- Shabiki mmoja wa Manchester United aitwaye, Frank Illet maarufu ‘The United Strand’ amekuwa gumzo kubwa mitandaoni.
- Hii ni baada ya shabiki huyo kupitisha siku 500 bila kunyoa nywele zake akiahidi kufanya hivyo pale tu, Man United itakaposhinda mechi 5 mfululizo.
- Sakata lake limegeuka gumzo wakati huu United wakiwa wameshinda mechi 4 mfululizo. Kama mechi ya West Ham vs Man United itaisha kwa ushindi wa United basi shabiki huyo atanyoa nywele kwa mara ya kwanza baada ya kupita zaidi ya mwaka na nusu.
- Je, unamjua shabiki huyu ni nani? Makala hii inakuletea taarifa muhimu kumhusu.
Shabiki wa Manchester United aitwaye, Frank Illet maarufu ‘The United Strand’ amekuwa gumzo kubwa mitandaoni. Ni baada ya shabiki huyo kupitisha siku 500 bila kunyoa nywele zake akiahidi kufanya hivyo, pale tu Man United itakaposhinda mechi 5 mfululizo. Sakata lake limegeuka gumzo wakati huu United wakiwa wameshinda mechi 4 mfululizo. Kama mechi ya West Ham vs Man United itaisha kwa ushindi wa United basi shabiki huyo atanyoa nywele kwa mara ya kwanza baada ya kupita zaidi ya mwaka na nusu.
SOMA HII PIA: ‘Manchester derby’ Manchester United vs Manchester City: Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Kumbuka unaweza kuwa mshindi mpya wa mamilioni ya SportPesa muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kucheza kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Frank Ilett ‘The United Strand’ ni nani? Na kwanini alitoa ahadi hiyo?
Frank Ilett ni Shabiki wa kutupwa wa Man United, ambaye hajakata nywele zake kwa takribani siku 500, baada ya kuahidi kwamba hatofanya hivyo hadi timu yake ishinde mechi 5 mfululizo.
Mnamo Oktoba 5, 2024, baada ya kipindi kirefu cha matokeo mabaya ya timu yake, shabiki wa Man United, Frank Ilett aliapa kwenye mitandao ya kijamii hatakata nywele mpaka timu ishinde mechi tano mfululizo. Akitumia jina la theunitedstrand, amefanikiwa kupata zaidi ya wafuasi milioni 1.2 kwenye Instagram kufikia tarehe 9 Februari 2026. Kadri muda ulivyoendelea na nywele zake kuendelea kukua, Frank amezidi kuwa maarufu mtandaoni, na hata kufuatiliwa na baadhi ya wachezaji wa timu.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja, baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanafahamu vizuri kuhusu tukio hilo, na wana hamu ya kumsaidia Frank.
Ushindi mmoja tu ananyoa nywele

Baada ya ushindi wa Man United kwa mabao 2-0 dhidi ya Spurs Jumamosi tarehe 7 Februari, sasa amebakiwa na ushindi mmoja tu, ili hatimaye apate nafasi ya kupunguza nywele zake. Kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick, alifanikiwa kuandikisha ushindi wa nne mfululizo tangu alipotua United mbele ya Spurs wikiendi iliyopita.
Kadi nyekundu aliyopata, Cristian Romero baada ya kumchezea vibaya Carlos Casemiro bila shaka ilisaidia United kushinda, timu ilitumia vizuri nafasi hiyo. Bryan Mbeumo alifunga bao kipindi cha kwanza, huku Bruno Fernandes akiongeza jingine kipindi cha pili na kuhakikisha pointi tatu zinapatikana. Ushindi huo ulimaanisha kuwa shabiki huyo anaweza hatimaye kupata nafasi ya kukata nywele.
SOMA HII ZAIDI: Manchester United vs West Ham: Cunha arejea, live Score, h2h, line-up, utabiri
Wachezaji wapania kumpeleka Saluni
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kiliiambia SunSport: “Wachezaji wanafurahia sana mwenendo wa sasa wa timu. Lakini pia wanajua kuhusu Frank kwa, sababu anaonekana mara kwa mara kwenye mitandao yao ya kijamii. Baadhi yao walikuwa wanataniana wakisema, Haya tumsaidie huyu jamaa akate nywele.’”
Frank alianza safari yake wakati Erik ten Hag akiwa kocha.

Shabiki huyo kutoka viunga vya Oxford ambaye anaishi Hispania, alianza safari hiyo wakati Erik ten Hag akiwa kocha. Pasipo kutarajia kocha huyo akifutwa kazi siku chache baada ya kikosi chache kuwa na mwenendo usioridhisha. Nywele ziliendelea kukua wakati kocha, Ruben Amorim alipopewa kibarua cha kuinoa timu hiyo. Angalau kwa kocha huyo wa Ureno, alijaribu na kuwahi kushinda mechi tatu mfululizo ambalo lilitokea mara moja tu.
Nywele atapeleka wapi?
Iwapo hatimaye atakata nywele, Frank amepanga kuzichangia kwa shirika la hisani la Uingereza liitwalo Little Princess Trust. Shirika hili hutoa wigi kwa watoto waliopoteza nywele, kutokana na magonjwa. Hii ni kama sehemu ya kurudisha kwa jamii.
SOMA HII PIA: Arsenal vs Manchester United EPL: Live score, h2h, lineups, utabiri, Habari za timu
Hitimisho: ‘The United Strand’ mwenyewe anasemaje?

Kufuatia hali hii, Frank ‘The United Strand’ alionekana akiwa na hamu ya kuona ushindi huo wa tano unapatikana ambapo alisema: “Carrick ndiye anaiongoza timu, nywele hizi zinaenda kukatwa hivi karibuni, West Ham ndiyo inayofuata. Nne kati ya tano zimekamilika, hii ni mara ya kwanza kufikia ushindi wa nne mfululizo tangu nilipojipa changamoto hii. Naamini safari hii itatokea! Asante sana Carrick — asante, asante, asante. Sare au kupoteza kunamaanisha safari inaanza upya.

