipzig: Champions League Clash Preview
Hitimisho: Thierry, Seedorf amkosoa Mourinho

Kocha wa Benfica, José Mourinho, amekosolewa na gwiji wa soka wa zamani, Clarence Seedorf pamoja na wachambuzi wengine wa televisheni. Hii ni baada ya kauli zake zilizotafsiriwa kupendekeza kwamba, Vinícius Júnior alichochea maneno ya kibaguzi kwa namna alivyosherehekea bao lake.
Mourinho alisema alizungumza na wachezaji wote wawili wakati mchezo umesimama, na kwamba hakujua nani alikuwa anasema ukweli. Alipoulizwa kama alidhani Vinícius alichochea mashabiki kwa kucheza na kucheza dansi karibu na bendera ya kona, Mourinho alisema: “Alipaswa kubebwa mabegani na wachezaji wenzake badala ya kucheza na watu 60,000 katika uwanja huu.”
Seedorf alimkosoa vikali Mourinho akisema: “Nadhani alifanya kosa kubwa kuhalalisha ubaguzi wa rangi. Hatupaswi kamwe kuhalalisha unyanyasaji wa kibaguzi.”
Gwiji wa Ufaransa na Arsenal, Thierry Henry, alisema alivunjika moyo na kauli za Mourinho na kuongeza kwamba suala la ubaguzi wa rangi, linapaswa kushughulikiwa kwa uzito bila kuhamisha mjadala. Shirika la kupinga ubaguzi ‘Kick It Out’ liliunga mkono kumkosoa Mourinho.

