- Anas Bach mfungaji pekee wa goli la ushindi ugenini dakika za jioni
- AS Far Rabat 1-0 Yanga SC CAF Champions League yaongeza vita kusaka mshindi wa pili kutinga robo fainali.
- Nani kutinga hatua ya robo fainali kati ya Yanga SC vs AS Far Rabat? Swali ambalo litajibiwa wikiendi
AS Far Rabat 1-0 Yanga SC CAF Champions League matokeo ya mwisho kabla ya kuhitimisha mechi za makundi. Februari 7,2026 Anas Bach alipachika goli hilo dakika ya 8. Ushindi huo umeishusha Yanga SC nafasi ya pili mpaka ya tatu huku ushindani wa kutinga robo fainali ukiongezeka zaidi.
SOMA HII: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League, CAF Champions League/ Live scores
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

AS Far Rabat 1-0 Yanga SC CAF Champions League kundi B lamoto

Baada ya ubao kusoma AS Far Rabat 1-0 Yanga SC CAF Champions League kundi B limekuwa lamoto. Al Ahly tayari wamekata tiketi kutinga robo fainali bado timu moja itakayofuata kutoka kundi hilo. AS Far Rabat mchezo wao wa mwisho itakuwa dhidi ya Al Ahly na Yanga SC vs Kabylie, Uwanja wa New Amaan Complex, Februari 13,2026.
Ikiwa Yanga SC atashinda anapaswa kuwa na mtaji wa magoli angalau kuanzia mawili ili asonge mbele kwa tofauti ya magoli. Ikiwa AS Far Rabat atashinda ama atapata sare yeye anakata tiketi moja kwa moja na kama akipoteza basi afungwe angalau kuanzia magoli mawili.
Chaguo la Yanga SC ni kushinda mchezo wa mwisho huku AS Far Rabat ushindi ama sare kwake ni faida. Hivyo dakika 90 za maamuzi zitatoa mshindi ambaye atatinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
SOMA HII: Matokeo ya Yanga SC CAF Champions League 2025/26/ Standings, fixture

Msimamo wa kundi B
| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Al Ahly | 5 | 2 | 3 | 0 | 9 |
| 2. AS Far | 5 | 2 | 2 | 1 | 8 |
| 3. Yanga SC | 5 | 1 | 2 | 2 | 5 |
| 4.Kabylie | 5 | 0 | 3 | 2 | 3 |
Matokeo ya Yanga SC CAF Champions League

22/11/2025 Yanga SC 1 0 AS Far Rabat
28/11/2025 JS Kabylie 0 0 Yanga SC
23/01/2026 Al Ahly 2 0 Yanga SC
31/01/2026 Yanga SC 1 1 Al Ahly
07/02/2026 AS Far Rabat 1 0 Yanga SC
Hitimisho
AS Far Rabat 1-0 Yanga SC CAF Champions League wapinzani walitumia faida ya uwanja wa nyumbani. Katika mchezo wa kwanza walipotua Tanzania, Yanga SC ilishinda kwa goli 1-0 Uwanja wa New Amaan Complex. Kundi B limekuwa moto mpaka mchezo wa mwisho itafahamika timu ya pili kutinga hatua ya fainali.

