- Baada ya vipigo vitatu mfululizo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kikosi cha Simba SC kimerudi Tanzania
- Mnyama sasa ataanza rasnmi kuijiandaa na mchezo ujao wa Simba SC vs Mashujaa FC.
- Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), utapigwa kwenye Uwanja wa Meja Generali Isamuhyo.
- Huu ni mchezo wa 2 kwenye ligi kwa kocha mpya, Steve Barker je, atashinda?
Baada ya kupokea kipigo cha tatu mfululizo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Mnyama amerejea nchini kujiandaa na mchezo ujao wa Simba SC vs Mashujaa FC. Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), utapigwa kwenye Uwanja wa Meja Generali Isamuhyo. Mchezo huu utakuwa wa pili kwenye ligi kwa kocha mpya, ikumbukwe mchezo wa kwanza alipata sare dhidi ya Mtibwa Sugar.
SOMA HII PIA: Simba SC vs Mashujaa FC, mwenye kisu kikali kula nyama dakika 90
Unataka kushinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege kupitia kampuni bora ya kubashiri ya SportPesa. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Simba SC vs Mashujaa FC
Simba SC wameonekana kuwa na uwiano mzuri mbele ya Mashujaa ambapo, wamefanikiwa kushinda mechi 4 mfululizo za karibuni. Mashujaa bado hawajafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Simba kwenye michezo ya ligi. Hivyo hii ni nafasi kwao ya kuandika historia mpya.
Fomu na matokeo ya Simba SC katika mechi 5 zilizopita

Esperance 1-0 Simba SC
Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar
Simba SC 0-2 Azam FC
Simba SC 3-0 Mbeya City
Stade Malien Bamako 2-1 Simba SC
Fomu na matokeo ya Mashujaa FC katika mechi 5 zilizopita
Young Africans 6-0 Mashujaa
Mashujaa 0-0 Coastal Union
Mashujaa 0-0 Dodoma Jiji FC
Mashujaa 1-0 Mbeya City FC
Mashujaa 1-0 Namungo FC
SOMA HII ZAIDI: Simba SC yamalizana na Mashujaa FC yaipiga nje ndani dakika 180
Kikosi tarajiwa cha Simba SC vs Mashujaa FC

Kipa: Kassali
Walinzi: Kapombe, Nangu, De Ruck, Kibabage
Viungo: Chama, Kagoma, Camara, Morice, Mpanzu
Washambuliaji: Mwalimu
Habari za timu

Mchezo huu ni kipimo kingine kwa kocha mpya, Steve Barker ambaye ataiongoza Simba katika mchezo wa pili wa ligi. Licha ya timu hiyo kutoka kupoteza mchezo uliopita kwenye ligi ya Mabingwa Afrika, wengi wameanza kuona mabadiliko ya kikosi. Simba anahitaji sana ushindi katika mchezo huu, ili kupata moral kuelekea michezo ijayo.
Mashujaa wao wanaingia katika mchezo huu wakitoka kwenye kichapo kizito cha mabao 6-0 kutoka kwa Yanga SC. Licha ya matokeo hayo, bado hii sio timu ya kubeza kwani imewahi kuifunga Simba SC mara kadhaa katika hatua za mtoano za mashindano ya kombe la Ligi. Hivyo ni lazima Simba SC wauendee mchezo huu wakiwa na tahadhari kubwa kuwa lolote linaweza kutokea.
Msimamo wa NBC Premier League wapi zilipo Simba SC na Mashujaa FC?

Mpaka sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara Simba SC wanakamatia nafasi ya 6, wakiwa wamekusanya pointi 13 katika michezo 6 waliyocheza. Kwa upande wa mashujaa wao wanakamatia nafasi ya 8 katika msimamo na pointi zao 13 sawa na Simba SC. Mashujaa amekusanya pointi hizo baada ya kucheza mechi 10.
SOMA HII PIA: Ishu ya Chama kurudi Simba SC ukweli huu hapa! Kipa mpya atambulishwa: Tetesi za usajili mpya Ligi Kuu Bara 2025/26
Hitimisho
Zipo mechi nyingi kwa mnyama lakini, Simba SC vs Mashujaa FC ni zaidi ya mchezo. Hii ni nafasi kwa Simba SC kurejesha heshima yake ndani ya ligi, ambayo imeonekana kupungua katika michezo ya siku za karibuni. Simba SC haionekani kuogofya kama ilivyokuwa hapo awali. lakini hii pia ni nafasi ya kurejesha hali ya kujiamini kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ambao Simba SC wanahitaji ushindi kwa namna yoyote.
Kwa Mashujaa nao ni nafasi ya kurekebisha makosa ya mchezo uliopita. Kipigo cha mabao 6-0 hakionekani kuwa kitu cha kuvumilika kwa mashabiki wa timu hiyo, na bila shaka wamefanyia kazi makosa yao. Utabiri wa mchezo huu ni ushindi kwa Simba licha ya kwamba watabidi wafanye kazi ya ziada kufanikisha hilo.

