- Esperance Tunis dakika za jioni walikosa penati baada ya mpigaji kukosa pigo hilo
- Simba SC 2-2 Esperance Tunis CAF Champions League, Uwanja wa Mkapa
- Shomari Kapombe, Yusuph Kagoma walifungua pazia la kufunga kimataifa
- Matumaini ya mnyama kutinga hatua ya robo fainali yamefifia jumla
Licha ya wenyeji kutangulia kufunga ubao umesoma Simba SC 2-2 Esperance Tunis CAF Champions League. Ni mchezo wa hatua ya makundi Uwanja wa Mkapa, Februari Mosi 2026. Shomari Kapombe dakika ya 39 na Yusuph Kagoma dakika ya 45 walifunga magoli ya Simba SC. Kipindi cha pili dakika ya 64 kupitia kwa Aboubacar Diakite na Kouceilia dakika ya 79 wapinzani waliweka mzani sawa.
SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Simba SC 2-2 Esperance Tunis CAF Champions League mchezo ulikuaje?

Mnyama amelazimishwa sare matokeo ya Simba SC 2-2 Esperance Tunis CAF Champions League. Wababe hawa waligawana dakika 45 za mwanzo zilikuwa kwa Simba SC kufunga na kipindi cha pili Esperance Tunis. Katika dakika ya 90 mnyama alikoswa kufungwa baada ya wapinzani kukosa penati.
Msimamo wa kundi D
| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Stade Malien | 4 | 2 | 2 | 0 | 8 |
| 2. Esperance de Tunis | 4 | 1 | 3 | 0 | 6 |
| 3. Petro de Luanda | 4 | 1 | 2 | 1 | 5 |
| 4.Simba SC | 4 | 0 | 1 | 3 | 1 |
H2H
Januari 24 2026
Esperance de Tunis 1-0 Simba SC
Februari Mosi 2026
Simba SC 2-2 Esperance de Tunis
Takwimu za Simba SC vs Esperance Tunis
| Simba SC | Esperance Tunis | |
| 8 | Mashuti | 11 |
| 3 | Kipa okoa | 1 |
| 57% | Umiliki | 43% |
| 14 | Faulo | 14 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 3 | Kadi za njano | 0 |
| 4 | Kona | 1 |
| 2 | Magoli | 2 |
Kikosi cha Simba SC kilichoanza vs Esperance Tunis

Mlinda mlango
Kassali
Mabeki
Shomari Kapombe
De Reuck
Kibabage
Wilson Nangu
Viungo
Oura
Kante
Kagoma
Chama
Gueye
Kibu Dennis
Wachezaji wa akiba
Abel
Duchu
Sowah
Toure
Naby Camara
Morice Abraham
Seleman Mwalimu
Loemba
Mpanzu.
SOMA HII: Esperance Tunis 1-0 Simba SC CAF Champions Leagues/ Highlights, stats, stands

Kikosi cha Esperance Tunis
Mlinda mlango
Ben Said
Mabeki
N. Laifi
M.Ben Hmida
H.Jelassi
I. Keita
Viungo
H.Teka
A.Konate
J.Diarra
O. Ogbelu
Y.Sasse
Mshambuliaji
- Diakite
Hitimisho
Simba SC 2-2 Esperance Tunis CAF Champions League yameongeza ugumu kwa mnyama. Nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali inazidi kufifia. Rekodi inaandikwa kwa watoto wa Msimbazi kucheza mechi nne bila ushindi anga la kimataifa.

